My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, September 21, 2015

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya CHADEMA na UKAWA, Bw. Edward Lowassa

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya CHADEMA na UKAWA, Bw. Edward Lowassa ameendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais  wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Lowassa jana aliendelea na kampeni zake katika majimbo matatu ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo ni Ukonga, Kigamboni na Mbagala 
  
Jimbo la Ukonga
Akiwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tungine, Jimbo la Ukonga,Bw. Lowassa alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, CCM wataisoma namba kwani Watanzania wanahitaji mabadiliko.
  
Alisema anataka kutimiza ndoto yake ya kuondoa umaskini wa Watanzania kwani ana utashi na ataweza kuuondoa kwa nguvu zote ili kuijenga Tanzania mpya wanayoitaka wananchi.
  
"Nimeamua kugombea urais ili niweze kuwatumikia Watanzania; hivyo  naomba mniamini niijenge Tanzania mpya ili kila mtu awezekuishi kwa amani na kujituma kwenye kazi," alisema.
  
Aliongeza kuwa, akiwa rais atafanya maamuzi magumu ili kuwaonesha Watanzania maana ya mabadiliko na maendeleo yanayohitajika ambapo anayekula mlo mmoja atakula mitatu, mwenye kanga tano awe na kumi lengo ni kuijenga Tanzania yenye maendeleo.
  
Bw. Lowassa aliahidi kuondoa ushuru kwenye zana za kilimo ili kila mkulima aweze kunufaika na kuuza mazao yake mahali popote iwe ndani au nje ya nchi ili aweze kujipatia kipato cha uhakika.
  
"Serikali yangu itatoa elimu bure kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu,nawashangaa viongozi wa CCM wanaposema hawawezi kutoa elimu burewakati wao wanatembelea mashangingi ya gharama kubwa.
  
"Nilikwenda Pugu kwa daladala ili kutembelea wananchi; wakaanza kuongea kwani hizi daladala za kazi gani, mbona wao wanapandisha twiga kwenye ndege na hawasemi?" alihoji Bw. Lowassa. 
  
Alisema atahakikisha matatizo ya wananchi kama alivyoyataja mgombea ubunge wa jimbo hilo, Mwita Waitara, ambapo atayatatua ambayo ni pamoja na tatizo la ukosefu wa umeme, umaskini, huduma mbovu za afya, ukosefu wa maji pamoja na hali ngumu ya maisha. 
  
Jimbo la Kigamboni
Bw. Lowassa akiwa kwenye Jimbo la Kigamboni, alisema akiwa rais wananchi watatumia Kivuko cha Kigamboni bure na kujenga upya mji huo ili uwe mfano wa kuigwa.
  
Jimbo la Mbagala
Akiwa Jimbo la Mbagala katika Uwanja wa Zakheem, alisema ataunda Serikali maalumu ambayo itashughulikia matatizo ya wakazi wa jiji hilo na kuleta maendeleo ya haraka ambayo hayajawahi kutokea.
  
Juma Duni Haji
Naye mgombea mwenza, Bw. Juma Duni Haji, alisema mwaka huu,CCM lazima waachie Serikali watake wasitake kwani miaka 50 waliyokaa madarakani imekuwa ya dhuluma na kuwanyanyasa wananchi. 
  
Alisema baada ya kuona wanashindwa, wameanza kuleta vurugu kwakuwaambia Watanzania kutakuwepo na vurugu baada ya uchaguzi. 
  
James Mbatia
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, alisema pamoja na CCM kumpaka matope Bw. Lowassa, wataendelea kusonga mbele hadi waingie Ikulu, hivyo Rais Jakaya Kikwete na Serikali yake,waanze maandalizi ya kukabidhi Ikulu.
  
Mbowe amvaa Bulembo, Lubuva 
Akihutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Abdallah Bulembo kuwa UKAWA wataachiwa vitu vyote isipokuwa Ikulu ni ya kichochezi.
  
