Rais Jakaya Kikwete kushoto akiwa na Rais Barack Obama
....................................................................................
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, SAID MECK
SADICK, amesema serikali imechukua tahadhari zote katika kuhakikisha
shughuli zote za wananchi za kibiashara zinaendelea kama kawaida wakati
wa ziara ya rais wa Marekani Barack Obama.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema katika kipindi hicho wafanyabiashara
kutoka mikoani na ndani ya jiji wataendelea kuingiza bidhaa zao katika
masoko kama kawaida bila kuzuiliwa, na kwamba si barabara zote
zitakazofungwa na kutolea mfano wa barabara itakayofungwa kuwa ni
barabara ya Nyerere ambayo wageni wengi hutumia na kwamba ziara hiyo
haitaathiri maonesho ya 37 biashara maarufu kama sabasaba yanayoendelea
katika viwanja vya Mwl. JULIUS NYERERE.
Rais wa Marekani Barack Obama anatarajia kuzuru Tanzania siku ya
jumatatu ambapo miongoni mwa masuala atakayoangazia ni pamoja na
kuhamasisha demokrasia na kukuza fursa za kiuchumi.
Maandalizi ya mapokezi ya Rais Obama yamezidi kupamba moto hasa katika
jiji la Dar-es salaam ambapo ndipo kituo chake cha kwanza kwa rais huyo
nchini Tanzania huku suala la usafi na matengenezo katika barabara
nyingi Jijini likionekana kupewa kipaumbele tofauti na siku zote.
Pia abiria wa ndege na wale wa
mabasi ya mikoani wametakiwa kuripoti mapema katika vituo vyao ili
kuepuka kukosa usafiri siku hiyo ,huku akitaka mabasi ya mikoani
ambayo yanaondoka baada ya saa 3 kuzingatia muda kwani baada ya saa 3
barabara zitafungwa hivyo kukosa kusafiri hadi ugeni utakapoondoka
No comments:
Post a Comment