My Web

Emmanuel

CONTACT

Monday, February 15, 2016

KOSA MOJA TENA DOGO LINAWEZA LIKAKUFANYA UWE MTUMWA WA KUDUMU.


Vijana wawili waliokuwa na hali ngumu ya maisha waliamua kwenda kuomba kazi kwa tajili mmoja aliyekuwa amejenga pembeni kidogo mwa mjii wenye watu masikini. Vijana hao mara baada ya kufika na kuonana na huyo tajili walijieleza namna maisha yao yalivyo magumu huku wakimuomba tajili huyo awape kazi yoyote, kwa kipato chochote, nao watafanya kwa moyo wote.

Yule tajili baada ya kuwasikiliza kwa umakini alijisikia kuwapa wale vijana kazi na akawaomba wafanye kazi kwa moyowote kama walivyojieleza huku akiwasisitiza wawe makini pindi wanapofanya kazi kwani alikuwa hapendi kuona kitu chochote kikihalibiwa kwa uzembe. Basi akatoa kazi mbili na kumsihii kila mmoja achague kazi anayoipenda.Kazi ya kwanza ilikuwa ni kazi ya jikoni yanii Kupika, pamoja na kufanya usafi wa ndani kama vile kudeki, kusafisha vyombo pamoja na kufua nguo na kazi ya pili ilikuwa inahusu shughuri zote za nje yani kufyeka majani, kupalilia bustani pamoja na kulisha mifugo.

Vijana walichagua kazi na kila mmoja aliipenda kazi yake, Hao vijana walijitaidi kufanya kazi vizuri ili wapendwe zaidi na boss wao. baada ya kumaliza kufanya kazi ya siku vijana walikuwa huru kucheza au kukaa tuu huku wakisubiri siku ipite. Kijana aliyekuwaanafanya kazi za nje alikuwa anamaliza kazi zake mapema kwani baadhi ya kazi zilikuwa sii za kufanya kila siku kwa mfano kupalilia bustani na kufyeka majani, kazi iliyokuwa kubwa kakwe ilikuwa ni kulisha mifugo asubhi, mchana na jioni.

Basi sikumoja kijana anayefanya kazi za nje baada ya kumaliza kazi zake alitengeneza manati na kuanza kulenga vindege vilivyokuwa vinatua kwenye mabanda ya mifupo, kwa bahati mbaya alikosea shabahaa na kupiga kuku aliyekufa papohapo. kijana yule alimkimbilia yule kuku na kumtia kwenye mfuko kisha alimzika haraka kabla boss wake hajaona, kwa bahati mbaya yule rafiki yake anayefanya kazi za jikoni alimuona akifanya kosa hilo. Basi yule Kijana anayefanya kazi za nje alimuomba kijana anayefanya kazi za ndani asiseme kwa boss kwani alikuwa anaogopa sana kufukuzwa kazi endapo boss angejua, yule kijana anayefanya kazi za ndani alikubaliana na ombi la rafiki yake kwa mashariti ya kusaidiwa kazi za ndani kwa siku hiyo. Hiyo siku kijana anayefanya kazi za nje aliambiwa aoshe vyombo, basi yule kijana anayefanya kazi za nje akaona siyo mbaya mara mia aoshe vyombo kuliko kufukuzwa kazi. Bahati mbaya ule utumwa uliendelea siku hadi sikuu na alipojalibu kukataa kufanya kazi za ndani basi yule mfanyakazi wa ndani alikuwa anamtishia na kusema kama unakataa naenda kwa boss na kumwambia habari za KUKU.

Basi zikapita siku, wiki, hatimaye miezi kadhaa, kijana anayefanya kazi za nje akajikuta amekuwa mtumwa wa kazi za ndani na nje, akakonda kwa kazi nzito huku jamaa yake akiendelea kunenepa maana ulifika wakati yule anayehusika na kazi za ndani hakuwa anafanya kazi yoyote. Siku moja yule kijana aliyekuwa anahusika na kazi za nje baada ya kupata taabu nyingi akakata shauri na akaamua kwenda kuonana na boss ili aombe msamaha kwa kosa alilofanya. Boss alimkalibisha yule kijana ili aweze kusikiliza mahitaji yake. Yule kijana alianza kulia kabla ya kujieleza hatimaye boss alijitaidi kumnyamazisha kisha alimsihii aelezee yanayomsibu. Kijana alipiga magoti na kuelezea kosa alilotenda ikiwa ni pamoja na taabu (utumwa) alizopata baada ya kufanya kosa lile la kuua kuku. Boss alishanga kuona lile jambo limemkondesha yule kijana kiasi kile na alisema mimi siku ile ile ya kwanza unamuua yule kuku nilikuona na nilisha kusamehe siku ile ile maana nilijua wazi kuwa hukukusudia kufanya hivyo lakini kwa bahati mbaya nilikuwa sijui kama lile jambo liliendelea kukutesa na kukufanya uwe mtumwa hadi ukakonda kiasi hiki. Basi yule kijana baada ya kusamehewa alishukuru ndipo boss akamwambia kila siku hakikisha unapikiwa mayai manne na rafiki yako ili mwili wako ujirudi haraka.

Kijana alimshukuru sana boss kwa msamaha aliopewa kisha akaondoka akiwa na furaha, bahati mbaya sana yule kijana aliyekuwa anahusika na kazi za jikoni alikuwa amelala akitegemea yule anayefanya kazi za nje atafanya kazi za ndani siku hiyo asijue kuwa kijana anayefanya kazi za nje ataenda kuomba msamahaa kwa boss. Basi aliamka na kukuta hamna kazi ya ndani iliyofanywa, Alimsihii kijana anayefanya kazi za nje aanze mara moja kufanya hizo kazi laa sivyo ataenda kusemelea habari za kuku kwa Boss. Kijana anayefanya kazi za nje akamjibu hunitishii kama vipi nenda ukaseme ndo kwanza kabisa nakusindikiza, basi yule kijana aliekuwa anahusika na kazi za ndani kwa hasira alitoka na kwenda kusemelea kwa boss habari za mauaji ya kuku. Boss alishangaa kuona jambo la zamani anaambiwa siku ile, akamuhoji yule mfanyakazi kwanini hukusema siku ile unaamua kusema leo? yule mfanyakazi alikosa maelezo ya kutosheleza kwani alisingizia kuwa alikuwa anaogopa kumbe boss ameshapata stori yote hata jinsi alivyomtumikisha mwenzake.

Ikabidi boss aelezee namna alivyofanya kosa la kuka na udhaifu wa mtu kwa mda mrefu huku akisikitishwa sana na jinsii alivyoutumia udhaifu huo kumtesa mwenzeke hadi kufikia hali ya kukonda kiasi kile, kisha akamwambia hawezi kukaa na mtu anayeficha maovu kwa mda mrefu na anaamua kuyaweka peupe hadi siku anayoona hanufaiki na uovu huo. Basi siku hiyohiyo yule kijana anayefanya kazi za ndani alisimamishwa kazi kisha yule boss akatafuta mfanyakazi mwingine.

USHAURI WANGU, CHINI YA JUA HAYUPO ALIYEKAMILIKA NA MUNGU ANAYETUJUA VEMA MDA  MWINGINE ANATUSAMEHE HATA KABRA YA KWENDA KUOMBA MSAMAHAA,JITAIDI KUSAMEHE BURE NAWE UTASAMEHEWA BURE.

No comments:

Post a Comment

New