My Web
Emmanuel
CONTACT
Saturday, September 24, 2016
Monday, April 11, 2016
Jua kilimo rahisi
Kwa wale tuishio mjini
Jitengenezee bustani ili kujipatia mboga zinazoamnika
Kwana utasave 1000 ya kila siku kununua mbonga
Pili utakuwa na uhakika wa mboga unayokula isiyo na Dawa za kubust
Wala maji machafu
Wednesday, April 6, 2016
UMUHIMU WA SHANGA ZA KIUNONI - Bi zaishanga
<iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/bU6B7WTh1aA" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>
Sunday, April 3, 2016
JIONI MAALUM KWA VIJANA MBEZI BEACH TAREHE 02-04-2016
It was A great day kwa vijana wa mbezi beach KKKT kujumuika pamoja na kubadilishana uzoifu pamoja na shuhuda mbalimbali za maisha nje ya ajira nimatumaini yangu makampuni mapya mengi yataibuka miongoni mwa vijana wa KKKT mbezi beach na tutaibua millionaires wengi sana kutoka katika Umoja wetu wa vijana.
Tuesday, March 29, 2016
UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KAMA MRADI
MAHITAJI
1. Kuku(tetea) 10 na Jogoo 01
2. Banda bora
3. Vyombo vya chakula na maji
4. Chakula bora
5. Madawa na chanjo kwajili ya magonjwa
6. Chanzo cha nishati joto na mwanga
7. Elimu na ujuzi wa malezi bora
8. Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga
9. Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa)
10. Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu
KUKU 10
Wakati wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 10 (matetea) wenye umri sawa na hawajawai kutaga hata mara moja. Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika familia bora kutegemea malengo ya mradi wako. Mfano kama lengo lako ni kuzalisha kuku wa kienyeji kwa ajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa haraka na yenye uzito mkubwa,Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi.
Ili kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao. Kuku hawa utawapata kwa bei ya chini, tena watafaa sana maana watakua na umri mmoja
JOGOO 01
Jogoo mmoja tu anatosha kuwahudumia kuku matetea yote kumi.
Hakikisha katika uchaguzi wa jogoo bora lililochangamka, rangi mzuri, upanga umesimama, macho angavu, uzito wa kutosha, rangi nzuri na uwezo mkubwa wa kuzalisha. Ni vema mfugaji akaelewa kwamba kuku wote watakaozalishwa watategemea ubora wa jogoo wake. Uwezo wa kutaga kwa kuku na upatikanaji wa mayai pia hutegemea kwa karibu ubora wa jogoo aliyechaguliwa.
BANDA BORA
Miongoni mwa mambo mhimu naya kwanza kuzingatiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji kama mradi ni maandalizi ya banda bora. Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Mfugaji anatakiwa kuandaa banda lenye ukubwa wa mita 10 kwa mita 04.
Yaani urefu uwe mita 10 na upana upana wa mita 04. Kisha kata vyumba vya mita 2 urefu na upana mita 4 kutoka katika banda lako hivyo utakuwa na jumla ya vyumba vitano vyenye ukubwa unaolingana.
Ujenzi uzingatie malighafi na vifaa vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira husika.
Mfano katika maeneo ambayo fito
zinapatikana kwa urahisi banda linaweza kuandaliwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo.
Au sehemu ambayo mabanzi hupatikana kwa urahisi basi banda laweza kujengwa kwa kutumia mabanzi.
Vifaa vya kujengea banda vizingatie pia gharama na upatikanaji wake katika eneo husika.
Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-
Sakafu: Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito
Kuta: Fito, mabanzi, mbao, nguzo mianzi,udongo, matofali, mawe, mabati na wavu
Paa: Nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati na vigae.
Wigo: Matofali, mbao, fito nguzo, mabanzi, mianzi, matete, wavu na mabati
Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari.
Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.
Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.
Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala.
Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga.
Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo vya chakula na maji.
Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa.
Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga
JINSI YA KUFANYA
Wakuze kuku wako hadi watakapofikia muda wa kutaga.
Wakianza kutetea ni kiashiria kwamba wakati wa kutaga umekaribia hivyo andaa viota kwajili ya kutagia.
Viota vinapaswa viwe na ukubwa stahiki ili kumwezesha kuku kuyafunika mayai yote vizuri wakati wa kuetamia, viota viwe vinavyozuia mayai kutawanyika, viwe mahali pakavu na safi.
Hakikisha kuku wote wanataga katika viota tofauti. Kuku anapotaga
mayai matatu unapashwa kuchukua mayai mawili na kumwachia yai moja ili kumfanya aendelee kutaga zaidi. Kuku akifikia yai la kumi na mbili anza kumwachia mayai matatu ili kumwandaa kwa kazi ya kutamia.
