My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, September 30, 2013

DAWA DAWA KWA WALE VIJANA WA KIUME WANAOPENDA KUJICHUA....!! HAYA NDIYO MADHARA YAKE NA TIBA YAKE NI HII HAPA..!!




PILIPILI 
Punyeto ( kwa wanaume ) ni kitendo cha mwanaume, kujifikisha mwenyewe kileleni kwa kujichua uume hadi kumwaga mbegu za kiume.   Uchunguzi unaonyesha katika watu wa jinsia ya kiume kumi wenye umri wa kuanzia miaka 16 hadi 45, angalau wanne kati yao wamewahi kupiga punyeto katika kipindi fulani cha maisha yao, na wawili kati yao wanajihusisha na upigaji punyeto.  Uzoefu unaonyesha, asilimia kubwa ya wanaume wanao piga punyeto huanza katika umri wa kubalehe ( miaka 14-16 ), wengine huachana na tabia hiyo mara baada ya kupata wapenzi wa kike ama kuoa na wengine huendelea na tabia hiyo hata baada ya kuoa 


 Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekondari  za  bweni  za  wavulana  tu ), kujiepusha  na  hatari  ya  kupata  maambukizi  ya  v.v.u  nakadhalika          ATHARI  ZA  PUNYETO    KWA WAVULANA.

Punyeto  ina  athari  nyingi  na  kubwa  sana  kwa  wanaume  wanao  jihusisha  nayo, lakini  kwa  leo, tutaangalia  athari  moja  kubwa  kati  ya  nyingi. Athari  hii  si  nyingine  bali  na  KUUA  NGUVU  ZA  KIUME.  Mwanaume  anayepiga  punyeto  hutumia  nguvu  nyingi  kuibana  mishipa  inayo  fanya  uume  usimame. 
 

Mwisho  wa  siku  uume  hulegea  na  kusinyaa, na  kukosa  nguvu  kabisa  na  hatimaye  mhusika  kuwa  khanithi. Uchunguzi  unaoonyesha, kuna  idadi  kubwa  sana  ya  wanaume  wanao  sumbuliwa  na  tatizo  la  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  kama  matokeo  ya  kupiga  punyeto  kwa  muda  mrefu. Athari  za  mwanaume  kutokuwa  na  nguvu  za  kiume, nadhani  zinajulikana, ila  kwa  faida  ya  wote  tutazizungumzia  kwa  kina  siku  za  mbele, lakini  kwa  ufupi  ni  aibu  kubwa  sana   kwa  mwanaume  kukubali  kuua  ufanisi  wa  uume  wake  kwa  sababu  ya  kupiga  punyeto.

Sunday, September 22, 2013

Blackberry Yatibitisha: BBM sasa kuanza kupatikana kwenye sim za Android na Iphone

HAPPINESS WATIMANYWA NDIYE REDD'S MISS TANZANIA 2013



Redd's Miss Tanzania 2013,Happiness Watimanywa akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa mwaka huu.Kushoto ni mshindi wa pili,Latifa Mohamed na kushoto ni mshindi wa tatu,Clara Bayo.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa Onyesho la Taifa la Urembo linalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Sunday, September 1, 2013

dhana-mbaya-zinazowarudisha-watu-wengi

Watu wengi wana mitazamo mibaya wanayodhani ni sahihi lakini sio kweli, tafakari haya mambo niliyooredhesha hapo chini. Kudhani hivyo kama watu wengine wanavyofikiri kunaweza kukufanya usifanye mambo yako kwa kiuhalisia zaidi na kukupelekea usipate matunda mazuri kama unavyotegemea. 
1. Kuwa busy ni kufanya kazi nyingi kwa siku.
-Kutingwa na mambo mengi  hakumaanishi ndio unafanya kazi  kwa tija. Watu wengi hudhani kuwa busy sana ndio kupata mafanikio lakini hebu fikiria hili ‘’You Might Be Busy For Nothing Instead Of Something.’’ Ninachomaanisha hapa ni kwamba sio lazima ukiwa busy ndio kuwa utafanikiwa au kupata matokeo mazuri, unachotakiwa ni kujipanga vyema na kujua nini unafanya. Jishughulishe kwa malengo kwa kujua zao la kazi zako ni nini.

