1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubutu wako.
2. Mwanamke anaemuheshimu mumewe ni mwanamke bora ambae kila mwanaume angetamani kuwa nae.
3. Tabia yako na misimamo yako ndio itakayomfanya mumeo ajute au afurahie kukuoa wewe.
4. Kuwa mke bora inakubidi uwe vizuri katika maarifa ya kutawala hasira zako na sio kuwa mtu wa kulipiza visasi.
5. Kuwa kiongozi huko kazini kwako lakini kuwa mtu wa kunyenyekea nyumbani kwako kwa mumeo. Hiyo ni busara.
6. Usiweke mashindano na mumeo, mpe hongea na mtie moyo kwa kila hatua anayopiga katika maisha.
7. Kuwa na ubinadamu, sio kosa dogo tu mumeo amefanya ukatamani kulipiza kisasi. It won't help u!
8. Kuwa mkarimu, kila mwanaume anamuheshimu mwanamke mkarimu na mwenye msimamo.
9. Usijaribu kumpa adhabu mumeo ya kumnyima chakula cha usiku kitandani, hii itamlazimu kutafuta chakula nje ya ndoa.
10. Hakuna kitu kibaya kama utakubali kuwa ulikosea kama kweli ulikosea. Kuwa mrahisi kukubali kama kweli ulikosea. Na omba radhi pale inapobidi.
11. Jiandae kumsamehe mumeo pale anapokosea kwa maana mke atoae msamaha kwa mumewe ni mke mwema tofauti na yule aliejaa visasi.
12. Tengeneza maamuzi ya kuwa mke mwema, pasina kuwa na hofu yoyote na Mungu atakubariki.
13. La mwisho na la muhimu tambua kwamba mwanamke aliejaliwa umbo zuri na sura nzuri pasina maarifa kichwani anafaa kwa usiku mmoja, lakin yule mwenye maarifa na ufahamu yeya afaa kwa maisha yote!
MUNGU AWABARIKI WANAWAKE!
DONDOO KUMI KWA WANAUME ILI KUTENGENEZA MAHUSIANO YENYE AFYA.
1. Usijisahau katika mahusiano ukawa comfortable kiasi kwamba zile mbwembwe zote za kipindi unamtongoza ukazipotezea. Mwanaume smart haachi kumfanya mwanamke wake ampende zaidi. Mwanaume anaemfanya mwanamke wake ampende zaidi mahusiano yao hudumu mpaka uchweo.
2. Usisahau kufanya tabasamu kuwa kipaumbele cha mwanamke wako. Ole wao wanaume wanaowanyima tabasamu wapenzi wao wakaacha wanaume wengine ndio wawape tabasamu wanawake zao. Nawaambien mpo kwenye matatizo makubwa.
3. Yatunze maneno yako kwa uaminifu mkubwa. Uaminifu ni msingi imara wa mahusiano yenye afya. Mwanaume wa kweli hakimbii majukumu.
4. Usiwe mkoloni katika mahusiano. Kuna haki ya kusikiliza na kusikilizwa (natural justice). Kuwa mwanaume, admit kama umekosea. Kuwa na ujasiri wa kurekebisha pale ulipokosea
5. Usimfanye mwanamke wako aone kama anashindana na muda wako, mfanye ajisikie na yeye anathamani katika muda wako. Sio sababu ya kuwa na muda au laa bali ni jitihada ya wewe kutengeneza muda wa pamoja.
6. Usiwe mvivu. Kuna mtu mwingine pembeni ambaye anatamani kuwa na huyo mwanamke. Linda tunu yako kwa upendo, furaha na amani nae. Usiwe mvivu kumfurahisha, kumlinda, kumridhisha na kumsifia. Pombe na nyama choma zisije zikakuponza.
7. Usihukumu. Kila mmoja anafanya makosa na anajifunza kwayo. Usihukumu makosa yake wala past yake. Na kitu cha muhimu usimhukumu kwa vile unafikiri tofauti na yeye. Binadamu tunatofautiana sana. Enjoy kuwa nae kwa jinsi alivyo. Usilazimishe awe kama wewe.
8. Usi assume kwamba anajua kama unamjali, mwonyeshe kweli unajali. Mpe support katika shughuli zake i.e masomo, biashara, kilimo, etc. Mtumie sms, msikilize, msifie, muonyeshe mapenzi kwa maneno na vitendo na uwe mbunifu.
9. Usiwe mwanaume jina, acha tabia ya kuzila na kususa ,onyesha kuwa wewe ni mtu wa majukumu na ni kichwa katika mahusiano, jenga mahusiano kwa busara zaidi na sio kwa ki imla (dictatorship). Maumuzi yako ya kijinga kijinga yatakutokea puani.
10. Usikate tamaa kirahisi, najua maisha ni magumu ila mwanaume wa kweli anapotaka kitu, atafanya kila awezalo kukipata, unasubiri nini? fanya hivyo sasa.
Nawatakia week njema.