Kwa kufanya hivi, kuku atataga mayai 15 au zaidi na ikiwa atataga mayai 15 au chini ya hapo nakushauri utafute mayai mengine ujazilizie ili kufikisha mayai 20 kwa kila kuku. Zingatia kwamba mayai unayoyatoa kwa kila kuku, yanatunzwa sehemu salama, mahali pakavu, pasafi na penye joto la wastani.
Kuku wote wanapaswa kuanza kuetamia kwa siku moja. Ili kufanikisha hili inapasa uwe karibu na kuku wako. Kuku mmoja akianza kutamia mwekee mayai ya kuku wa kisasa au mayai mabovu ya kuku wa kienyeji. Utafanya hivi hadi kuku wako wote watakapoanza kuetamia mayai. Kuweka mayai mabovu au mayai ya kuku yaliyotumika humfanya kuku aendelee kuetamia akijua ni mayai yake.
Baada ya kuona kwamba kuku wako wote wapo tayari kwa kuetamia mayai, waandalie banda maalumu kwajili ya kuetamia yani chumba kimoja katika lile banda letu. Ninashauri kwamba chumba kwajili ya kuetamia kiwe chumba cha kwanza au cha mwisho katika mfuatano wa vyumba vya banda lako. Andaa viota bora vya kuetamia, weka mayai 20 kwa kila kiota, ikiwa hayajatimia unaweza kununua kwa wafugaji wengine ili kuifikia idadi yako.
Waamishe kuku kutoka wanapotagia na kuwaweka katika chumba ulichokiandaa kwajili ya kuetamia. Ili ufanikiwe katika zoezi hili inafaa lifanyike wakati wa usiku na unafanya katika giza. Mweke kuku katika kila kiota na asubuhi wajikute kila mmoja katika kiota chake. Wahudumie kwa chakula na maji ya kutosha.
Wakati wa usiku waongezee joto la ziada kwa kuweka jiko au ndoo ya chuma yenye chengachenga za mkaa au kama una umeme weka taa za joto.
Baada ya siku 21-25 kuku wako wataanza kuangua vifaranga.
Huu ndio wakati unaotakiwa kuwa karibu sana na kuku wako kuliko wakati wote. Watenge vifaranga mara tu baada ya kuanguliwa; waweke katika chumba chao maalumu mbali na kuku. Kama chumba cha kutamia kilikuwa cha kwanza basi vifaranga wawe chumba cha mwisho n.k
Ukishawatenga vifaranga mbali na matetea wako, wawekee tena mayai mengine 20 kila tetea, mayai ambayo utayanunua kwa wafigaji wenzako. Hakikisha kuku waliotaga hayo mayai ni wazuri, hawana magonjwa na wanauzito/ukubwa unaofaa. Mayai yote yakaguliwe vizuri ili kujua kwamba yameharibika, yana nyufa au mabovu. Kabla ya kuweka mayai mengine hakikisha chumba chako ni kisafi na viota vimesafishwa, havina wadudu na uchafu wowote. Kuku wako bila kujijua wataanza kuetamia upya mayai uliowawekea.
Ukiwawekea mayai rudia mzunguko kama nilivyokwambia awali. Baada ya siku 21 hadi 25 tena utapata vifaranga wako wengine tena.
Fuata kila hatua kama nilivyokwambia hapo awali. Lakini kwa awamu hii nashauri waache matetea wako wapumzike wala usiwapatie mayai mengine tena.
JINSI YA KULEA VIFARANGA
Ikikaribia siku ya 20 tangu ulipowawekea matetea wako mayai katika chumba cha kuetamia, andaa chumba kwa ajili ya kulea vifaranga.
Safisha kwa kuondoa uchafu na wadudu wote.
Washa taa ya joto au weka chombo cha kutoa joto katika chumba cha vifaranga nusu saa kabla huja
anza kuingiza vifaranga wako. Weka pia chakula na maji ya kutosha katika vyombo vyenye umbile na ukubwa utakaowawezesha vifaranga kuvitumia. Tandaza magazeti, maboksi, makaratasi n.k katika sakafu ya chumba hicho. Hakikisha vifaranga wako hawajikusanyi sehemu moja maana wakifanya hivyo wengi wao watakufa ili ufanikiwe katika jambo hili, banda lako liwe la mduara katika kona zake.
Weka joto la kutosha. Joto la kutosha ni lile linalowafanya vifaranga watawanyike chini ya chanzo cha joto wakati kama joto limezidi vifaranya kukimbia mbali na chanzo cha joto na ikiwa joto halitoshi vifaranga hujukusanya chini ya chanzo cha joto.
