Ndege aina ya Cessna  5H-QTT  ikiwa imeanguka eneo la Kisongo,  karibu 
na Uwanja wa Ndege Arusha  juzi jioni, baada ya kugonga mti wakati 
ikijiandaa kutua  na kusababisha kifo cha mmiliki wake na aliyekuwa 
rubani, Bob Sambeke(katika picha ndogo juu).
Huu ni msiba wa tatu katika muda wa mwezi mmoja 
kwani mwishoni mwa mwezi jana, Wakili na Mfanyabiashara maarufu mkoani 
Arusha, Nyaga Mawalla alifariki dunia, ikiwa ni siku moja tagu kufariki 
ghafla kwa mfanyabiashara mwingine wa madini wa mkoani humo
Arusha/Moshi. 
Kwa mara nyingine, Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha imetikiswa, kutokana na kifo cha mfanyabiashara maarufu katika mikoa hiyo, Joseph Sambeke (49) maarufu kama Bob Sambeke.
Kwa mara nyingine, Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha imetikiswa, kutokana na kifo cha mfanyabiashara maarufu katika mikoa hiyo, Joseph Sambeke (49) maarufu kama Bob Sambeke.
Bob Sambeke alifariki dunia juzi jioni baada ya 
kuanguka na ndege ndogo aliyokuwa akiiendesha, kilomita moja kutoka 
Uwanja wa Ndege wa Arusha wakati akitokea mkoani Kilimanjaro.
Huu ni msiba wa tatu katika muda wa mwezi mmoja 
kwani mwishoni mwa mwezi jana, Wakili na Mfanyabiashara maarufu mkoani 
Arusha, Nyaga Mawalla alifariki dunia, ikiwa ni siku moja tagu kufariki 
ghafla kwa mfanyabiashara mwingine wa madini wa mkoani humo, Henry 
Nyiti.
Ndege ya Sambeke aina ya MT 7- namba 5H-QTT 
ilianguka saa 12.34 jioni baada ya bawa lake kugonga mti katika eneo la 
Magereza linalopakana na uwanja huo.
Alijeruhiwa na baadaye alifariki akiwa njiani 
wakati akiwahishwa hospitalini na askari wa Magereza ambao wanaishi 
katika kambi alipoanguka. Mazishi yake yamepangwa kufanyika Alhamisi 
eneo la Karanga, Moshi.
Meneja wa Uwanja wa Ndege Arusha, Ester Dede 
alithibitisha jana kutokea kwa ajali hiyo, na kueleza kuwa taarifa za 
awali zinaonyesha ndege hiyo ni mali ya marehemu Mawalla ambaye alikuwa 
mbia wa biashara na Bob Sambeki na imesajiliwa kupitia Kampuni ya 
Quality Tours & Travellers.
Hata hivyo, Wakili Alex Msando, ambaye pia alikuwa
 mshirika wa Mawalla, aliliambia gazeti hili kuwa Sambeke alikuwa 
ameinunua ndege hiyo kutoka kwa marehemu.
Dede alisema ndege hiyo, ilianguka mita 200 kutoka
 njia namba 8 ya kuruka ndege katika uwanja huo ikitokea Kilimanjaro, 
katika dakika 15 za muda wa nyongeza wa matumizi ya uwanja huo.
Alisema ndege hiyo ikiongozwa na rubani Bob 
Sambeki ina uwezo wa kubeba watu wanne akiwamo rubani. Baadhi ya 
walioshuhudia tukio hilo, walisema kabla ya kuanguka ndege hiyo, ilikuwa
 ikiyumba na iligonga mti mkubwa katika moja ya mabawa yake na kupoteza 
mwelekeo.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Julias Laizer 
alisema kwamba aliona ndege hiyo ikigonga mti na kuyumba, kisha 
kudondoka chini na ndipo askari wa magereza walipojitokeza kutoa msaada.
 Laizer alisema Sambeki alikuwa peke yake na alijeruhiwa kichwani.
 
No comments:
Post a Comment