Alisema Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva, anatetea kauli hiyo akisema ni maneno ya kisiasa na kumtaka atoe tamko juu ya hilo kwani nchi inaweza kuwaka moto. 
  
"Mtu ambaye atashinda lazima apewe haki yake, Jaji Lubuva asifanye utani na kauli za akina Bulembo, nchi inaweza kuwaka moto, wananchi wapo tayari kwa mabadiliko hivyo wapewe haki yao,"alisema.
  
Aliongeza kuwa, NEC ilipaswa kukemea kauli za aina hiyo pamoja na kutoa tamko rasmi akitumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa UKAWA, kukubaliana na maamuzi ya viongozi wakuu wa umoja huo juu ya kusimamisha mgombea mmoja katika kila jimbo na kata.
  
"Tuko katikati ya mabadiliko hatutaki mchezo, kiongozi wa NLD, CUF, CHADEMA au NCCR-Mageuzi katika ngazi za kata na wilaya ambaye atadharau maamuzi yetu tutamfukuza," alisema. 
  
Frederick Sumaye 
Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye, alisema hali anayoiona, hakuna sababu ya CCM kubaki madarakani ambapo wanachofanya sasa ni kuwabembeleza na kuwarubuni Watanzania ili wawape kura.
  
"CCM lazima iondoke madarakani, kote tulikozunguka watu wanataka mabadiliko wakisema Oktoba 25, mwaka huu, wachukue chao kila eneo wakidai CCM ina kiburi," alisema.
  
Alisema CCM imefilisika na kuishiwa sera ndiyo maana mgombea urais wao, Dkt. Magufuli anajinadi yeye badala ya chama akitumia nembo za CHADEMA; hivyo alimtaka aache kuwadanganya Watanzania.
  
Dkt. Makongoro Mahanga
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira ambaye alitoka CCM na kuhamia upinzani, Dkt. Makongoro Mahanga, alisema Bw. Lowassa ndiye mwarobaini wa tatizo la ajira.
  
Alisema inashangaza kuona Dkt. Magufuli kudai ataanzisha mahakama ya mafisadi wakati idadi kubwa ya wagombea ubunge wa CCM wamepata nafasi hizo baada ya kutoa rushwa.

Tuesday, September 1, 2015

Wahamiaji 2 wajificha ndani ya injini

Image captionMtu aliyejificha ndani ya injini ya Gari
Mhamiaji mmoja kutoka Afrika Magharibi, alifanikiwa kuingia eneo la Ceuta nchini Uhispania kutoka Morocco, huku akiwa amejikunja ndani ya injini ya gari na mwingine akiwa amejificha nyuma ya kiti cha gari moja aina ya Mercedes-300.
Maafisa wa polisi wa Uhispania waliwapata wawili hao siku ya Jumapili wakati wa msako wao wa kawaida katika kituo cha El Tarajal, karibu na mpaka wa Morocco.
Watu hao wawili kutoka Guinea, kwanza walipewa huduma ya kwanza, kwa sababu walikuwa wamekosa hewa safi ya kupumua.
Image copyrightGetty
Image captionMtu aliyejificha ndani ya injini ya Gari
Raia wengi wa mataifa ya Afrika kujaribu kuingia Cueta kama njia moja ya kufika Ulaya.
Gari hilo linasemekana kuwa na nambari bandia ya usajili.
Polisi nchini Uhispania wanawazuilia watu wawili raia wa Morocco waliokuwa ndani ya gari hilo, wakati iliposimamishwa.
Haijabainika mtu aliyekuwa katika injini alikuwa katika hali hiyo kwa muda gani kwa sababu alikuwa akivuta hewa ya sumu.
Image captionMtu aliyejificha ndani ya injini ya Gari
Hata hivyo wahamiaji hao wawili hawakuwa na stakabadhi zozote za kuwatambulisha na kwa sasa wanachunguzwa na polisi.
Ceuta na Melilla ni himaya ndogo mbili za Uhispania karibu na pwani ya Kaskazini mwa Afrika na Uhispania imeweka ukuta mkubwa ili kuzuia wahamiaji kuingia nchini humo kinyume cha sheria.
Image copyrightBBC World Service
Image captionUkuta uliojengwa na Uhispania
Ukuta huo umewalazimisha wahamiaji wengi kutumia mbinu zingine kuingia Uhispania kama vile kuogelea hadi bandari nyakati za usiku na hata kujificha ndani ya mikoba.
Mwezi uliopita mto mmoja kutoka Morocco alifariki baada ya kukosa hewa safi ya kupumua pale nduguye alipojaribu kumsafirisha kwa mkoba wake.