Baada ya siku 3 utawapatia chanjo ya Gumboro na siku 7 wapatie chanjo ya New Castle, utarudia tena kuwapa chanjo hii baada ya mwezi mmoja kisha utafanya hivi kila baada ya miezi mitatu mitatu
MAPATO YA MRADI WAKO
Katika uzazi wa kwanza utapata vifaranga 150 kwa wastani wa vifaranga 15 kwa kila kuku.
Tuseme haujazingatia kanuni za ufugaji za makala hii ukapata vifaranga 100 yani wastani wa vifaranga 10 kwa kila kuku. Kisha baadaye wakakua wakafa kuku 50 yani watano kwa kila kuku utakuwa na jumla ya kuku 50.
Baada ya wiki 3 utapata tena kuku tufanye kwa mahesabu kama hayo hapo juu kwa hasara utakuwa na kuku wengine 50, na kufanya jumla ya kuku 100. Ikiwa kuku wako baada ya uzao wa pili uliwapumzisha kwa miezi miwili basi mwezi wa 3 utapata tena kuku vifaranga 100 na wiki 3 baadaye utapata wengine 100. Kwa mahesabu kama hayo awali wakikuwa utakuwa na kuku wengine 100 ambao watakuwa.
Baada ya miezi 6 utakuwa na kuku wakubwa wa uzao wa kwanza 50, uzao wa pili kuku 50 na utakuwa na kuku wenye umri wa miezi mitatu 50 wa uzao wa 3 na kuku wengine 50 wa uzao wa 4.
Katika kuku 100 wa uzao wa kwanza na pili, tufanye kuku 50 wawe matetea ukijumlisha na kuku 10 ulioanza nao mradi utakuwa na matetea 60. Ikiwa kila tetea atatotoa vifaranga 10 na vikakua vitano tu, mwishoni utakuwa na kuku 300 na baada ya miezi mitatu kuku wengine 900 toka katika kutoka kwa uzao wa kwanza, wapili na watatu.
Hivyo mwaka wa pili utafunga na kuku si chini ya 1,200/= wanaotaga mayai.
Ukiuza majogoo yote 1,200/= kwa bei ya 8,000/= ili upate pesa ya kujenga miundombinu bora maana sasa utakuwa na kuku wengi wanaoendelea kuzaliana kwa kasi utapata pesa kiasi cha TZS 7,200,000/=. Sasa ongeza kuku wako wa kutaga hadi wafikie kuku 4,000 maana sasa utakuwa na pesa za kutosha kuendesha mradi wako.
Sasa ukiwa na kuku 4000 wa kienyeji wa kutaga mayai, ikiwa kuku 3000 tu watataga ukauza yai moja kwa bei ya haraka haraka ya TZS 250 tu, utapata TZS 750,000/= kwa siku ambayo sawa na TZS 22,500,000/= kwa mwezi na TZS 270,000,000/= kwa mwaka sawa sawa na 128,572 USD. Kumbuka kwamba makadilio haya niya chini sana. Ukifata kanuni zote kwa makini na maombi huku ukimtanguliza Mungu utafikia hata TZS 500,000,000/= kwa mwaka.
Kumbuka unapofanikiwa kupata mapato ya kila aina, umtolee Mungu zaka(x10%) ya mapato yako, pia ukatoe sadaka ambayo ni kubwa kuliko zaka na uwasaidie masikini na wahitaji.
Tunza kumbukumbu zako zote za fedha katika daftari maalumu kuhusu mapato na matumizi ya mradi wako. Pia hali ya kuku wako kuhusu tarehe za chanjo ya mwisho, siku walipoanza kutamia, magonjwa yanayowasumbua mara kwa mara n.k
JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA.!
1. #Mathayo.
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali kwa kutetea kanisa. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.
2. #Simoni_Zelote (Mkananayo)
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishowe akafariki.
3. #Filipo
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.
4. #Yohana (nduguye Yakobo)
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na alitolewa akiwa mzima kabisa.
Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.
5. #Simoni (Petro)
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisulubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya "X". Petro mwenyewe aliomba asulubiwa kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18)
6.#Yakobo (wa Alfayo)
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe. Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga na mawe mpaka akafa.
7. #Yakobo (mwana wa Zebedayo nduguye Yohana)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa lakini alichinjwa huko Yerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).
8. #Batholomayo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo. Alipigwa fimbo nyingi zilizochubua ngozi yake na kutengeneza vidonda. Kisha akawekewa chumvi ktk vidonda hivyo, na kuanikwa juani hadi mauti ilipomfika.
