My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, March 6, 2016

HONEYMOON



Mke wangu Harusi sasa imeisha, kila mtu amesharudi kwao. Hakuna muziki tena, hakuna kwaito tena. Harusi yetu ilikuwa nzuri. Nilijitahidi kuandaa harusi ya ndoto yako. Najua ulikuwa ukiangalia sana kipindi cha chereko TBC 1. Ukatamani tuwe na harusi nzuri kuzidi zile zilizokuwa zikioneshwa. Nimejitahidi katika hilo. 

Nilichoshindwa ni kuirusha tu live. Sasa ni historia. Harusi tumemaliza ni muda wa kujenga ndoa yetu.

 Kilichobaki ni sisi wawili tu. Kila kitu kinachotarajiwa na sisi kinaanza usiku huu.

Maisha yetu hayapo kawaida sasa, kuna siku fulani ulikuwa umevaa gauni lako jekundu. Ulionekana mrembo sana siku ile. Ni siku ile ambayo nilikuona nikavutiwa nawe Maradufu. Nilipokuona tu nilitamani nikukiss, nlitamanai nikushike kwa jinsi ulivokua ukinivutia. 

Sasa nipo nawewe maisha yangu yote, naweza nikakushika muda wowote ninaohitaji pamoja na kukikiss muda wowote ule.

 Ngoja nikuambie vitu vichache. Sina kitu cha kukuficha kuanzia sasa. Simu yangu unaweza ukaitumia kama yako, unaweza ukaingia fb yangu kama kwako, twitter, Whatsapp, Instagram na kwingineko ila simu isiwe kipimo cha Mapenzi yetu. Simu imetengenezwa na Mtu ila Mapenzi yetu yameumbwa na Mungu.

Mke wangu Kuanzia leo mimi nimekuwa mtoto wako, kwa wiki moja iliyopita nilikuwa mvulana. Nilikuwa nikiamka mwenyewe asubuhi, muda mwingine nililala na njaa. Hizi zote zilikuwa changamoto za maisha. Nilirudi gheto kwangu muda wowote niliojisikia. Na sikuwa na mshauri wa karibu mtu wa ku share nae siri zangu. Lakini vyote vimeisha kuanzia sasa.

Nisikie mke wangu Kuanzia leo wewe ni mama yangu, utakayeniuliza kama nitachelewa kurudi nyumbani bila sababu ya msingi, mama yangu utakae niamsha asubuhi saa kumi na mbili niwahi kazini, mama yangu utakae hakikisha silali na njaa. Ninajivunia kuwa na mama mwingine hivi sasa.

Ni matumaini yangu kuwa utakuwa mama mzuri kwangu. Usiwe na hasira sana na mimi nakuahidi ntakuwa mwema kwako. Usinichunguze sana maana huko mbeleni utaanza kujenga taswira ambazo hazipo zikaja kuleta ugomvi kati yetu. Najua muda mwingine nitakusababishia maumivu ya kichwa ila nakuahidi nitakuwa mfumbuzi wa hayo maumivu ya kichwa pia.

Mke wangu sikiliza Baba yangu Alipofariki, mimi ndio nilikuwa mwangalizi wwadogo zangu. kama baba kwao. Hivyo sioni kama kutakuwa na tabu yoyote mimi kuwa baba yako.

Tujenge taasisi yetu sasa...,


No comments:

Post a Comment

New