Papa Francis alegeza msimamo wa Katoliki

Image copyrightAFP
Image captionPapa Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ameitikia shinikizo kutoka kwa wanawake wengi waumini wa kanisa hilo na kulegeza msimamo wa kanisa hilo kuhusu uavyaji mimba mwaka ujao wa jubilee.
Huwa ni marufuku kwa waumini wa kanisa Katoliki kuavya mimba, kitendo ambacho huchukuliwa kuwa kosa kubwa katika kanisa hilo.
Papa Francis amesema atawaruhusu mapadri kuwasamehe wanawake wanaoavya mimba na pia madaktari wanaowasaidia kutoa mimba.
Kinyume na watangulizi wake, Papa Francis, huchukulia fadhila na huruma kuwa nguzo kuu zinazozidi nyingine zote.
Image copyrightGetty
Image captionWaandamanaji nchini Marekani wakitaka serikali kuhalalisha uaviaji mimba
Papa huyo mzaliwa wa Argentina, alisema anafahamu shinikizo ambazo baadhi ya wanawake hukumbana nazo ndipo waavye mimba lakini akasema pia amekutana na wanawake wengi wanaobeba moyoni kovu la alichosema ni uamuzi wa kusikitisha na mchungu.
Ametangaza mwaka wa jubilee, ambao kawaida huhusishwa na msamaha, uadhimishwe na wakatoliki kote duniani kuanzia mwezi Desemba.
Maneno hasa aliyotumia Papa Francis yanaashiria kuwa anafahamu kuna wengi wa wanaojidai kutetea utamaduni wa kanisa hilo ambao hawatafurahishwa na uamuzi wake.
"Nimeamua," Papa Francis alisema. "Bila kujali pingamizi, kuwaruhusu mapadri kutoa msamaha wa dhambi wa kuavya mimba kwa wale wanafanya hivyo na wanaotafuta msamaha wakati wa mwaka wa jubilee."
Image copyrightGetty
Image captionRaia wa Ireland wakipinga uaviaji wa mimba

Wanariadha wa Kenya warejea nyumbani

Image captionJulius Yego akikaribishwa kwa kupewa maziwa katika uwanja wa JKIA
Mbwembwe zinaendelea katika jumba la mikutano ya Kimataifa la KICC, ambako wanariadha wa Kenya wamepokewa na kuandaliwa dhifa ya chakula cha mchana na shirikisho la mchezo wa riadha nchini Kenya AK.
Kikosi hicho kilichowasili leo asubuhi kutoka Beijing ambako kiliibuka mshindi wa mashindano ya riadha ya dunia, kililakiwa na maelfu ya wakenya na wakuu wengine wa serikali wakiongozwa na makamu wa rais William Ruto.
Akihutubia dhifa iliyoandaliwa na serikali, Ruto aliwapongeza mashujaa hao walioiweka Kenya katika nafasi ya duniani katika mashindani hayo ya riadha yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Beijing China.
Image captionMakamu wa rais akielekea kuwakaribisha wanariadha wa Kenya katika uwanja wa JKIA
Kenya imepata dhahabu saba, miongoni mwao urushaji mkuki na mita mia nne kuruka vizuizi, mashindano ambayo ni mara ya kwanza kwa Kenya kushinda medali katika mashindano ya Kimataifa.
Image captionWacheza danse waliowatumbukiza wanariadha wa Kenya
Dhahabu zingine zilinyakuliwa katika mbio za mita elfu kumi na kina dada, kwa upande wa wanaume ni mbio za mita mia nane , mita elfu tatu kuruka maji na viunzi na mita elfu moja mia tano.
Kenya pia ilinyakuwa medali sita ya fedha na tatu za shaba na kuweka rekodi hiyo ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwahi kuwa mshindi wa mashindano hayo ya riadha ya dunia.
Image captionMakamu wa rais William Ruto akiwa na mshindi wa mbio za mita 400 kuruka viunzi

