MH. SAMUEL SITTA NDIYE MWENYEKITI WA KUDUMU WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ameshinda nafasi hiyo kwa kura 487 dhidi ya mpinzani wake, Mhe. Hashim Rungwe aliyepaya kura 69 kati ya kura 593 zilizopigwa, na saba kuharibika katika uchaguzi uliofanyika muda mfupi uliopita Bungeni mjini Dodoma.
Akitoa Neno la Shukrani mara baada ya kupata nafasi hiyo,Mh. Sitta amewashurukuru Wajumbe wote wa Bunge la Katiba kwa kuweza kumpa nafasi hiyo adhimu. Pia amempongeza mpinzani wake,Mh. Hashim Rungwe kwa kukubali matokeo hayo.
Wajumbe wakipiga kura
Upigaji kura ukiendelea
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimpongeza Mhe. Sitta kwa ushindi wake wa kishindo