Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb) akimpokea Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Kaguta Museveni alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Museveni yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia tarehe 25 hadi 26 Machi, 2015.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe akimpokea Rais wa Burundi Mhe.Pierre Nkurunziza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimatafa wa Mwalimu Julius Njerere.
Rais Museveni akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Balkis Mvungi kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.
Rais Museveni akikagua gwaride la heshima
Mheshimiwa Nkurunziza akifurahia ngoma za asili muda mfupi mara baada ya kuwasili.
Rais Museveni na Waziri Membe wakiangalia burudani ya ngoma za asili uwanjani hapo.
Waziri Membe akiwa ameongozana na Rais Museveni mara baada ya kukagua gwaride na kushuhudia ngoma za asili.
Waziri Membe akimtambulisha Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya kwa Rais Nkurunziza mara baada ya kuwasili nchini.
No comments:
Post a Comment