Binti alienda kwa bibi yake na kumuelezea jinsi anavyoishi na ugumu wa maisha katika ndoa yake. Mume wake amekua hamuheshimu ni ugomvi na malumbano kila siku iitwayo leo. Hakujua afanye nini na aliazimia kukata tamaa. Alichoka na ugomvi na manyanyaso. Ilionekana kila akitatua jambo hili linaibuka jambo jingine fasta.
Bibi yake alimchukua binti na kumpeleka jikoni. Bibi akajaza maji sufuria tatu na zote akaziweka katika moto. Punde maji ya kila sufuria yakachemka. Katika sufuria ya kwanza bibi akaweka karoti, sufuria ya pili akaweka yai, na la tatu akaweka mbegu ya kahawa. Akaacha vichemke bila kusema neno.
Baada ya kama dakika ishirini akazima moto na kuepua sufuria zote tatu. Akatoa karoti na kuiweka katika bakuli, akatoa yai na kuweka kwenye bakuli pia na akamimina kahawa katika kikombe.
Baada ya hapo akamgeukia mjukuu wake na kumwambia "niambie sasa unaona nini?"
Binti akajibu "karoti, yai na kahawa"
Bibi akamsogezea vile vitu kwa karibu zaidi na akamwambia aiguse karoti na kuibinya. Akafanya hivyo na kugundua kuwa ilikuwa imelainika sana. Bibi akamwambia mjukuu wake alichukue lile yai na kujaribu kulivunja. Akagundua kuwa lilikuwa gumu mno.
Mwishoe bibi akamwambia ajaribu kuonja kahawa. Binti akatabasamu baada ya kujaribu ladha nzuri ya kahawa. Baada ya hivyo binti akamuuliza bibi "vitu hivi vinamaaninsha nini?"
Bibi akamfafanulia kwa kumuambia kwamba kila kitu yani kahawa, yai na karoti vimekabiliwa na tabu moja ya kuunguzwa na maji. Na kila kimoja kime react tofauti. Karoti kabla ya kuwekwa ktk maji ilikuwa ngumu kweli lakini baada ya kuunguzwa ikawa laini laini na kusinyaa.
Yai kabla ya kukutana na dhahama ya maji ya moto lilikuwa fragile kiasi kwamba ni rahisi kupasuka na ganda la nje lilikuwa likilinda kimiminika cha ndani ya yai. Lakini baada ya kuunguzwa na maji ya moto kimiminika cha ndani kikawa kigumu na si kimiminika tena.
Mbegu ya kahawa ilikuwa ya kipekee, lakini baada ya kuunguzwa na maji ya moto imeyabadilisha rangi maji yote.
Wewe upo wapi kati ya hivyo vitu vitatu? Bibi akamuuliza mjukuu wake. "pale unapokabiliana na matatizo ambayo kwa muktadha huu nimeyafananisha na maji ya moto huwa unareact vipi? Je wewe ni karoti, yai au mbegu ya kahawa?
Fikiria hivi: mimi ni nani? Je mimi ni karoti ambayo huwa ngumu, lakini pale ambapo ninakabiliana na maumivu na mateso makali nakuwa laini na kupoteza nguvu zangu?
Je mimi ni yai ambae nina moyo wa kimiminika lakini nabadilishwa na joto kali la maji. Nina moyo wa kimiminika ambapo baada ya kifo, kuachana, matatizo ya kiuchumi au majaribu mengine nakuwa mgumu na imara? Je ganda la nje linaonekana vile vile lakini ndani ni moyo jasiri, enye nguvu usioteteleka?
Au mimi ni kama mbegu ya kahawa? Ambayo kimsingi inayabadilisha maji ya moto rangi, je mimi ni jasiri kiasi kwamba ingawa nakabiliana na matatizo mengi lakini nakuwa jasiri kukabiliana nayo na kuyabadili?
Mjukuu wangu ni vema ukawa kama kahawa au yai. Kamwe usiwe kama karoti, ukiwa hivyo utawanufaisha wale wakuumizao! Maana kwao watafurahi kukuona ukizidi kuwa mnyonge na mwenye kunyong'onyea pale wakuumizapo. Lakini kama utakuwa mgumu kama yai utawaacha wakijiuliza maswali mengi pasina majibu.
Hakuna tunu kubwa duniani kama furaha mjukuu wangu, wewe hata wakuumize kiasi gani! Usioneshe huzuni mbele yao! Wewe tabasamu tu. Kufanya hivyo utawaacha wakiwa na maswali yasiyo na majibu!
Unakabiliana vipi na majaribu yako? Je wewe ni karoti, yai au kahawa!!
Jibu unalo wewe mwenyewe.
No comments:
Post a Comment