2. Kuwa jasiri ni kutoogopa.
-Ni muhimu uwe jasiri lakini sio kila kitu ni cha kukiwekea kifua mbele pasipo kufikiri. Tumeona watu wengi wameumia kwenye mambo ya hatari au hata kuharibu mambo mbalimbali katika maisha yao kama kuvunjika kwa mahusiano kwaajili ya kukomalia mambo yasiyo ya msingi, kuhatarisha maisha kwa kujifanya huogopi hata kama ni kitu hatari na mambo mengine ya kukuletea hasara. Kuwa imara na mwenye msimamo kwenye mambo mazuri na yenye faida pia ogopa vya kuogopwa na sio kila kitu ni cha kuogopa. ''Fear fear, and not everything have to be feared.''

3. Kuwa shupavu ni kuvumilia pasipo kuumia.
-Kuna mambo mengine ambayo yakikuumiza lazima uonyeshe kuwa umeumia. Tena haswa sisi wanaume mara nyingi huwa tunajifanya hatujaumia hata kama ni kweli tumeumizwa. Kuonyesha kuwa umepatwa na maswahibu haimaanishi kuwa wewe ni bwege au ni mnyonge bali wakati mwingine ina maanisha kuwa wewe ni shupavu kwa kukubali matatizo yaliyokukumba. Ukijisikia kulia ni vyema ukalia ukayamaliza kuliko kukaa nayo moyoni na kuteseka nayo bila sababu. Siku zote kuwa mkweli kwa furaha na majonzi yako kwa kueleza chochote kilichopo ndani mwako. ''Be open to your happiness and sadness.''

4. Kuamua kuwa utajisikia furaha pale tu utakapofanikiwa kupata vitu fulani kwa watu wengine.
-Huwezi kukimbia matatizo, na si vyema uwe mpweke na mwenye majonzi wakati wote kwa sababu ya matatizo. Usihuzunike leo ukitegemea utakapopata kesho kitu fulani ndio utafurahi. Ukifanya hivyo utakuwa unajidhulumu maisha yako, kuwa na furaha kulingana na hali yako au chochote ulichonacho hata kama ni kidogo. Muhimu hapo ni kuwa mvumilivu, mtafutaji na mwenye imani kuwa utafanikiwa utakacho.

5. Kuamini umechelewa kwa kila jambo unaloona sio wakati wake.
-Kuna msemo unaosema ‘’It’s Never Too Late’’ nami naamini hivyo kwasababu kwa kila jambo unalokosea leo kuna nafasi nyingine ya wewe kurekebisha mambo yako na kuyaweka vizuri kama unavyotaka. Hebu fikiri kama ungekuwa na siku ya leo tu pasipo kuwa na kesho ungefanya nini? Lakini kwa bahati nzuri una kila sababu ya kuona hujachelewa kufanya mambo yako kwasababu kama umeshindwa leo basi jiandae vizuri kesho utaweza. JipangeWeka nia na Tekeleza utakalo.

6. Kutegemea kuwa utajisikia amani pale muda mzuri utakapowadia.
-Kama huna amani sasa hivi usitegemee utakuwa mwenye amani hapo baadae. Amani huletwa na wewe mwenyewe kwa kutuliza moyo wako. Usifanye muda kukupangia amani yako bali kuwa na imani mambo yatakuwa vizuri tu maana hata ukifikiri vibaya utajiumiza bure pasipo kuwa na maana. Hakuna muda mzuri wala mbaya bali kuna hali nzuri na hali mbaya, na kiukweli  kabisa hakuna hali ya kudumu, kama una hali mbaya leo haitadumu milele ikiwa utaamua kubadilisha mambo. Muda mzuri utawadia iwapo utaamua kubadilsha hali yako kwa kutatua shida zako. Ufumbuzi wa shida zako ndio amani na furaha yako na sio muda kama watu wanavyodhani.
- See more at: http://www.kamotta.blogspot.com/2013/07/dhana-mbaya-zinazowarudisha-watu-wengi.html#.UiJ2YL_4JSp

Pata sababu kumi (10) za wewe kuwa jasiri



Sababu kumi (10) za wewe kuwa jasiri.


Kuwa jasiri ni ule uwezo wa mtu kutenda jambo fulani pasi na uoga. Ujasiri humfanya mtu kutekeleza na kufanikisha mambo yake.

UJASIRI + NIA + KUTEKELEZA = MAFANIKIO.

''This is Jules founder of The Confidence Garden, she is a coach, speaker, trainer and author here explaining to you how to build and gain confidence.''



