My Web

Emmanuel

CONTACT

Saturday, October 13, 2012

Mkuu wa mashtaka Misri akaidi rais

Mkuu wa mashtaka wa Misri, AbdalMajid Mahmoud, amerejea ofisini na ulinzi mkali na hivo kukaidi amri ya Rais Mohamed Morsi ya kumtoa kazini.
Mkuu wa mashtaka wa Misri
Rais Morsi alijaribu kumtoa kazini mkuu wa mashtaka siku ya Alkhamisi baada ya afisa huyo kuwafutia mashtaka maafisa zaidi ya 40 watiifu kwa rais wa zamani, Hosni Mubarak, ambao walishtakiwa kwa kuongoza mashambulio dhidi ya waandamanaji wakati wa mapinduzi ya mwaka jana.
Mkuu wa mashtaka na wafuasi wake wanasema rais hana madaraka hayo.
Kuachiliwa kwa washtakiwa hao kulizusha maandamano ya ghasia katika medani ya Tahrir mjini Cairo Ijumaa, ambapo watu zaidi ya mia moja walijeruhiwa kwenye maandamano makubwa kabisa dhidi ya rais tangu kushika madaraka mwezi wa Juni.
Mkuu wa mashtaka, Abdel Maguid Mahmoud, alirudi ofisini mwake huku amezungukwa na walinzi na mamia ya mahakimu na mawaikili.
Alitaka kuonesha uhuru wake baada ya Rais Morsi kujaribu kumtoa kazini, kwa kumteua kuwa balozi wa Misri Vatikani.
Inaarifiwa kuwa majaji kadha walitishia kujiuzulu piya.
Tena mkuu wa mashtaka alikwenda kwenye mkutano na mmoja kati ya ma-naibu wa rais kujaribu kuzimua mambo.
Wakati wa serikali ya zamani kulikuwa na malalamiko mengi kuwa mahakimu na maafisa wa mashtaka wakishawishiwa na serikali.
Sasa, chini ya serikali mpya, wanajaribu sana kuonesha uhuru wao.
Hichi kisa kimeleta aibu kwa rais - na tayari kuna ishara kuwa anajaribu kubadilisha uamuzi wake wa kumtoa kazini mkuu wa mashtaka.

Wednesday, October 10, 2012

Mtetezi wa elimu Pakistan anusurika kifo



Malala Yousafzai,

Madaktari nchini Pakistan wamefanikiwa kutoa risasi kichwani mwa msichana wa miaka 14 mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Malala Yousafzai.
Hii ni baada ya msichana huyo kushambuliwa kwa kupigwa risasi hapo jana alipokuwa akitoka shuleni Kaskazini Magharibu mwa eneo la Swat.
Taarifa kutoka kwa madakatari wake zinaeleza kuwa hali ya msichana huyo iko shwari kwa sasa.
Malala alituzwa tuzo la nobel kutokana na juhudi zake za kupigania haki ya elimu kwa wasichana wa Taliban ambao kwa mujibu wa desturi za kitaliban haswa katika eneo la Swat walikuwa hawaruhisiwi kupata elimu
Ndugu yake aliambia BBC kuwa, madaktari,wangali wanatafakari ikiwa wampeleke nje kwa matibabu zaidi.
Kundi la Taliban lilisema lilihusika na shambulizi hilo.
Malala Yousafzai aliandika kitabu cha kumbukumbu zake binafsi kwa niaba ya BBC miaka mitatu iliyopita wakati eneo la Swat lilikuwa linadhibitiwa na kundi laTaliban.
Wanasiasa nchini Pakistan, walilaani shambulizi hilo huku Marekani ikilitaja kama kitendo cha uoga