BARUA PEPE ZA HILLARY CLINTON KUKAGULIWA

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bi. Hillary Clinton.
New York, Marekani
Maelfu ya kurasa za barua pepe (emails) binafsi za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bi. Hillary Clinton zilizotumwa kwa anuani binafsi ya Waziri huyo, zimewekwa wazi hii leo na idara za Usalama nchini humo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema kuwa, kati ya barua pepe hizo, 150 kati yake ni zile zinazodaiwa kuwa na taarifa muhimu na za siri za serikali ya Marekani. Hata hivyo, Bi. Clinton mwenyewe amesema kuwa barua pepe hizo alizituma kimakosa, kwa kutumia anuani binafsi kwa shughuli rasmi za kiserikali.
Shirika la Ujasusi la Marekani FBI linachunguza ili kubaini kama ni kweli barua pepe hizo zilitumwa kimakosa au la.
Tukio hili limekuwa gumzo nchini Marekani hasa wakati huu ambapo Hillary Clinton anatafuta ridhaa ya chama chake kuwania urais wa taifa hilo kubwa katika uchaguzi wa mwaka 2016.

NA BBC SWAHILI

DK. Wilbroad Slaa amesema hakuwa likizo ila aliamua kuachana na siasa

DK. Wilbroad Slaa.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), DK. Wilbroad Slaa amesema hakuwa likizo ila aliamua kuachana na siasa baada ya kutokubaliana na maamuzi ya chama chake yaliyotokea Julai 28,2015 saa 3 usiku.

-Asema lazima ajitokeze kusema na kuweka ukweli hadharani
-Asema sina tabia ya kuchengachenga nasimamia ninachokiamini
-Mengi yamesemwa na kuandikwa magazetini
-Sina ugomvi na kiongozi yoyote, maana siasa si ugomvi, sina chuki, sina hasira na mtu yeyote
-Siasa inayoongozwa na propaganda, ulaghai ni kuleta vurugu katika taifa na nimekataa hayo
yote.
-Ni kweli nilishiriki katika majadiliano tangu mwanzo
-Misingi niliyoweka ni kwamba Lowassa atangaze kuwa ameachana na chama chake na aeleze anakwenda chama gani kwanza na ajisafishe na tuhuma zake
-Asema hawezi kumsafisha mtu bila yeye kufanya hivyo
-Asema alihoji kama Lowassa anakuja Chadema kama faida au mzigo (assets au liability)
-Asema anataka mgombea mwenye uwezo, sifa na kuiongoza Chadema kuiondoa CCM.
-Kama ni assets anakuja na akina nani? vijana wa mitaani, bodaboda au watu wa aina gani? ni viongozi makini?
-Asema aliambiwa kuwa anahama na wabunge 50, wenyeviti wa mikoa 22, wenyeviti wa CCM wilaya 82.
-Sikupewa majina ya wabunge wala wenyeviti.
-Nikatakiwa kuitisha kikao nikaitisha lakini sikuwa na majibu kama Lowassa ni
Assets au Liability.
-Tangu 2004 sikuwahi kutofautina na mwenyekiti wangu bali tulitofautia kwa hilo.
- Asema aliandika barua ya kujiuzulu kwa M/kiti Prof. Safari barua ikachanwa.
-Siasa ni sayansi haitaki uongo wala ulaghai au propaganda
-Asema mke wake halipwi chochote kutoka Chadema na amekuwa akizunguka nchini kwa mshahara wa Dk. Slaa.

New