Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa,
akipungia mkono maelfu ya wana CCM na wananchi wa Musoma, alipowasili
uwanja wa ndege wa Musoma Juni 9, 2015, kuendelea na kampeni yakle ya
kuomba wana CCM wamdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na
CCM kuwania nurais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25, 2015
Lowassa, (kulia), akiwatuliza wana CCM na wananchi wa Musoma,
waliojaribu kuvunja geti ili walao wapate kugusana naye alipowasili
uwanja wa ndege wa Musoma, Juni 9, 2015, kwa nia yabkuomba wana CCM
wamdhamini
Wana CCM na wananchi wa Musoma, wakipiga kelele kumwita Mh. Lowassa,
ili awasogelee kumsalimia huku wakiwa nje ya geti la uwanja wa ndege wa
Musoma
Mh. Lowassa, akiongea na bibi kizee huyu aliyeomba walau amshike
mkono ili kumpa baraka katika safari yake ya matumaini 2015, alipowasili
kwenye ofisi za CCM wilaya ya Bunda, mkoani Mara, Juni 9, 2015 kuomba
wana CCM wamdhamini
Mh. Lowassa, akiwasili ofisi za CCM wilaya ya Bunda
Mh. Lowassa, (kushoto), akiwashukuru wana CCM na wananchi
waliojitokeza kwenye ofisi za CCM wilaya ya Bunda, wengine kwa nia ya
kumdhamini na wengine kumuona
Umati wa watu uliofurika kwenye ofisi za CCM wilaya ya Bunda, huku wengine wakiwa juu ya mti walau wapate kumuona
Mh. Lowassa a,kiwasili ofisi za CCM wilaya ya Musoma
Mh. Lowassa akiwasili ofisi za CCM, wilaya ya Tarime mkoani Mara
Mh. Lowassa mkiwapungia wana CCM na wananchi wengine alipowasili ofisi za CCM, wilaya ya Tarime
Msanii huyu yeye aliamua kuja na ritungu huko Rorya wakati Mh. Lowassa a.lipowasili ofisi za CCM wilaya ya Rorya
No comments:
Post a Comment