Rais wa Kenya atibua njama ya wabunge



Kero la wananchi wa Kenya kwa wabunge wao
Rais wa Kenya Mwai Kibaki, amekataa kuidhinisha mipango ya wabunge wa taifa hilo kujipatia kitita kikubwa cha pesa kama marupurupu ya kuhudumu kama wabunge.
Wabunge hao walipanga kujilipa dola alfu mia moja na kumi kila mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Lakini bwana Kibaki amesema kuwa hatua hiyo inakiuka katiba na haiwezi kutekelezwa wakati ambapo walimu pamoja na madaktari nchini Kenya wamekuwa wakigoma kudai nyongeza ya mishahara.
Waandamanaji waliojawa na ghadhabu nchini Kenya walijitokeza hapo jana kulaani hatua ya wabunge hao kutaka kujilipa mamilioni ya pesa kama pesa za ziada wakati bunge litakapofunga vikao vyake kwa maandalizi ya uchaguzi mwaka ujao.
Waliwataja wabunge hao kama fisi wenye ulafi.
Wabunge wa Kenya ni baadhi ya wale wanaopokea mishahara mikubwa sana barani Afrika , wakipokea takriban dola elfu 10,000 kama mshahara kila mwezi.
Malipo hayo ya ziada ya dola 110,000 kwa kila mmoja walitaka yalipwe wakati watakapofunga vikao vyao kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2013.
Wadadisi wanasema kuwa wananchi wangetozwa kodi zaidi ili kugharamia malipo hayo ya dola milioni 23.
Hatua hii imewakasirisha watu wengi, hasa ikizingatiwa kuwa inakuja baada tu ya migomo katika sekta ya umma ambapo madaktari, walimu na hata wahadhiri wa vyuo vikuu walisusia kazi wakidai nyongeza ya mishahara.
Mswaada huo ulipitishwa siku ya Alhamisi ikiwa sehemu ya mabadiliko yaliyofanyiwa mswaada wa fedha bungeni.
Mnamo mwezi Septemba, shule za umma zilifungwa kwa wiki tatu wakati walimu walipogoma wakidai nyongeza ya mishahara na huku madaktari nao wakitaka mazingira bora ya kazi.

Thursday, October 4, 2012

Uchunguzi waakhirishwa Afrika Kusini

Tume inayochunguza mauaji ya Marikana

Tume ya kuchunguza mauaji ya wachimba migodi nchini Afrika Kusini, imetoa muda kwa mawakili kushauriana na jamaa za waliouawa
Wakili mmoja wa familia kadhaa za waathiriwa, alisema kuwa sio wachimba migodi wote waliouawa wamezikwa na kwa hivyo hakupata muda wa kuwasiliana na familia zao.
Makamishna wa tume hiyo, tayari wamezuru eneo la mauaji karibu na mgodi wa Marikana unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin
Majasusi na wataalamu wa uchunguzi wa mauaji wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.
Tume hiyo yenye makamishna watatu, pia itachunguza mauaji ya wachimba migodi wengine kumi akiwemo polisi mmoja aliyeuawa wakati wa vurugu katika mgodi huo.
Siku hiyo ya mauaji inasemekana kuwa mojawapo ya siku zilizosuhudia ghasia mbaya kuwahi kutokea tangu kumalizika kwa enzi ya utawala wa ubaguzi wa rangi ,mwaka 1994.
Ghasia hizo zilianza kufuatia vuta ni kuvute ya mishahara kati ya wachimba migodi na wamiliki wa migodi hiyo.
Tume hiyo ina vikao vyake katika ukumbi mmoja ulio karibu na eneo la mauaji Kaskazini Magharibi mwa Johannesburg.
Rais Jacob Zuma ndiye aliunda tume hiyo punde baada ya mauaji kutokea. Inaongozwa na jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa, Ian Farlam.
Tume hiyo itachunguza namna ambavyo polisi, wamiliki wa mgodi, vyama vya wafanyakazi na serikali walivyohusika na mauaji hayo.
Tume hiyo inatarajiwa kutoa tathmini yake kuhusu mauaji hayo katika muda wa miezi minne, huku ripoti yake ya mwisho ikitolewa mwezi mmoja baadaye.
Takriban watu 46 waliuawa katika ghasia hizo ambazo zilifanyika wakati wa wiki moja ya vurugu kwenye mgodi wa Marikana.

Tuesday, October 2, 2012

BASI LA DAR EXPRESS LIKITEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI

Basi la Dar Express lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar likiteketea kwa moto eneo la Segera, mkoani Tanga leo asubuhi. Abiria wote 65 wamenusurika.

