Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa wamesema “hawatakubali wala kuvumilia” hujuma dhidi ya chama chao.
Dar es Salaam.
Viongozi hao kwa nyakati tofauti jana walisema hujuma hizo zimekuwa zikifanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Serikali ambayo imekuwa ikitumia vyombo vya dola na kwamba sasa wanapanga ugaidi wa kuwateka maofisa wa ngazi ya juu wa Chadema.
Viongozi hao kwa nyakati tofauti jana walisema hujuma hizo zimekuwa zikifanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Serikali ambayo imekuwa ikitumia vyombo vya dola na kwamba sasa wanapanga ugaidi wa kuwateka maofisa wa ngazi ya juu wa Chadema.
Suala la ugaidi liliibuka kwa nguvu katika wiki ya
kwanza ya Bunge la Bajeti na sasa limehamia nje ya chombo hicho cha
kutunga sheria kutokana na Chadema kuwatuhumu CCM na Serikali yake
kwamba wanapanga njama za kuwateka maofisa wakuu wa chama hicho.
Jana Dk Slaa alipokuwa akimkaribisha Mbowe
kufungua Mkutano wa Mafunzo na Mipango ya Vuguvugu la Mabadiliko ‘M4C’
na Kongamano la Katiba Mpya kwa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, alisema
taarifa walizonazo zinaonyesha kuwa CCM ndiyo wanaofanya vitendo vya
kigaidi wakishirikiana na Serikali.
“Tuna taarifa zote zinazoonyesha kwamba CCM ndiyo
magaidi wakishirikiana na Serikali yake, lakini sisi tuko makini kuliko
hata Serikali ya CCM na tuko makini kuliko hata Usalama wa Taifa na
umakini huu ndiyo utakaotupeleka Ikulu mwaka 2015,”alisema Dk Slaa.
Hata hivyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,
Nape Nnauye alipotafutwa kujibu tuhuma hizo alisema hakuna jipya ambalo
Chadema wamelisema.
“Kuna jipya katika hilo, ni yale yale ya kawaida
na jana (juzi) Mwingulu alizungumza vizuri sana bungeni. Hiyo ni sawa na
mchawi anapomwangia mtu na kufa anakuwa wa kwanza kwenda kulia msibani,
nchi siku yoyotete haijengwi kwa ngonjera za maneno bali inajengwa kwa
mipango,”alisema Nape.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,
Pereira Ame Silima alipotakiwa kutoa msimamo wa Serikali juu ya tuhuma
hizo alisema, “Mimi siwezi kuzungumza ila mtafute Waziri (Dk Emmanuel
Nchimbi),”alisema Silima.
Alipotafutwa Dk Nchimbi kupitia simu yake ya mkononi, ilikuwa ikiita bila kupokewa.
Alipotafutwa Dk Nchimbi kupitia simu yake ya mkononi, ilikuwa ikiita bila kupokewa.
Kauli ya Mbowe
Kwa upande wake Mbowe alisema, CCM imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha inakisambaratisha chama hicho bila mafanikio.
Kwa upande wake Mbowe alisema, CCM imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha inakisambaratisha chama hicho bila mafanikio.
“Watu wa Usalama wa Taifa wakishirikiana na CCM
wamekuwa wakifanya mipango ya kutaka kuwateka maofisa wetu. Hawa watu ni
wepesi sana na msiwaogope hata kidogo,”alisema Mbowe huku akishangiliwa
na wanachama na makada waliofurika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue
Pearl.
Mbowe alisema: “Ukiona chama chochote tawala
kinatumia jeshi la polisi kutengeneza ushahidi wowote wa kihalifu hiyo
ni dalili ya hatari kwa mustakabali wa usalama wa nchi.”
Mbowe alisema mbinu za sasa za CCM zinatokana na kushindwa kukivuruga chama hicho kwa propaganda kuwa ni chama cha familia, ukabila, ukanda na baadaye udini.
Katiba na ElimuMbowe alisema mbinu za sasa za CCM zinatokana na kushindwa kukivuruga chama hicho kwa propaganda kuwa ni chama cha familia, ukabila, ukanda na baadaye udini.
Kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, Mbowe alisema ikiwa itafika Aprili 30 mwaka huu bila hatua zozote kuchukuliwa, watamwamuru mjumbe wa tume hiyo kutoka Chadema, Profesa Mwesiga Baregu kujiondoa
No comments:
Post a Comment