Rais
wa kwanza Mzalendo na Mpigania Uhuru wa Afrika Kusini, Nelson Mandela
‘Madiba’ akiwa ameshikilia viatu vyake ambavyo aliviacha nyumbani kwa
Mzee Nsilo Swai alipoingia Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 1962
akitokea Afrika Kusini.
Mandela
aliahidi kuvichukua viatu hivyo pindi atakaporejea Tanzania lakini
katika safari hiyo ndipo alipoishia mikoni mwa makaburu wa Afrika Kusini
na kumfunga kwa miaka 27.
Viatu
hivyo aina ya Buti vilihifadhiwa hadi alipotoka na kukabidhiwa kwa
Mandela na mjane wa Mzee Nsilo Swai, Bi Vicky Nsilo Swai (pichani kulia)
mwaka 1995 Mandela alipotoka gerzani na hatim,aye kuwa Rais wa kwanza
Mweusi wa Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment