My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, March 29, 2016

UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KAMA MRADI



MAHITAJI

1. Kuku(tetea) 10 na Jogoo 01
2. Banda bora
3. Vyombo vya chakula na maji
4. Chakula bora
5. Madawa na chanjo kwajili ya magonjwa
6. Chanzo cha nishati joto na mwanga
7. Elimu na ujuzi wa malezi bora
8. Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga
9. Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa)
10. Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu 

KUKU 10
Wakati wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 10 (matetea) wenye umri sawa na hawajawai kutaga hata mara moja. Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika familia bora kutegemea malengo ya mradi wako. Mfano kama lengo lako ni kuzalisha kuku wa kienyeji kwa ajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa haraka na yenye uzito mkubwa,Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi.
Ili kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao. Kuku hawa utawapata kwa bei ya chini, tena watafaa sana maana watakua na umri mmoja

 JOGOO 01
Jogoo mmoja tu anatosha kuwahudumia kuku matetea yote kumi.
 Hakikisha katika uchaguzi wa jogoo bora lililochangamka, rangi mzuri, upanga umesimama, macho angavu, uzito wa kutosha, rangi nzuri na uwezo mkubwa wa kuzalisha. Ni vema mfugaji akaelewa kwamba kuku wote watakaozalishwa watategemea ubora wa jogoo wake. Uwezo wa kutaga kwa kuku na upatikanaji wa mayai pia hutegemea kwa karibu ubora wa jogoo aliyechaguliwa.

 BANDA BORA
Miongoni mwa mambo mhimu naya kwanza kuzingatiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji kama mradi ni maandalizi ya banda bora. Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Mfugaji anatakiwa kuandaa banda lenye ukubwa wa mita 10 kwa mita 04. 
Yaani urefu uwe mita 10 na upana upana wa mita 04. Kisha kata vyumba vya mita 2 urefu na upana mita 4 kutoka katika banda lako hivyo utakuwa na jumla ya vyumba vitano vyenye ukubwa unaolingana. 
Ujenzi uzingatie malighafi na vifaa vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira husika. 
Mfano katika maeneo ambayo fito
zinapatikana kwa urahisi banda linaweza kuandaliwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo. 
Au sehemu ambayo mabanzi hupatikana kwa urahisi basi banda laweza kujengwa kwa kutumia mabanzi. 
Vifaa vya kujengea banda vizingatie pia gharama na upatikanaji wake katika eneo husika. 
Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-

Sakafu: Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito

Kuta: Fito, mabanzi, mbao, nguzo mianzi,udongo, matofali, mawe, mabati na wavu

Paa: Nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati na vigae.

Wigo: Matofali, mbao, fito nguzo, mabanzi, mianzi, matete, wavu na mabati

Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari.

Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.

Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.

Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala.

Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga.

Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo vya chakula na maji.

Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa.

Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga

JINSI YA KUFANYA

Wakuze kuku wako hadi watakapofikia muda wa kutaga. 
Wakianza kutetea ni kiashiria kwamba wakati wa kutaga umekaribia hivyo andaa viota kwajili ya kutagia.
Viota vinapaswa viwe na ukubwa stahiki ili kumwezesha kuku kuyafunika mayai yote vizuri wakati wa kuetamia, viota viwe vinavyozuia mayai kutawanyika, viwe mahali pakavu na safi.
Hakikisha kuku wote wanataga katika viota tofauti. Kuku anapotaga
mayai matatu unapashwa kuchukua mayai mawili na kumwachia yai moja ili kumfanya aendelee kutaga zaidi. Kuku akifikia yai la kumi na mbili anza kumwachia mayai matatu ili kumwandaa kwa kazi ya kutamia. 
Kwa kufanya hivi, kuku atataga mayai 15 au zaidi na ikiwa atataga mayai 15 au chini ya hapo nakushauri utafute mayai mengine ujazilizie ili kufikisha mayai 20 kwa kila kuku. Zingatia kwamba mayai unayoyatoa kwa kila kuku, yanatunzwa sehemu salama, mahali pakavu, pasafi na penye joto la wastani.
Kuku wote wanapaswa kuanza kuetamia kwa siku moja. Ili kufanikisha hili inapasa uwe karibu na kuku wako. Kuku mmoja akianza kutamia mwekee mayai ya kuku wa kisasa au mayai mabovu ya kuku wa kienyeji. Utafanya hivi hadi kuku wako wote watakapoanza kuetamia mayai. Kuweka mayai mabovu au mayai ya kuku yaliyotumika humfanya kuku aendelee kuetamia akijua ni mayai yake.
Baada ya kuona kwamba kuku wako wote wapo tayari kwa kuetamia mayai, waandalie banda maalumu kwajili ya kuetamia yani chumba kimoja katika lile banda letu. Ninashauri kwamba chumba kwajili ya kuetamia kiwe chumba cha kwanza au cha mwisho katika mfuatano wa vyumba vya banda lako. Andaa viota bora vya kuetamia, weka mayai 20 kwa kila kiota, ikiwa hayajatimia unaweza kununua kwa wafugaji wengine ili kuifikia idadi yako.
Waamishe kuku kutoka wanapotagia na kuwaweka katika chumba ulichokiandaa kwajili ya kuetamia. Ili ufanikiwe katika zoezi hili inafaa lifanyike wakati wa usiku na unafanya katika giza. Mweke kuku katika kila kiota na asubuhi wajikute kila mmoja katika kiota chake. Wahudumie kwa chakula na maji ya kutosha. 
Wakati wa usiku waongezee joto la ziada kwa kuweka jiko au ndoo ya chuma yenye chengachenga za mkaa au kama una umeme weka taa za joto.
Baada ya siku 21-25 kuku wako wataanza kuangua vifaranga. 
Huu ndio wakati unaotakiwa kuwa karibu sana na kuku wako kuliko wakati wote. Watenge vifaranga mara tu baada ya kuanguliwa; waweke katika chumba chao maalumu mbali na kuku. Kama chumba cha kutamia kilikuwa cha kwanza basi vifaranga wawe chumba cha mwisho n.k
Ukishawatenga vifaranga mbali na matetea wako, wawekee tena mayai mengine 20 kila tetea, mayai ambayo utayanunua kwa wafigaji wenzako. Hakikisha kuku waliotaga hayo mayai ni wazuri, hawana magonjwa na wanauzito/ukubwa unaofaa. Mayai yote yakaguliwe vizuri ili kujua kwamba yameharibika, yana nyufa au mabovu. Kabla ya kuweka mayai mengine hakikisha chumba chako ni kisafi na viota vimesafishwa, havina wadudu na uchafu wowote. Kuku wako bila kujijua wataanza kuetamia upya mayai uliowawekea.
Ukiwawekea mayai rudia mzunguko kama nilivyokwambia awali. Baada ya siku 21 hadi 25 tena utapata vifaranga wako wengine tena. 
Fuata kila hatua kama nilivyokwambia hapo awali. Lakini kwa awamu hii nashauri waache matetea wako wapumzike wala usiwapatie mayai mengine tena.

JINSI YA KULEA VIFARANGA
Ikikaribia siku ya 20 tangu ulipowawekea matetea wako mayai katika chumba cha kuetamia, andaa chumba kwa ajili ya kulea vifaranga. 
Safisha kwa kuondoa uchafu na wadudu wote.
Washa taa ya joto au weka chombo cha kutoa joto katika chumba cha vifaranga nusu saa kabla huja
anza kuingiza vifaranga wako. Weka pia chakula na maji ya kutosha katika vyombo vyenye umbile na ukubwa utakaowawezesha vifaranga kuvitumia. Tandaza magazeti, maboksi, makaratasi n.k katika sakafu ya chumba hicho. Hakikisha vifaranga wako hawajikusanyi sehemu moja maana wakifanya hivyo wengi wao watakufa ili ufanikiwe katika jambo hili, banda lako liwe la mduara katika kona zake.
Weka joto la kutosha. Joto la kutosha ni lile linalowafanya vifaranga watawanyike chini ya chanzo cha joto wakati kama joto limezidi vifaranya kukimbia mbali na chanzo cha joto na ikiwa joto halitoshi vifaranga hujukusanya chini ya chanzo cha joto.
Baada ya siku 3 utawapatia chanjo ya Gumboro na siku 7 wapatie chanjo ya New Castle, utarudia tena kuwapa chanjo hii baada ya mwezi mmoja kisha utafanya hivi kila baada ya miezi mitatu mitatu