 Kama mtu atakosa ujasiri ni vigumu kwake kufanikiwa labda angalau afanye jitihada za kufanya jambo alilokusudia ili afanikiwe. Hii ni sawa na mu anayetaka kufika mahali fulani, mtu huyo hawezi fika anapokusudia mpaka aondoke na kwenda mwenyewe anapopataka.
Kwa kuwa kukosa ujasiri kunamfanya mtu ashindwe kutenda na kufanikiwa atakalo zifuatazo ni sababu za wewe kuwa jasiri ambazo zitakupelekea wewe kufanikiwa.

1. Ujasiri humfanya mtu atekeleza mambo yake.
Watu jasiri hutenda na kufanikisha watakalo, hawaoni aibu kufanya mambo yao ikiwa wapo sahihi na lile wafanyalo.

 2. Ujasiri humfanya mtu kujisimamia mambo yake mwenyewe bila uoga.
Kwa kuwa na ujasiri unaweza kusimama kidete kwa lile unaloona ni sahihi na unapaswa ni kulisimamia. Lahasha ukiwa jasiri huwezi kudhuliumiwa au kuonewa kwa kuwa utasimamia haki yako.

3. Ujasiri humfanya mtu aweze kusema hapana.
Neno HAPANA, ni rahisi kwa mtu mwenye ujasiri kusema SITAKI pale panapobidi kukataa.


 4. Ujasiri humfanya mtu aweze kusema ndiyo.
-Neno NDIYO pia hutumika na mtu jasiri pale anapokubaliana na jambo fulani au penye fursa kila inapojitokeza. Mtu jasiri haoni aibu kusema’’ NDIYO’’ pale anapotaka kitu chochote.


 5. Ujasiri humfanya mtu kutokuwa na uoga.
-Kukosa ujasiri kunaweza kumfanya mtu ashindwe au kufeli mtihani wowote wa maisha. Mtu kuogopa kushindwa , mtu kufikiri hawezi kufanya jambo lolote akafanikiwa ni sababu kubwa ya watu wengi kushindwa kufanikiwa . Uoga huondolewa kwa mtu kuwa jasiri.

6. Ujasiri humfanya mtu ajiamini.
-Kujiamini ni silaha kubwa ya kukusaidia kutenda mambo yanayokuletea mafanikio. Henry Fordmwanzilishi wa kampuni Ford Motors alisema ‘’Whether You Think You Can, Or You Think You Can’t - You’re Right.’’


 7. Ujasiri humfanya mtu ajiwekee malengo ya juu kimafanikio.
-Watu jasiri hujiamini na kutegemea matokeo makubwa kwa kuwa wanajiamini kwa yale wanayoyafanya. Hata wewe ukijiwekea mategemeo makubwa na kuweka jitihada nyingi kwa kitu unachotaka kufanikiwa utapata kile kikubwa ulichotegemea.

8. Ujasiri humfanya  mtu kutenda mambo makubwa kuvuka mipaka ya uwezo wake.
-Ujasiri hukufanya ujue mipaka  ya  uwezo wako na kutenda mambo kwa kadri unavyoweza. ‘’You’re Stronger Than You Think, By Stretching Your Limits You Can Increase Them To Your Maximam Level.”


 9. Ujasiri humfanya mtu ajiamini kuwa atashinda.
-Mtu jasiri huamini kuwa atashinda , huu ni ukweli kuwa washindi hutegemea kufanikiwa kwa kuwa wamejianda kushinda na hupata ushindi kwasababu wanastahili kupata walichokusudia. Matokeo mazuri hutegemea ulichopanda. Hakuna ushindi au mafanikio ya kubahatisha kama una ndoto za kufanikiwa anza leo kujiwekea malengo.


10. Ujasiri humfanya mtu aulize maswali au ajieleze anachotaka.
-Ukiwa na ujasiri unaweza kujieleza mwenyewe kwa mtu/watu unachotaka na wakakusikiliza. Ukweli wa maisha ni kwamba huwezi pata chochote bila kuuliza au kuomba upewe. Mfano: Unataka kazi sharti uombe, ukitaka msaada omba usaidiwe nakadhalika. Vilevile ujasiri humfanya mtu aulize maswali pale anapotaka maelezo kuhusu kitu fulani, kwa kuuliza unajifunza, unaelewa na kupatiwa majibu ya maswali uliyouliza.

