Hili lilikuwa tangazo kwa ajili ya maandamano ya leo.
Magari ya Jeshi la Wananchi yakipita katika mitaa ya Kariakoo kuwataarifu wananchi kutawanyika eneo hilo.
Baada ya baadhi ya waumini wa
dini ya Kiislamu kutawanywa kwa mabomu na askari wa Kikosi cha Kutuliza
Ghasia hapo awali, kwa sasa waumini hao wanajipanga kuvamia kituo cha
polisi mtaa wa Msimbazi wakiwa katika makundi makundi mikononi wakiwa na
mawe na wakiimba nyimbo. Awali magari ya Jeshi la Wananchi yalipita
mitaa ya Kariakoo yakiwa na wanajeshi waliokuwa wakiamuru wananchi
kutawanyika lakini hali inaonekana kubadilika maana kwa sasa waumini hao
wanajikusanya upya kutimiza azma yao ya kuandamana mara baada ya
kumaliza swala ya saa 10 katika msikiti wa Idrissa uliopo Kariakoo.
Baadhi ya madai ya waumini hao ni KUKAMATWA SHEIKH PONDA, KUTOONEKANA
KWA SHEIKH FARIDI WA ZANZIBAR NA KUKOJELEWA QURAN.KARIAKOO DAR LEO HAKUNA MSONGAMANO WA WATU
FFU wakizunguka maeneo ya Kariakoo leo huku wakitumia kipaza sauti kuwataka wananchi wote kurejea majumbani kwao |
Hili ni eneo la Msimbazi ambalo kwa kawaida huwa kuna msongamano mkubwa wa watu |
Eneo la mzunguko wa Kariakoo ambalo jiupe kama unavyoliona hapa |
Hapa sio maduka yamefungwa muda umepita ama wahusika wamefiwa hapana ni baada ya vurugu kutokea |
Hii ni kariakoo sio biashara mbaya ni usalama hakuna |
Tukio hilo la kukosa
watu kabisa eneo hilo kama picha
zinazoonyesha limetokea leo kutokana na vurugu kubwa
vilizoibuka toka majira ya mchana
eneo hilo vurugu zilizohusisha jeshi la
polisi kikosi cha
kutuliza ghasia (FFU) na badhi ya
waumini
wa dini ya kiislam ambao
wanashinikiza wenzao ambao
wanashikiliwa kwa tuhuma
za kufanya vurugu na
kupora mali wakati wa vurugu
za waumini wa dini
hiyo katika eneo la Mbagala .
Vurugu hizo
ambazo chanzo chake ni watoto
kugombana na mmoja kati ya watoto
hao wawili ambaye ni mkristo
kukojolea Msaafu jambo
lilozua vurugu na hata waislam
kuandamana na kuchoma makanisa .
Hivyo kutokana na utata huo
leo mkuu w mkoa
wa Dar es Salaam na kamanda
wa polisi kamnda maalum ya Dar
walionya kutokuwepo kwa maandamano ila
bado watu sita wafuasi wa Sheikh Ponda
waliokua wakiandamana kwenda Ikulu kabla ya
kukamatwa na polisi na
ndipo vurugu zilipoanza.
Wakati vurugu
hizo zikianza eneo la Kariakoo na maeneo mbali mbali ya jiji maduka na
benk zote zilifungwa pamoja na wananchi kutawanywa kuondoka
maeneo hayo .
Mtandao huu
umeshuhudia wananchi wakitawanywa
na waliopo ndani kama ni zaidi ya
watano walikuwa wakitolewa kwa virungu huku baadhi ya wananchi
wakijeruhiwa kwa kukimbia vurugu
na wengine kwa kupigwa na polisi na mgambo
wa jiji.
Vipo taarifa ambazo bado
kuthibitishwa kuwa watu
kadhaa wamejeruhiwa vibaya na
mali mbali mbali ikiwemo pikipiki
mmoja kuchomwa moto .
Hadi
mwandishi wa mtandao huu anaondoka eneo hilo la Kariakoo tayari magari ya
wanajeshi wa JWTZ yalikuwa yakifika
eneo hilo huku polisi wakitawanywa katika misikiti mbali mbali kuthibiti hali hiyo.
Baadhi ya wananchi
wamemwomba Rais Jakaya Kikwete
kusitisha safari zake za nje na kuingilia kati kurejesha amani na utulivu nchini huku
baadhi wakidai kuwa kitendo
kinachofanywa na waislam hao
ni kuiharibia dini
hiyo kwa waumini wake kukosa imani kwa wananchi pindi wanapoomba nafasi mbali mbali za uongozi hivyo
kumwomba kiongozi wa waislam nchini kutoa tamko dhidi ya haya yanayoendelea
ili kurejesha imani kwa watanzania.
Uchunguzi wa mtandao
huu pia umebaini kuwa vurugu
hizo zinachochew zaidi na polisi na mgambo ambao wamekuwa
wakiwapiga wananchi hata wasio na hatia na baadhi ya askari wakizunguka maeneo mbali mbali na
kuwatoa nje watu
waliojificha ndani ya nyumba na maduka yao bila kuangalia na muumini wa dini ya kiislam ama mkristo na kuwakamata .
Moja kati ya
maswali ambayo polisi wanapaswa
kujibia ni pamoja na hili kuwa
maandamano ya waislam ,wakristo wanakamatwa na kupigwa kwa sababu zipi? Pili kwa waislam
kwanini wanafanya maandamano kwa jambo ambalo lipo tayari mahakamani ?
Mungu ibariki Tanzania ,Mungu wabariki
viongozi wa Tanzania na Mungu
wabariki waumini wa dini
zote ili kuifanya Tanzania kubaki kuwa nchi ya Amani.
No comments:
Post a Comment