MAGARI MAWILI YAGONGANA NA KUWAKA MOTO MBALIZI MKOANI MBEYA, 10 WALIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, MBUNGE WA VITI MAALUM MARY MWANJELWA ANUSURIKA, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO

 HIVI NDIVYO MAAFA YALIVYO.

 GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI.


 MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI JIJINI MBEYA.


GARI HILI LILIVYOPINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI.
 MKUU WA MKOA WA MBEYA ALIYEVAA SUTI YA BLUU, MH. ABAS KANDORO AKIWA ENEO LA AJALI.
 HII NI GARI NYINGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA.
 ZIMAMOTO WAKIWA ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO.
 ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAKIWA ENEO LA TUKIO AMBAPO AJALI HIYO IMESABABISHA VIFO VYA WATU KUMI.
 WATU WAKIWA WAMEONGEZEKA KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA AJALI.
 MUONEKANO WA GARI HILI LIKIWA LIMEUNGUA LOTE.
MABAKI YA GARI HILI AMBALO NALO LILIUNGUA LOTE.
WANANCHI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI HUKU WENGINE WAKIWA WANAENDELEA KUOKOA MAJERUHI WA AJALI HIYO.
KIKOSI CHA FFU NAO WALIKUWEPO SAMBAMBA KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI LA UOKOAJI LINAENDA KIKAMILIFU.
PIA KATIKA ENEO HILI  MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWA ALIKUWEPO NDANI YA PICK UP ILIYOUNGUA MOTO, KATIBU WAKE AMETEKETEA KWA MOTO NDANI YA GARI HILO.
HABARI KAMILI ITAWAJIA BAADAE.
 TONE MEDIA LIVE GROUP TUMESHUHUDIA TUKIO HILI

Kamanda wa jeshi kizimbani I.Coast



General Dogbo Ble (kulia) alikuwa mshirika wa rais wa zamani Laurent Gbagbo

Mshirika mkubwa wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, amefunguliwa mashtaka mjini Abidjan, katika kesi ya kwanza ya watu waliotuhumiwa kwa ghasia za baada ya uchaguzi wa kati ya mwaka 2010 na 2011.
Generali Dogbo Ble alikuwa kamanda wa jeshi la Republican Guard chini ya uongozi wa bwana Gbagbo.
Yeye pamoja na maafisa wengine wa usalama wanatuhumia kwa mauaji ya kanali mmoja mkuu wa jeshi wakati wa mzozo huo uliodumu kwa miezi sita.
Bwana Gbagbo anasubiri kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC. Anakana madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita.
Ivory Coast imekuwa ikituhumu washirika wa Gbagbo, katika nchi jirani ya Ghana kwa kufanya uvamizi mipakani kwa lengo la kuitikisa serikali ya Rais Alassane Ouattara.
Mwandishi wa BBC John James anasema kuwa mahakama ilifurika watu kushuhudia kuanza kwa kesi ya Generali Dogbo Ble
Generali Ble, anayetoka kabila la bwana Gbagbo, aliibuka kama kamanda wa jeshi wakati wa vurugu la mwaka 2011 la kutaka udhibiti wa Abidjan, na kuendeshea harakati katika kambi ya muda iliyokuwa katika ikulu ya rais.
Alikuwa mmoja wa majenerali, ambao hawakumuunga mkono Rais Ouattara wakati wa kilele cha mapigano hayo.
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamepongeza hatua ya kumfungulia mashtaka kamanda huyo lakini wanaonya kuwa lazima kesi iendeshwe kwa usawa au la sivyo itaibua taharuki nchini humo