Sababu tano (5) za wewe kutokata tamaa




Ni rahisi mtu kukata tamaa pale mambo yanapomuendea vibaya au anapopata ugumu ambao hakuutegemea hapo awali alipokuwa akipanga mipango yake. Kukata huko tamaa ndipo panapompelekea mtu kutoweza kufikia makusudio yake. Jambo lolote lililofanyika na kufanikiwa kasoro mbalimbali zilitatuliwa. 

Ni vyema ukaelewa changamoto zitakuwepo katika kila kitu unachotaka kufanya, kwa kufahamu hivyo utaweza kufanya mambo yako mpaka yatimie bila kukatishwa na vikwazo au sababu nyinginezo ikiwemo ''kukata tamaa'' hata pale unapopata shida.
Wazo la kukata tamaa ni adui wa wewe kutofanikisha ulichokianza, hivyo nimeona niandike sababu tano(5) za wewe kutokata tamaa zikusaidie kushikamana na malengo yako.

 1. Kukata tamaa hukufanya ufikie kikomo cha mafanikio.

-Moja ya sababu ya watu wengi kushindwa kufanikiwa katika mambo yao ni kukata tamaa mapema kabla hajafika mbali kuendelea kufanya alichokianza. Kukata tamaa ni kudhihirisha hutaki tena kufanikiwa kwa maana ya hutofanya chochote kuhusiana na hicho ulichoamua kuacha. Kuwa mstahimilivu na ushikamane na malengo yako mpaka mwisho.

2. Kukata tamaa ni kuamua umepoteza muda wako wa thamani.

-Unaweza kuwa umetumia nguvu na muda wako mwingi kufanya kitu fulani ambapo thamani yake ni kubwa ya kuweza kukugarimu iwapo utaachana na malengo yako kwa kukata tamaa. Mfano mzuri ni ‘’usiku wenye giza na mchana wenye mwanga’’ linapoingia giza leo jioni kesho yake hakuwezi pambazuka mpaka upite wakati wa giza nene usiku wa manane ndio mwangaza utokee wakati wa asubuhi. Kwa mfano huo halisi ni kwamba unapokata tamaa wakati huko nyuma umejitahidi kwa kadri uwezavyo ni sawa na kuishia njiani ukiwa umeshafika karibu kabisa na mahali ulipotaka kufika.

3. Kukata tamaa ni dhana mbaya ya kujiona umeshindwa.

-Huna sababu ya kukata tamaa ikiwa wengine wameweza. Ikiwa unataka kufanikiwa muda mzuri wa kujipa matumaini kuwa unaweza ni pale unapojihisi unataka kukata tamaa. Usikubali hisia zako zinazokusukuma ukate tamaa zikutawale. Lady Jay Dee, Asha Rose Migiro au Ali Remtulla wasingeweza kuwa na mafanikio makubwa ya kazi zao kama wangekata tamaa na mambo wanayofanya. Unaposhindwa kitu jaribu tena na tena bila kukata tamaa  na hii ndio siri ya kutumiza malengo yako.

4. Kukata tamaa ni kikwazo kidogo kinachokuzuia kufanya mambo makubwa.

-Mambo yote mazuri tunayoona leo yamehangaikiwa kwa kutengenezwa na kuwa kama yalivyo. Amani na uhuru tulio nao leo wazee wetu na watu mbalimbali walipigania mpaka kufikia sasa. Huwezi jua uwezo wako ni mkubwa kwa kiasi gani mpaka uthubutu kutenda makubwa licha ya kuwa utakumbana na vikwazo. Kutokata tamaa kwako ndiko kutakokuwezesha kufanya mambo makubwa na kukufanya uwe mtu bora uliyekomaa.

5. Kukata tamaa ni kizuizi cha kufikiri njia mbadala ya kuendelea kuyaendea malengo yako.

-Matatizo mengi yanaufumbuzi ikiwa tutafikiri vizuri, kukata tamaa ni sawa na kusema hakuna njia nyingine yeyote ya kutatua shida yako. Kizuizi hiki cha kukata tamaa kinaweza kukufanya ushindwe kufikia malengo yako kwasababu tu yakupungukiwa na mawazo sahihi yakukuwezesha utafute njia mbadala na kuendelea kuyaendea na malengo yako.

