Wadandiaji wa treni nchini Indonesia wakiwa kwenye treni liendalo mkoa wa Banten.
• Yatawekwa matufe ya zege kwenye madaraja juu ya reli
MAMLAKA za reli nchini Indonesia zimeamua kupambana na watu wanaokwepa kulipa nauli kwenye treni kwa kuning’iniza matufe ya zege katika madaraja juu ya reli hususani kwa wakwepaji ambao hupanda juu ya mapaa ya treni.
Kwa mujibu wa maofisa wa shirika la reli ambalo ni la umma, matufe hayo yenye umbo la mipira lakini yaliyotengenezwa kwa zege yatakomesha watu wanaohatarisha maisha yao kwa kusafiri wakiwa nje kwenye mapaa ya treni.
Msemaji wa shirika hilo, P.T. Kerea Api alisema: “Tumefanya kila kitu mpaka kuweka seng’enge za miiba lakini haikuwezekana, labda hatua hii itafanikiwa.”
Hatua za kupambana na watu hao zimekuwa zikigonga mwamba kila mara ambapo wakwepa nauli hao wamekuwa wakiwashambulia maofisa wa reli kwa mawe, na pale ambapo walijaribu kuweka matufe mara ya kwanza, nyaya za kuyaning’iniza zilikuwa fupi mno kiasi hayakuweza kuwafikia wadandiaji.
Hivyo, watu watabidi kuchagua kulipa nauli au kubondwa na matufe hayo.
No comments:
Post a Comment