Kim Kardashian akifanyiwa uchunguzi kwa njia ya Ultra Sound.
...Akiwa na mwanaye North.
MWANAMITINDO maarufu wa Marekani, Kim Kardashian, amefichua kwamba anaweza kukumbwa na kisukari cha uzazi wakati akisubiri kujifungua mtoto wake wa pili.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 na anayeelekea mwishoni mwa kipindi chake cha ujauzito aliyasema hayo akiwa na familia yake katika matayarisho ya msimu wa kipindi kinachorushwa na vyombo vya habari cha Keeping Up With The Kardashians.
Kipindi hicho kinatayarishwa kurushwa mwezi ujao. Kim anayetegemea kujifungua mtoto wa kiume mwezi Desemba mwaka huu, alionekana akipimwa na daktari ambaye alimwambia: “Ukishakuwa na dalili za matatizo yanayoanzisha shinikizo la damu, matatizo ya kibofu na figo (reeclampsia) utakuwa unakabiliwa na tatizo la kukumbwa na kisukari cha wakati wa uzazi. Mwanamitindo huyo alikwepa tishio hilo alipokuwa na ujauzito wa binti yake, North, ambapo alibidi apelekwe kujifungua kabla ya wakati wake.
Ugonjwa huo huwapata wanawake katika kipindi chao cha mwishoni cha ujauzito, lakini huwa unapotea mara tu wanapojifungua. Wanawake wajawazito hubidi kufuatiliwa kwa karibu viwango vya sukari mwilini mwao ambapo wengine hupewa matibabu ya kuzuia kutokea kwake.
Kitu kingine ambacho kinampa wasiwasi mke huyo wa mwanamuziki maarufu wa Marekani, Kanye West, ni pale ambapo Kim alimwambia mama yake, Kris Jenner na dada yake, Kourtney Kardashian, kwamba: “Madaktari waliona majimaji mengi katika kondo, hali ambayo inamaanisha ninaweza kupatwa na kisukari.” Hivi majuzi, Kim alikiri kwamba huwa hafurahii kuwa mjamzito kwani huwa hapendi jinsi mwili wake unavyopanuka na kujikuta anashindwa kuvaa nguo zake.
No comments:
Post a Comment