FILAMU YA FOOLISH AGE YAZINDULIWA

 Elizabeth Michael Aka Lulu akitoa Shukrani kwaWadau wote waliojitokeza katika Usiku wake wa uzinduzi wa Filamu yake Mpya iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City 

The Obamas' New Dog

Bondia Francis Cheka awafurahisha waTanzania,Amfumua mmarekani na kunyakua Ubingwa wa Dunia



 Mgeni Rasmi katika Mpambano wa Kimataifa wa kuwani Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,kati ya Mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phil Williams wa Marekani,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangala (mwenye koti jeupe) akimvisha Mkanda wa Ubingwa huo,Bondia Francis Cheka baada ya kumshinda kwa Point Mpinzani wake,katika Mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Bingwa wa Zamani wa Masumbwi,Fransous Bhotha.
 Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kushoto) akimrushia makonde makali mpinzani wake,Phil Williams kutoka nchini Marekani wakati wa mpambano wao wa Kimataifa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,uliofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Bondia Francis Cheka ameibuka kidedea baada ya kumchapa mpinzani wake huyo kwa Point.
Bondia Phil Williams kutoka nchini Marekani (kulia) nae alikuwa akijibu mashambulizi kwa mpinzani wake,Francis Cheka.hadi mwisho wa mchezo uliokuwa wa raundi 12,Francis Cheka aliweza kuibuka Kidedea kwa kumchapa mpinzani wake huyo kwa point na kufanikiwa kumnyang'anya mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU.
 Chukua hiyoooooo...
 Hapa lazima ukae,mie ndio kisiki cha mpingo:hivyo ndivyo Bondia Francis Cheka alivyoonekana kuifanya kazi yake vilivyo.
 Refa wa Mchezo huo akimzuia Bondia Francis Cheka baada ya kumkoleza makonde kisawasawa mpinzani wake,yaliyompelekea kwenda chini.
Mpambano ukiendelea.
Wanahabari wakipata taswira za mpambano huo.

Rais Barack Obama wa Marekani azungumza juu ya nchi ya SYRIA

Wafanyakazi wa migodi kugoma Afrika Kusini

Wamiliki wa migodi ya madini nchini Afrika Kusini, wamesema kuwa wafanyakazi wao wameitisha mgomo wa kitaifa kuanzia siku ya Jumanne, kutaka mishahara yao kuongezwa.
Chama cha kitaifa cha wachimba migodi, NUM kimeitisha nyongesa ya mishahara ya hadi asilimia sitini.
Mapema wiki hii wafanyakazi hao walikataa pendekezo la waajiri wao la kutaka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia sita, kiwango ambacho ni sawa na mfumuko wa bei kwa sasa nchini Afrika Kusini.
Afrika Kusini ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa uzalishaji wa dhahabu, lakini kiwango chake kimeshuka kutokana na uwekezaji duni na uhasiano mbaya kati ya wafanyakazi na wamiliki wa migodi hiyo.
Kampuni kubwa za kuchimba madini nchini humo za AngloGold Ashanti, Gold Feilds, Harmony Gold na Sibanye na kampuni zingine ndogo ndogo tayari zimepokea ilaani hiyo ya mgomo.
Chama hicho cha NUM huakilisha asilimia sitini na nne ya wafanyakazi wa migodi wapatao elfu mia moja ishirini.
Taifa la Afrika Kusini kwa sasa linakabiliana na athari za mgomo wa wafanyakazi wa secta ya utengenezaji magari, ujenzi na wale wa viwanja vya ndege.
Wafanyakazi wa secta ya kuuza mafuta vile vile wameitisha mgomo kuanzia wiki ijayo.
Serikali ya nchi hiyo imetoa wito kwa wafanyakazi hao kudumisha amani wakati wa mgomo wao.
Mwaka uliopita, wafanyakazi thelathini na wanne wa migodi waliokuwa wakiandamana waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati ghasia zilipoibuka wakati wa mgomo wao.
Wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanasema utawala wa rais Jacob Zuma unakabiliwa na changamoto kutoka pande zote.
Wanachama wa chama chake tawala cha African National Congress ANC wanamtaka rais Zuma, kutenda zaidi ili kupunguza viwango vya umasikini, nao wafanyabiashra wanataka serikali yake kupunguza ukiritimba ili kuvutia uwekezaji kutoka mataifa ya kigeni na kuimarisha mikakati za kufufua uchumu wa taifa hilo.

New