Wasiwasi wa muungano wa mataifa ya Magharibi kuishambulia Syria
umenukia, kufuatia Marekani, Uingereza na Ufaransa kusema kuwa itatoa adhabu kwa
taifa hilo la kiarabu kwa kutumia silaha za kemikali katika mapigano dhidi ya
waasi nchini humo juma lililopita.
Mataifa ya Magharibi, yakiongozwa na Marekani yanaunga mkono hatua ya kijeshi
dhidi ya Syria huku mataifa ya Mashariki na Asia yakiongozwa na Urusi
yakipinga.Hapa uamuzi ulifanywa, kupitia Umoja wa Mataifa, kuwa wataalamu wa silaha za kemikali wa Umoja huo, wasafiri hadi Syria ili kuchunguza ukweli. Baada ya kushawishi Serikali ya Rais Assad kwa muda, idhini ilitolewa na pia wanajeshi wa Syria wakaahidi kuwa siku hiyo ya kuchunguza mapigano kati ya Serikali na waasi wanaoungwa na mataifa ya Magharibi watasitisha mapigano.
Juma lililopita wachunguzi hao walishambuliwa na wadenguaji mara mbili wakielekea kwenye eneo la kuchunguza, na isitoshe muda mfupi baadaye shambulio kubwa zaidi la silaha za kemikali likafanywa katika makaazi wa waasi, karibu sana na jiji la Damascus.
Kufuatia shambulio la pili ilikuwa wazi sasa kuwa Marekani, Uingereza na Ufaransa ziko tayari kushambulia.Suala la pekee ambalo hadi dakika hii watu wanajiuliza ni, lini?
No comments:
Post a Comment