Hoja  kubwa ya msingi leo ni jinsi gani mwanamke anaweza kuolewa haraka na mpenzi  wake. Ikumbukwe kwamba,  hapa tunazungumza na wanawake ambao tayari wapo katika  uhusiano, lakini  wenzi wao hawana habari kabisa na mambo ya  ndoa.
  
Leo  nazungumzia juu ya wewe  ambaye upo katika uhusiano ambao haueleweki, lakini  ndoa unaitaka.  Unajua cha kufanya? Soma hapa chini mambo ya kufanya ili mpenzi  uliyenaye akuoe haraka...
  
1.EPUKA MAKUNDI  MABAYA
  
Mwanaume anapenda kuwa na mke  mwenye staha,  ambaye hana tabia za hovyo. Kuwa na makundi ya  ‘mashangingi’ ni alama ya kwanza  kabisa kuwa unapenda au tayari una  tabia za  kishangingi. Wanaume wengi hawapendi kabisa wanawake wenye  tabia za hovyo,  wenye kampani ambazo si nzuri.
  
Lakini yawezekana, jamaa  alishakuambia juu ya  kilio chake hiki, lakini wewe umekuwa kama umeweka  pamba masikioni mwako, hili  ni tatizo. Linda heshima yako, kaa mbali na  makundi hatari, ili umfanye jamaa  akuone wewe ni mwanamke thabiti ambaye huigi, hushabikii na wala huna tabia  mbaya. Utaonesha hili kwa kukaa  mbali na makundi ya wanawake  hatari! 
  
2. ZINGATIA MAVAZI  YAKO
  
Kila mtu anamjua mtu wake alivyo, mwanamke hata  wewe unamjua mpenzi wako alivyo. Sina shaka unafahamu  anapenda nini na nini  anachukia. Unajua kabisa, nina uhakika na hilo.  Lakini pamoja na kwamba jamaa  anaweza kuwa na vitu ambavyo vinamvutia  zaidi, hata wewe kama mtoto wa kike,  una mapendekezo yako au vitu  ambavyo unapenda zaidi  kuvifanya!
  
Huzuiwi, lakini swali la msingi,  mwenzi wako  anapenda? Kama wewe unapenda sana skin jeans na top  inayoacha kitovu nje, yeye  hapendi kwa sababu ana nia ya kukufanya mke  hapo baadaye. Sasa utakuwa mke gani  ambaye hata Salim anaona sehemu zako za faragha  hadharani?
  
Ukiachana na chaguo la mwenzi  wako, lakini  lazima wewe mwenyewe kama mwanamke wa mtu, ujitambue!  Jisitiri vyema. Kwani  kuna urembo gani wa kuvaa nguo inayoonesha mwili  wako ulivyo? Kuna burudani  gani kuacha nyeti zako wazi? Unataka nani  akuone ulivyo? Mke hana sifa hiyo  dada yangu, sasa ili uweze kuwa na  sifa hii muhimu, lazima uzingatie sana  mavazi yako.
  
3. JIPE  MOYO
  
Hili nilishawahi kulizungumza  sana katika mada  zilizopita, baadhi ya wanawake wamekuwa wakikatishwa  tamaa na rafiki zao au  watu wengine wanaowazunguka, eti hawana hadhi ya  kuolewa au watahangaika sana  lakini hawatapata mume, kisa eti HAVUTII!
  
Mwingine anajinyima mwenyewe  nafasi akisema;  “Mimi nina balaa, sina bahati ya kuolewa, ndiyo maana  wadogo zangu wote  wameolewa nimebaki mimi.”
  
Huu  ni uvivu wa kuwaza. Lakini dada yangu, habari iliyo njema kwako ni kwamba, ndoa  unaitengeneza wewe mwenyewe.
  
Unaitengeneza kwa misingi ya  kwanza, kujipa  moyo mwenyewe kwamba wewe ni mzuri na una sifa na haki za kuolewa kama wanawake  wengine. Jipe moyo mwenyewe, huna nuksi wala  balaa, wewe ni mzuri na una sifa  za kuwa mke hapo baadaye.
  
Iko  hivi, ukianza kujishusha  mwenyewe, ni dhahiri kwamba hata mavazi yako  hayatakuwa mazuri, uso wako hautakuwa na tabasamu na wala hutakuwa na matumani  moyoni, hapo sasa ni mwanzo wa kuzorota afya yako. Utapata mchumba kweli?  Utasubiri sana kwa mtindo huo. 
4. ACHA PAPARA
  4. ACHA PAPARA
Haizuiwi kuuliza kuhusu  mustakabali wa uchumba  wenu, lakini ni vizuri basi kuwa na kiasi.  Kuuliza kila wakati au kuwa mtu wa  kulaumu, hakutakusaidia kumfanya  jamaa achukue maamuzi ya haraka ya kukuoa na  badala yake yanaweza kumpa  picha tofauti.
 Ni rahisi kuwaza kwamba, unachohitaji kwake ni ndoa na baada ya hapo hutakuwa na staha tena. Kuwa mjanja, achana na papara. Usilogwe ukamfanyia jambo zuri mpenzi wako, halafu ndiyo umuulize; “Sasa honey, mbona hata huzungumzii ndoa yetu? Hivi utanioa kweli? Eeeh baby? Niambie basi mpenzi wangu