MAPATO YA MRADI WAKO
Katika uzazi wa kwanza utapata vifaranga 150 kwa wastani wa vifaranga 15 kwa kila kuku. 
Tuseme haujazingatia kanuni za ufugaji za makala hii ukapata vifaranga 100 yani wastani wa vifaranga 10 kwa kila kuku. Kisha baadaye wakakua wakafa kuku 50 yani watano kwa kila kuku utakuwa na jumla ya kuku 50.
Baada ya wiki 3 utapata tena kuku tufanye kwa mahesabu kama hayo hapo juu kwa hasara utakuwa na kuku wengine 50, na kufanya jumla ya kuku 100. Ikiwa kuku wako baada ya uzao wa pili uliwapumzisha kwa miezi miwili basi mwezi wa 3 utapata tena kuku vifaranga 100 na wiki 3 baadaye utapata wengine 100. Kwa mahesabu kama hayo awali wakikuwa utakuwa na kuku wengine 100 ambao watakuwa.
Baada ya miezi 6 utakuwa na kuku wakubwa wa uzao wa kwanza 50, uzao wa pili kuku 50 na utakuwa na kuku wenye umri wa miezi mitatu 50 wa uzao wa 3 na kuku wengine 50 wa uzao wa 4.
Katika kuku 100 wa uzao wa kwanza na pili, tufanye kuku 50 wawe matetea ukijumlisha na kuku 10 ulioanza nao mradi utakuwa na matetea 60. Ikiwa kila tetea atatotoa vifaranga 10 na vikakua vitano tu, mwishoni utakuwa na kuku 300 na baada ya miezi mitatu kuku wengine 900 toka katika kutoka kwa uzao wa kwanza, wapili na watatu.
 Hivyo mwaka wa pili utafunga na kuku si chini ya 1,200/= wanaotaga mayai.
Ukiuza majogoo yote 1,200/= kwa bei ya 8,000/= ili upate pesa ya kujenga miundombinu bora maana sasa utakuwa na kuku wengi wanaoendelea kuzaliana kwa kasi utapata pesa kiasi cha TZS 7,200,000/=. Sasa ongeza kuku wako wa kutaga hadi wafikie kuku 4,000 maana sasa utakuwa na pesa za kutosha kuendesha mradi wako.
Sasa ukiwa na kuku 4000 wa kienyeji wa kutaga mayai, ikiwa kuku 3000 tu watataga ukauza yai moja kwa bei ya haraka haraka ya TZS 250 tu, utapata TZS 750,000/= kwa siku ambayo sawa na TZS 22,500,000/= kwa mwezi na TZS 270,000,000/= kwa mwaka sawa sawa na 128,572 USD. Kumbuka kwamba makadilio haya niya chini sana. Ukifata kanuni zote kwa makini na maombi huku ukimtanguliza Mungu utafikia hata TZS 500,000,000/= kwa mwaka.
Kumbuka unapofanikiwa kupata mapato ya kila aina, umtolee Mungu zaka(x10%) ya mapato yako, pia ukatoe sadaka ambayo ni kubwa kuliko zaka na uwasaidie masikini na wahitaji.

Tunza kumbukumbu zako zote za fedha katika daftari maalumu kuhusu mapato na matumizi ya mradi wako. Pia hali ya kuku wako kuhusu tarehe za chanjo ya mwisho, siku walipoanza kutamia, magonjwa yanayowasumbua mara kwa mara n.k

JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA.!



1. #Mathayo.
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali kwa kutetea kanisa. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.

2. #Simoni_Zelote (Mkananayo)
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishowe akafariki.

3. #Filipo
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.

4. #Yohana (nduguye Yakobo)
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na  alitolewa akiwa mzima kabisa. 

Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.

5. #Simoni (Petro)
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisulubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya "X". Petro mwenyewe aliomba asulubiwa kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18)

6.#Yakobo (wa Alfayo)
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe.  Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga na mawe mpaka akafa.

7. #Yakobo (mwana wa Zebedayo nduguye Yohana)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa lakini alichinjwa huko Yerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).

8. #Batholomayo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo. Alipigwa fimbo nyingi zilizochubua ngozi yake na kutengeneza vidonda. Kisha akawekewa chumvi ktk vidonda hivyo, na kuanikwa juani hadi mauti ilipomfika.

9. #Andrea
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la "X" miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri sana saa kama hii"

10. #Tomaso
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko.

11. #Yuda (Thadayo)
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

12. #Yuda (Iskariote)
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha. Alinunua shamba kwa zile fedha alizomuuza nazo Yesu. Lakini alijinyongea kwenye shamba hilohilo. Kamba aliyojinyongea ilikatika na akaanguka na tumbo lake kupasuka na matumbo kutoka nje. Shamba lile likaitwa "Akel Dama" yani Shamba la damu (Matendo 1:18-19).

NOTE:
13. #Mathia
Ni Mwanafunzi aliyechaguliwa kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (msaliti). Alipigiwa kura na wanafunzi 11 wa Yesu baada ya kifo cha Yuda (Matendo 1:26). Huyu alipigwa na mawe  hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

14. #Paulo
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka 65 (A.D). 

Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.

