My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, March 23, 2016

MJUE NYANGUMI (WHALE)





MJUE NYANGUMI (WHALE), KIUMBE MKUBWA KULIKO WOTE TANGU DUNIA IUMBWE!
Mambo 10 sahihi kumhusu Nyangumi)

1.Nyangumi aina ya “Humpback” anaweza kula hadi tani 1 (kilo 1000) za chakula kwa siku, kila siku.

2.Watoto wa Nyangumi wa Bluu” wanazaliwa wakiwa na urefu wa mita 6 – 7, wakiwa na uzito wa tani 5.5 – 7.5. Wanakunywa lita 225 za maziwa yenye kiwango kikubwa cha mafuta kwa siku na wanaongezeka wastani wa kilo 3.7 kwa saa. Watoto hawa Nyangumi wanapofikisha miezi 8 wanakuwa na urefu wa mita 15 na tani 22.5 na wanabalehe wakiwa na umri wa miaka 10 – 15.

3.Nyangumi wa Bluu ndiye mkubwa kuliko kiumbe chochote kilichowahi kuishi duniani, anaweza kukua hadi kufikisha urefu wa mita 30 (kuzidi dege aina ya Boeing 737) na akawa na uzito wa tani 144 sawa na zaidi ya wanaume 2000 au tembo kadhaa. Nyangumi huyu ni mkubwa kushinda “Dinosaur”, mnyama aliyewahi kuishi duniani karne zilizopita.

4.Nyangumi aina ya “Sperm” ndiye mwenye ubongo mkubwa katika rekodi ya dunia ya viumbe duniani, ubongo wake unaweza kufikisha kilo 9, kichwa chake kina uwazi mkubwa ambao unatosha kupaki gari.

5.Nyangumi wote hawawezi kupumua kupitia midomo yao kwa sababu midomo imeunganishwa moka kwa moja na tumbo.

6.Ulimi wa Nyangumi wa Bluu “ulimi peke yake” unaweza kuwa na uzito sawa na tembo mmoja. Timu nzima ya mpira wa miguu inaweza kusimama juu ya ulimi huo.

7.Moyo wa Nyagumi wa Bluu una kilo 450 na mshipa mkuu wa moyo wake“Aorta” ni mkubwa kiasi kwamba mtoto anaweza kuogelea hadi mwisho.

8.Nyangumi aina ya “Southern Right” ndiye mwenye korodani “testicles” kubwa kuliko kiumbe yoyote duniani. Seti moja ya korodani zake zina uzito wa tani moja.

9.Nyangumi aitwaye “Bowhead” ambaye hutumia muda wake kwenye maji baridi ya “Arctic” ndiye huishi maisha marefu zaidi hadi kufikisha miaka 200. 

10.Nyangumi wa Bluu ndiye kiumbe mwenye sauti kuliko wote waliowahi kuishi duniani. Sauti yake inaweza kufika kilomita mia kadhaa mbali na alipo. Kwa vipimo vya kisayansi vya sauti “decibels”, Sauti ya ndege aina ya JET ndiyo yenye rekodi kubwa kwa kipimo cha “decibels 140”. Nyangumi huyu tunayemuongelea hapa pia hutoa “decibels 140” ambazo zinaweza kuumiza masikio ya mwanadamu.


No comments:

Post a Comment

New