Mkuu wa mashtaka wa Misri,
AbdalMajid Mahmoud, amerejea ofisini na ulinzi mkali na hivo kukaidi
amri ya Rais Mohamed Morsi ya kumtoa kazini.
Mkuu wa mashtaka na wafuasi wake wanasema rais hana madaraka hayo.
Kuachiliwa kwa washtakiwa hao kulizusha maandamano ya ghasia katika medani ya Tahrir mjini Cairo Ijumaa, ambapo watu zaidi ya mia moja walijeruhiwa kwenye maandamano makubwa kabisa dhidi ya rais tangu kushika madaraka mwezi wa Juni.
Mkuu wa mashtaka, Abdel Maguid Mahmoud, alirudi ofisini mwake huku amezungukwa na walinzi na mamia ya mahakimu na mawaikili.
Alitaka kuonesha uhuru wake baada ya Rais Morsi kujaribu kumtoa kazini, kwa kumteua kuwa balozi wa Misri Vatikani.
Inaarifiwa kuwa majaji kadha walitishia kujiuzulu piya.
Tena mkuu wa mashtaka alikwenda kwenye mkutano na mmoja kati ya ma-naibu wa rais kujaribu kuzimua mambo.
Wakati wa serikali ya zamani kulikuwa na malalamiko mengi kuwa mahakimu na maafisa wa mashtaka wakishawishiwa na serikali.
Sasa, chini ya serikali mpya, wanajaribu sana kuonesha uhuru wao.
Hichi kisa kimeleta aibu kwa rais - na tayari kuna ishara kuwa anajaribu kubadilisha uamuzi wake wa kumtoa kazini mkuu wa mashtaka.
No comments:
Post a Comment