9. #Andrea
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la "X" miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri sana saa kama hii"
10. #Tomaso
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko.
11. #Yuda (Thadayo)
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.
12. #Yuda (Iskariote)
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha. Alinunua shamba kwa zile fedha alizomuuza nazo Yesu. Lakini alijinyongea kwenye shamba hilohilo. Kamba aliyojinyongea ilikatika na akaanguka na tumbo lake kupasuka na matumbo kutoka nje. Shamba lile likaitwa "Akel Dama" yani Shamba la damu (Matendo 1:18-19).
NOTE:
13. #Mathia
Ni Mwanafunzi aliyechaguliwa kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (msaliti). Alipigiwa kura na wanafunzi 11 wa Yesu baada ya kifo cha Yuda (Matendo 1:26). Huyu alipigwa na mawe hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.
14. #Paulo
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka 65 (A.D).
Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.
NB: Si muhimu kujua ni namna gani mitume walikufa, ila ni muhimu kujua kuwa mitume wote walikufa wakitetea imani yao. Walikua tayari kuchukiwa na kufa vifo vya mateso kwa ajili ya kumtetea na kumshuhudia Kristo.
Biblia imesema, "Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka." Mathayo Mtakatifu 10:23
Wednesday, March 23, 2016
MJUE NYANGUMI (WHALE)
MJUE NYANGUMI (WHALE), KIUMBE MKUBWA KULIKO WOTE TANGU DUNIA IUMBWE!
Mambo 10 sahihi kumhusu Nyangumi)
1.Nyangumi aina ya “Humpback” anaweza kula hadi tani 1 (kilo 1000) za chakula kwa siku, kila siku.
2.Watoto wa Nyangumi wa Bluu” wanazaliwa wakiwa na urefu wa mita 6 – 7, wakiwa na uzito wa tani 5.5 – 7.5. Wanakunywa lita 225 za maziwa yenye kiwango kikubwa cha mafuta kwa siku na wanaongezeka wastani wa kilo 3.7 kwa saa. Watoto hawa Nyangumi wanapofikisha miezi 8 wanakuwa na urefu wa mita 15 na tani 22.5 na wanabalehe wakiwa na umri wa miaka 10 – 15.
3.Nyangumi wa Bluu ndiye mkubwa kuliko kiumbe chochote kilichowahi kuishi duniani, anaweza kukua hadi kufikisha urefu wa mita 30 (kuzidi dege aina ya Boeing 737) na akawa na uzito wa tani 144 sawa na zaidi ya wanaume 2000 au tembo kadhaa. Nyangumi huyu ni mkubwa kushinda “Dinosaur”, mnyama aliyewahi kuishi duniani karne zilizopita.
4.Nyangumi aina ya “Sperm” ndiye mwenye ubongo mkubwa katika rekodi ya dunia ya viumbe duniani, ubongo wake unaweza kufikisha kilo 9, kichwa chake kina uwazi mkubwa ambao unatosha kupaki gari.
5.Nyangumi wote hawawezi kupumua kupitia midomo yao kwa sababu midomo imeunganishwa moka kwa moja na tumbo.
6.Ulimi wa Nyangumi wa Bluu “ulimi peke yake” unaweza kuwa na uzito sawa na tembo mmoja. Timu nzima ya mpira wa miguu inaweza kusimama juu ya ulimi huo.
7.Moyo wa Nyagumi wa Bluu una kilo 450 na mshipa mkuu wa moyo wake“Aorta” ni mkubwa kiasi kwamba mtoto anaweza kuogelea hadi mwisho.
8.Nyangumi aina ya “Southern Right” ndiye mwenye korodani “testicles” kubwa kuliko kiumbe yoyote duniani. Seti moja ya korodani zake zina uzito wa tani moja.
9.Nyangumi aitwaye “Bowhead” ambaye hutumia muda wake kwenye maji baridi ya “Arctic” ndiye huishi maisha marefu zaidi hadi kufikisha miaka 200.
10.Nyangumi wa Bluu ndiye kiumbe mwenye sauti kuliko wote waliowahi kuishi duniani. Sauti yake inaweza kufika kilomita mia kadhaa mbali na alipo. Kwa vipimo vya kisayansi vya sauti “decibels”, Sauti ya ndege aina ya JET ndiyo yenye rekodi kubwa kwa kipimo cha “decibels 140”. Nyangumi huyu tunayemuongelea hapa pia hutoa “decibels 140” ambazo zinaweza kuumiza masikio ya mwanadamu.
Subscribe to:
Posts (Atom)