Waziri
wa masuala ya Nje wa Marekani John Kerry amekashifu matokeo ya uchaguzi
ya Burundi yaliyotolewa hapo jana ambapo rais Pierre Nkurunziza
alitangazwa kusajili ushindi mkubwa.
Kerry ametaja uchaguzi huo
kuwa ukiukaji mkubwa wa katiba na kejeli kwa mfumo wa haki huku
akimlaumu rais Pierre Nkurunziza kwa ghasia zilizotokea nchini humo wiki
chache kabla ya kufanyika uchaguzi.Amesema kuwa rais huyo ametumia mbinu ghushi kung'ang'ania madarakani katika uchaguzi ambao sio huru wala wa haki.
Amesema kuwa hii ndio njia ya pekee ya kurejesha imani sio tu ya raia wa Burundi bali jamii ya kimataifa pia, na kuzuia ghasia zaidi nchini humo zilizosababisha watu kuikimbia nchi.
Hapo jana tume huru ya uchaguzi nchini Burundi ilitangaza kuwa rais Nkurunziza amepata asilimia karibu sabini ya kura zilizopigwa katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumanne wiki hii.
Viongozi wakuu wa upande wa upinzani nchini Burundi walisusia uchaguzi huo,lakini majina yao yalisalia katika karatasi za kupigia kura.
Kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa alimaliza katika nafasi ya pili akizoa asilimia kumi na tisa ya kura zilizopigwa.
No comments:
Post a Comment