Mataifa ya Afrika Magharibi
yanajitayarisha kukamilisha mipango yao ya kuingilia kijeshi nchini
Mali, kuwaondoa wapiganaji wa Kiislamu walioteka zaidi ya nusu ya nchi
hiyo kufuatia jaribio la kupindua serikali mwezi Machi.
Lakini hadi sasa ni mataifa machache tu ya Afrika Magharibi ambayo yamejitolea kutoa wanajeshi kwa kikosi hicho.
Baadae juma hili, Umoja wa Mataiafa, wakuu wa Ulaya na Umoja wa Afrika watajumuika na wawaikilishi wa Mali mjini Bamako, kujaribu kutafuta mkakati imara wa kuingia Mali kijeshi.
No comments:
Post a Comment