Wanafunzi 20 wauawa na Boko Haram



Abubakar Shekahu kiongozi wa kundi la Boko Haram
Takriban wanafunzi 20 wameuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Mubi, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Polisi wamefahamisha BBC kuwa shambulizi hilo limetokea katika mabweni yao mbali kidogo na chuo cha ufundi anuwai cha Mubi.
Mhadhiri mmoja amefahamisha BBC kuwa wanafunzi 40 wameuawa lakini bado taarifa hizo hazijathibitishwa.
Mauaji haya yanakuja siku chache baada ya operesheni kali kufanywa dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram mjini humo.
Aidha mhadhiri ambaye hakutaka kutajwa, aliambia BBC kwamba wanafunzi waliamrishwa kupanga foleni na kusema majina yao mmoja baada ya mwingine kabla ya kuuawa.
Haijulikani kwa nini baadhi waliuawa na wengine kuachwa, baadhi ya wale waliouawa ni waisilamu.
"kila mtu anaogopa na wamejifungia vyumbani," alisema mhadhiri huyo.
Aliongeza kuwa wanafunzi sasa wameanza kuuhama mji huo. Inasemekana wameweka majani ya rangi ya kijani kibichi kwenye magari yao kama ishara kuwa hawaungi mkono upande wowote.
Wapiganaji wa Boko Haram wanaopigana wakitaka sheria za kiisilamu kutumika, wamewaua zaidi ya watu 1,000 Kaskazini mwa Nigeria

Mlipuko, majeshi yakidhibiti Kismayo



Wenyeji wakiuhama mji wa Kismayo
Mlipuko mkubwa umesikika mjini Kismayo huku wanjeshi wa Somalia wakishirikiana na majeshi ya AU, ambao wamedhibiti maeneo muhimu ya mji wa Kismayo.
Wenyeji wanasema kuwa mlipuko huo ulisikika kama bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara ingawa hakuna majeruhi wameripotiwa.
Shambulizi hilo linakuja baada ya wapiganaji wa Al-Shabab wanaohusishwa na kundi la kigaidi la al-Qaeda, kuondoka Kismayo ambayo ndiyo ngome yake kubwa mwishoni mwa wiki.
Jeshi la Somalia limesema vikosi vyake vikishirikiana na wanajeshi wa kudumisha amani wa Muungano wa Afrika, AMISOM tayari vimeuteka Mji wa Kismayo, ambao ndiyo ngome kuu ya mwisho ya kundi la wapiganaji la Al - Shabaab.
Kamanda wa Jeshi katika eneo hilo Ismael Sahardiid ameiambia BBC kwamba wanamiliki taasisi zote za Serikali, Bandari pamoja na Uwanja wa ndege.
Jumamosi iliyopita, kundi la Al Shabaab lilisema limetumia mbinu ya kujiondoa kutoka kwenye Mji huo na linaendelea kutekeleza mashambulizi ya kujitolea muhanga katika maeneo wasioyamiliki tena.
Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir, majeshi ya Kenya na Somalia sasa yanasimamia Kituo kikuu cha Polisi cha Kismayo na Uwanja mpya wa ndege. Aliongezea kuwa pindi tu hali itakapokuwa shwari na salama, ndege zitaruhusiwa kutua katika Uwanja huo wa ndege.
Chirchir amesema kuwa wataalamu wa mabomu wametegua vilipuzi vilivyokuwa vimetegwa katika uwanja huo wa ndege na wapiganaji wa Al-Shabaab wenye uhusiano na kundi la Al-Qaida.
Vikosi vya Muungano wa Afrika vinaisaidia Serikali changa ya Somalia kudumisha amani katika Nchi hiyo iliyokumbwa na misukosuko tangu mibabe wa kivita walipoupindua Utawala wa muda mrefu wa kidikteta mwaka 1991.

Sunday, September 30, 2012

Shule ya kanisa yashambuliwa Nairobi

Shambulio la guruneti la mkononi dhidi ya shule ya Jumapili ya watoto wa Kikristo mjini Nairobi limeuwa mtoto mmoja na kujeruhi wengine kadha.


Polisi wa Kenya

Taarifa zinazohusianaKenya, GhasiaMkuu wa polisi wa Nairobi, Moses Ombati, ameliambia gazeti la Daily Nation kwamba watu watatu wamekamatwa, na kwamba watu hao walionekana wakipiga picha za kanisa la Saint Polycarp lilolengwa.

Msikiti ulio karibu na hapo ulishambuliwa na vijana waliokuwa na hasira.

Afisa wa polisi wa Nairobi aliwasihi watu wawe watulivu.

Shambulio lilitokea katika mtaa wa Juja Road, unaopakana na mtaa wa Eastleaigh.