NB: Si muhimu kujua ni namna gani mitume walikufa, ila ni muhimu kujua kuwa mitume wote walikufa wakitetea imani yao. Walikua tayari kuchukiwa na kufa vifo vya mateso kwa ajili ya kumtetea na kumshuhudia Kristo.

Biblia imesema, "Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka." Mathayo Mtakatifu 10:23


Wednesday, March 23, 2016

MJUE NYANGUMI (WHALE)





MJUE NYANGUMI (WHALE), KIUMBE MKUBWA KULIKO WOTE TANGU DUNIA IUMBWE!
Mambo 10 sahihi kumhusu Nyangumi)

1.Nyangumi aina ya “Humpback” anaweza kula hadi tani 1 (kilo 1000) za chakula kwa siku, kila siku.

2.Watoto wa Nyangumi wa Bluu” wanazaliwa wakiwa na urefu wa mita 6 – 7, wakiwa na uzito wa tani 5.5 – 7.5. Wanakunywa lita 225 za maziwa yenye kiwango kikubwa cha mafuta kwa siku na wanaongezeka wastani wa kilo 3.7 kwa saa. Watoto hawa Nyangumi wanapofikisha miezi 8 wanakuwa na urefu wa mita 15 na tani 22.5 na wanabalehe wakiwa na umri wa miaka 10 – 15.

3.Nyangumi wa Bluu ndiye mkubwa kuliko kiumbe chochote kilichowahi kuishi duniani, anaweza kukua hadi kufikisha urefu wa mita 30 (kuzidi dege aina ya Boeing 737) na akawa na uzito wa tani 144 sawa na zaidi ya wanaume 2000 au tembo kadhaa. Nyangumi huyu ni mkubwa kushinda “Dinosaur”, mnyama aliyewahi kuishi duniani karne zilizopita.

4.Nyangumi aina ya “Sperm” ndiye mwenye ubongo mkubwa katika rekodi ya dunia ya viumbe duniani, ubongo wake unaweza kufikisha kilo 9, kichwa chake kina uwazi mkubwa ambao unatosha kupaki gari.

5.Nyangumi wote hawawezi kupumua kupitia midomo yao kwa sababu midomo imeunganishwa moka kwa moja na tumbo.

6.Ulimi wa Nyangumi wa Bluu “ulimi peke yake” unaweza kuwa na uzito sawa na tembo mmoja. Timu nzima ya mpira wa miguu inaweza kusimama juu ya ulimi huo.

7.Moyo wa Nyagumi wa Bluu una kilo 450 na mshipa mkuu wa moyo wake“Aorta” ni mkubwa kiasi kwamba mtoto anaweza kuogelea hadi mwisho.

8.Nyangumi aina ya “Southern Right” ndiye mwenye korodani “testicles” kubwa kuliko kiumbe yoyote duniani. Seti moja ya korodani zake zina uzito wa tani moja.

9.Nyangumi aitwaye “Bowhead” ambaye hutumia muda wake kwenye maji baridi ya “Arctic” ndiye huishi maisha marefu zaidi hadi kufikisha miaka 200. 

10.Nyangumi wa Bluu ndiye kiumbe mwenye sauti kuliko wote waliowahi kuishi duniani. Sauti yake inaweza kufika kilomita mia kadhaa mbali na alipo. Kwa vipimo vya kisayansi vya sauti “decibels”, Sauti ya ndege aina ya JET ndiyo yenye rekodi kubwa kwa kipimo cha “decibels 140”. Nyangumi huyu tunayemuongelea hapa pia hutoa “decibels 140” ambazo zinaweza kuumiza masikio ya mwanadamu.


Saturday, March 12, 2016

NAMNA YA KUMTAMBUA MWANAMKE MPUMBAVU.....



