Mshirika mkubwa wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, amefunguliwa mashtaka mjini Abidjan, katika kesi ya kwanza ya watu waliotuhumiwa kwa ghasia za baada ya uchaguzi wa kati ya mwaka 2010 na 2011.
Bwana Gbagbo anasubiri kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC. Anakana madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita.
Ivory Coast imekuwa ikituhumu washirika wa Gbagbo, katika nchi jirani ya Ghana kwa kufanya uvamizi mipakani kwa lengo la kuitikisa serikali ya Rais Alassane Ouattara.
Mwandishi wa BBC John James anasema kuwa mahakama ilifurika watu kushuhudia kuanza kwa kesi ya Generali Dogbo Ble
Generali Ble, anayetoka kabila la bwana Gbagbo, aliibuka kama kamanda wa jeshi wakati wa vurugu la mwaka 2011 la kutaka udhibiti wa Abidjan, na kuendeshea harakati katika kambi ya muda iliyokuwa katika ikulu ya rais.
Alikuwa mmoja wa majenerali, ambao hawakumuunga mkono Rais Ouattara wakati wa kilele cha mapigano hayo.
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamepongeza hatua ya kumfungulia mashtaka kamanda huyo lakini wanaonya kuwa lazima kesi iendeshwe kwa usawa au la sivyo itaibua taharuki nchini humo
No comments:
Post a Comment