Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde kutoka Mkoani Arusha
zinaeleza kuwa Ndege Ndogo ya Shirika la Ndege la TANZAIR iliyokuwa
ikitokea Mjini Bukoba kuelekea Jijini Dar es Salaam, imelazimika kutua
katikati ya Ziwa Manyara lililopo Mkoani Arusha ili kunusuru abiria wake
sita (6) waliokuwamo katika ndege hiyo baada ya kupatwa na hitilafu kwa
kuzima ghafla kwa Injini moja wakati ikiwa hewani.
Aidha imeelezwa kuwa katika tukio hilo ni abiria watatu tu ambao
wamepatwa na majeraha makubwa huku wakipelekwa kupatiwa matibabu katika
Hospitali ya Sirialni ya Mkoani Arusha, huku wengine wakitazamiwa na
kuchunguzwa kabla ya kuruhusiwa kuweza kuendelea na safari.
Rubani wa ndege hiyo alilazimika kutaka kutua ghafla katika Uwanja wa
Arusha, kutokana na Hitilafu hiyo, lakini alishindwa baada ya kuona
mtikisiko ukizidi na kuamua kuielekeza ndege hiyo katikati ya Ziwa hilo,
ambapo alifanikiwa kutua salama na baadhi ya Boti na mitumbwi iliyokuwa
karibu iliweza kusogea na kutoa msaada wa kubeba abiria hao na
kuwasogeza nchi kavu na baadaye ilifika Helkopta ambayo iliweza kutoa
msaada zaidi.
No comments:
Post a Comment