Takriban polisi kumi wa Kenya wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi la guruneti
Maafisa hao wa polisi walikuwa wanasaka nyumba
moja mjini Mombasa, pwani mwa Kenya ambako walipata silaha ikiwemo
bunduki aina ya AK-47 na maguruneti mawili.Kenya kwa muda sasa imakumbwa na misururu ya mashambulizi ya maguruneti, tangu wanajeshi wake walipoingia Somalia kupambana na wanamgambo wa Al Shabaab mwaka jana.
Mkuu wa Polisi mkoani humo, Aggrey Adoli,aliambia waandishi wa habari kuwa washukiwa watatu wa kigaidi waliuawa katika makabaliano kati yao na polisi baada ya shambulizi hilo.
Washukiwa wa Al-Shabab wametekeleza mashambulizi kadhaa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita eneo la Pwani ambalo ni maarufu kwa watalii.
Wanajeshi wa Kenya nao wamekuwa vitani kuondoa kundi la Al Shabaab kutoka katika ngome yao kubwa na ya mwisho ambayo ni Kismayo kwa ushirikiano na wanajeshi wa Muungano wa Afrika tangu Oktoba mwaka jana, jambo ambalo walifanikisha mwanzoni mwa mwezi huu.
No comments:
Post a Comment