Rais
wa Marekani Barrack Obama amesifu uwezo wa biashara na uchumi wa bara
Afrika kwenye hotuba yake ya kwanza tangu aingie nchini Kenya siku ya
Ijumaa.
"Africa inasonga mbele,.. watu wanainuliwa kutoka kwa umasikini.Obama alisema hayo kwenye hotuba ya uzinduzi wa Kongamano la wajasiria mali.
Rais Obama alizuru kumbukumbu ya ubalozi wa Marekani uliolipuliwa na bomu mwaka wa 1998, kabla ya majadiliano ya usalama na rais wa Kenya katika ikulu ya Nairobi.
Obama ni rais wa kwanza wa Marekani kuzuru nchi ya Kenya.
Shughuli ya kwanza ya Obama ilikuwa ni kuhutubia Kongamano la wajasiria mali kutoka mataifa 120 kote duniani.
Alisema Afrika yapasa kuwa chemchemi ya maendeleo ya siku za usoni, na kuongeza kuwa serikali zinafaa kuhakikisha kuwa ufisadi haukiti kambi.
Rais Obama hivi sasa yuko katika ikulu ya Nairobi anakotarajiwa kutia sahihi makubaliano ya kiuchumi baina ya taifa lake na Kenya.
No comments:
Post a Comment