Katika maisha, mtoto mchanga chakula pekee ambacho anatakiwa apewe ni maziwa ya mama.
Kunyonyesha ndiyo njia ya kwanza kabisa kumpa mtoto chakula na vitamini sahihi. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo wakati ana miezi michache utoaji wako maziwa mama mzazi huathirika, kwa sababu jinsi mtoto anavyonyonya ndiyo maziwa yanavyotengenezwa.
Ndiyo maana watu wengi wanapoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao huanza kupungua.
Faida za kumnyonyesha mtoto mchanga ni nyingi lakini kubwa kabisa ni kwamba, maziwa ya mama yana virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa mtoto.
Maziwa ya mama humlinda na magonjwa mengi ya utoto pamoja na mzio (allergies) mbalimbali.
Lakini pia kunyonyesha hueleta ukaribu kati ya mama na mtoto, hupunguza uwezekano wa mama kupata kansa ya matiti.
Kikubwa zaidi kumnyonyesha mtoto ni kumpa chakula cha bure ambacho mzazi anaweza kumlisha mwanaye lishe hiyo bora wakati wowote bila usumbufu.
WAKATI GANI UANZE KUMPA CHAKULA
Mtoto akifikisha miezi sita unaweza kuanza kumpatia vyakula vingine kidogokidogo. Mtoto akianza kupewa vyakula nje ya maziwa mapema kabla ya miezi 4 ni hatari kwa afya yake maana mfumo wake wa kusaga chakula unakuwa bado haujawa tayari.
Lakini hata ukianza kumpa vyakula vingine hutakiwi kuacha kumnyonyesha hadi afikie miaka miwili na nusu.
Ili mtoto aweze kula vyakula ni kwamba awe amefikisha miezi sita, shingo iwe imekaza, awe anaweza kukaa kwa kuwekewa kitu (mfano kiti chenye mkanda).
Kumbuka unapoanza kumpa mtoto chakula hasa kwa kijiko lazima awe na uwezo wa kufungua mdomo, kutaka kupokea au kugeuza uso kwa ishara ya kukataa.
Akipokea chakula anakiweka mdomoni na kujaribu kumeza na siyo kukisukuma nje na kuacha mdomo wazi. Hakikisha mtoto wako yupo tayari kabla hujaanza kumpa
No comments:
Post a Comment