Ujio wa mtandao mpya wa kijamii kupitia simu za mkononi aina ya BlackBerry almaarufu BBM, sasa umezua kasheshe miongoni mwa mastaa wa Bongo waliojisajili kwenye huduma hiyo.
Kasha la upekuzi wa gazeti hili limesheheni habari mbichi za hivi karibuni kuwa, chokochoko, ugomvi na kumalizana kistaa, shetani wake ni meseji za umbeya zinazotundikwa na wadau wa mtandao huo.
UNATAKA KUJUA ZAIDI?
Habari zisizokuwa na chenga kutoka kwa baadhi ya wanachama wa BBM zinafafanua hivi: “Mtandao huu unawachonganisha sana mastaa na hasa akina dada, utakuta mtu anakutungia jambo na kuliweka kwenye ukurasa wake, lengo likiwa ni kukuharibia.
“Wanaosoma posti hiyo ya umbeya wanaamini, wanaanza kukutukana au kukudhalilisha, matokeo yake ni kuwekeana bifu zisozokuwa na msingi,” alisema Jane Abbas, mtumiaji wa BBM ambaye pia ni mwigizaji chipukizi.
VIONJO VYA MESEJI ZA BBM
Hakuna ubishi kwa sababu, timu ya Gazeti la Risasi mchanganyiko imeshuhudia baadhi ya meseji za vijembe vya baadhi ya mastaa zikisomeka: “Msanii maarufu hawezi kuishi Manzese (eneo moja jijini Dar). Usipende kuiga tembo we mwanamke. Mzuri atakuwa yeye?”
Inaelezwa kuwa maneno yenye sura hiyo huwa ni sawa na dongo gizani, atakayelia na kujibu kwa jazba ujue ujumbe umemgusa na kutoka hapo mtafutano wa kitemi huanza safari zake.
HITIMISHO
Mbali na matumizi hayo mabaya ya mtandao huo, wapo baadhi ya watu ambao hutumia BBM kuhabarishana ishu za kijamii na hivyo ‘kuwakipu bize’ muda mwingi. Mfano ni picha za ukurasa wa mbele ambazo mastaa walipigwa siku moja wakati Irene Uwoya akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa yaani birthday.
No comments:
Post a Comment