Inaaminiwa kuwa guruneti lilirushiwa kanisa la Saint Polycap kama saa tano punde baada ya misa ya asubuhi.

Al-Shabaab waondoka Kismayo

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Somalia, Al Shabaab linasema kuwa limeondoka katika ngome yao kubwa iliyobaki, yaani mji wa Kismayo.
Kismayo


Wakaazi wa Kismayo waliiambia BBC kwamba wapiganaji hao waliondoka usiku na kwamba mji sasa ni shuwari.

Majeshi ya Kenya na serikali ya Somalia, ambao walikuwa wakipigana na Al Shebaab kilomita kadha nje ya mji hapo jana, bado hawakuingia mjini.

Kismayo ni bandari ya pili ya Somalia kwa ukubwa na ikileta pato muhimu kwa al-Shabaab.

Wakaazi wa Kismayo wanasema waliamka leo asubuhi na kukuta Al Shebaab wameshaondoka.

Kwenye ukurasa wao wa mtandao wa internet wa twitter, kundi la al-Shabaab limetoa tangazo hili: "jana usiku, baada ya miaka mitano, utawala wa Kiislamu mjini Kismayo ulifunga ofisi zake".

Wanajeshi wa Kenya na serikali ya Somalia bado hawakuingia ndani ya mji.

Msemaji wa jeshi la Kenya aliiambia BBC kwamba ana wasiwasi kuwa kuondoka kwa al-Shabaab pengine ni mtego.

Kwa hivo kwa sasa, Kismayo haidhibitiwi na mtu yoyote.

Yote yanategemea vipi serikali ya Somalia na washirika wao wa Umoja wa Afrika watavosarifu maslahi yao yanayogongana, kudhibiti mji huo wenye bandari na unaoleta pato

Mkakati wa Kenya Somalia wasonga mbele

Wakati majeshi ya Kenya na Somalia yanakaribia mji wa Kismayo, sehemu ya mkakati wa miaka mingi wa Kenya karibu kukamilia.



Waziri wa uLinzi wa Kenya, Mohamed Yusuf Haji (kulia) na Waziri  Mkuu, Raila Odinga (kati)


Mpango wa kuwa na eneo la salama la kuzunguka mipaka ya Kenya karibu kukamilia:



Kwa miaka mingi, imekuwapo siri ambayo siyo siri tena, kwamba Kenya itapenda kuona taifa salama linaundwa nje ya mpaka wake na Somalia.



Huo ndio unaitwa makakati au mradi wa Jubaland.



Mpango huo unaungwa mkono na Wasomali wa Kenya.



Kati ya hao ni Waziri wa Ulinzi wa Kenya, Mohamed Yusuf Haji na mwanawe, Nuradin Yusuf, afisa wa ujasusi katika jeshi la Kenya.



Wote hao wanatokana na koo za Ogaden, ambazo zimetapakaa kaskazini mwa Kenya, kusini mwa Somalia na katika jimbo la Wasomali mashariki mwa Ethiopia.



Lakini kulikuwa na tatizo moja kubwa katika kuunda Jubaland, nalo ni upinzani wa Ethiopia.



Tangu miaka ya 1980, Waethiopia wamekuwa wakipigana vita na kundi la ONLF, wapiganaji wa jimbo la Ogaden.



Serikali ya Ethiopia inapinga kabisa wazo hilo la kuwa na Jubaland, ikiwa itaruhusu ONLF kuwa na kambi kupigana na majeshi ya Ethiopia.



Kwa hivo awali mwezi huu Waziri wa Ulinzi wa Kenya alipatanisha na kuleta makubaliano baina ya wapiganaji hao na serikali ya Ethiopia.



Kwa hivyo kikwazo cha mwisho dhidi ya mradi wa Jubaland sasa kimeondoka, na hivo kusukuma shambulio la hivi sasa dhidi ya Kismayo.



Tatizo moja limebaki: watu wa Kismayo siyo wa koo za Ogaden, na hiyo ndio sababu moja watu waliunga mkono al-Shabaab.



Kenya itabidi kusikiliza wasiwasi wao, ikiwa inataka kufanikiwa kukamilisha mradi wa Jubaland

New