 MWANAMKE MPUMBAVU
1.Anamkomoa mumewe
2.Analala mapema kabla ya mumewe
3.Anachelewa kuamka kabla ya mumewe
4.Mbishi, anahic kuonewa mda wote
5.Anadhani kumnyima mumewe unyumba ni kumkomoa
6.Mmekaa sebuleni anahadithia tu
Mafanikio ya familia za wa2
Wakati ye ndo kigezo cha kero.
7.Hataki kuzungumzia mshara wake
8.We unajenga family ye anajenga
Kwao
9.Mkikaa 2 anaanza umbea kuponda
Ndugu na majirani
10.Haridhiki (mwanaume unatoa jasho
ila ye anakudiscourage wakati
Ye akishuka kwenye kochi anakaa
Kwenye jamvi na baadaye anelekea
saloon kupiga umbea kuhusu mama
joyce kafumaniwa gesti.
11.Nyumbani housegirl hapumziki.
12.Anajali ajira yake hataki
kufuatiliwa mambo yake.
13..Anakera sana, cwezi kuacha kazi
yangu hata km anaumwa, kajikata
kucha halafu anadai apelekwe Agha
Khan au India.
NOTE: akikutana na mwanaume
kichwa ngumu anamrudisha kwao
ameshazalishwa watoto 3, anaenda
kwa mwingine anaongezewa watoto
2, anazinguliwa anapigwa toto lingine
mmoja mtaani, unakuta kazaa na kila
familia mtaani baadaye anaishi ghetto
au kwao.
MWANAMKE MWEREVU.
1.Unaamka yeye kashaamka na
kusema "baby amka maji ya kuoga
yapo bafuni" (mwanamke adimu sana)
2.Unajiandaa kwenda kazini khaa, nguo
zishapigwa pasi (jamani hiyo kazi
kafanya saa ngapi? unajikuta unaenda
kazini upo kwny daladala kimoyo
moyo unamwambia "I love u honey"
3.Unarudi jioni unakuta anakuvua
soksi acha 2 hujui hata anazifua saa
ngapi maana huwa hujui anazifua saa
ngapi?
4.Umejipumzisha kwny kochi au kitandani mara kakukalia
Mgongoni anakufanyia masej
Mgongoni, khaa alijuaje unataka
Ufanyiwe masej? Unaishia kusema
Thanks baby.
5.Kila anachotaka kufanya
kujiendeleza anakuambia na unaweza
kumpa mtaji mana ni mkweli (ni
baraka kwny familia)
6.Anapenda ndugu zako (cyo mama
mkwe akija anasimamisha pua juu
km kitimoto)
7.Anakupa moyo kwny wakati
mgumu, mf: umefukuzwa kazi
anakushauri (baby hayo ni maisha
tu, ucjal utafanikiwa km vp 2cmamie ule mradi wangu mpk
uajiriwe) khaa jamani yupo km huyu
fb? Upareni? Uchagani? Usukumani je?
8.Ukirudi nyumbani unakuta
anamfundisha mtoto wako maadili ya
kimungu (wow heri 2zae 2 wa pili)
9.Anakufariji...Baby usiogope ni
mapito ya dunia, jikaze mume
wangu, nipo upande wako), heheeee
hata ukinuna unabembelezwa.
10.Mwenye kushukuru na
suprises, hawezi kukusahau, (baby hii
zawadi kwa ajili yako,umenisaidia sana
mume wangu, u change my
life, "baby leo birthday yako, khaa
unaona keki mezani"),kuna mke km
huyo?
11.Ana uhakika mimba yako ("baby
nina suprise, kumbe mwezi uliopita
ulinipa toto, nina mimba yako (cyo ooh
khaaa 2mefanya mapenzi juzi 2
umenipa dragon mwingine)
NB. Mwanamke km huyu ni
blessing, kila jioni unaona toto zako
zimekaa kwenye kochi yaani vitoto
vizuri miguu mifupi hata vikikaa
kwenye kochi miguu hazifiki kwny
sakafu vinaangalia cartoons.
Hehehe ni mtazamo tu...

Monday, March 7, 2016

Sunday, March 6, 2016

Hii ni mojawepo wa daraja la kipekee duniani lililoko nchini Ujerumani.


Daraja hili kwa jina Magdeburg Water Bridge ni la mashua na boti, chini kuna mto na pia juu ni mto mwingine!












MLINDE MPENZI WAKO DHIDI YA MAGONJWA..



Mahusiano Mengi yamekua yakiingia Dosari kwa kudumu kwa kipindi kifupi na kisha kuvunjika huku kesi kubwa ikiwa ni usaliti. Wakinadada wengi wanalia kusalitiwa na wapenzi wao kwa kuingia katika Sex case na Rafiki zao au hata jirani bila kujua Tatizo linaanzia kwao.

Wanawake wanapenda sana Mahusiano yasiyo na Sex (Ngono) na unapoanza mahusiano tu na Msichana basi huweza kukwambia nimekubali kuwa na wewe ila No sex. Sababu ya Upendo Mwanaume anaridhika lakini anatafuta njia ya kumaliza hisia zake bila kukuumiza na ili asikuumize nasi ni kuhakikisha hugundui kama amekusaliti. Na inapofikia umegundua ndipo Penzi huzikwa na Lawama kubaki kuwa wanaume ni wabaya.

Ila Tambua Sex (Kujamiiana) ni sehemu muhimu katika Mahusiano na pia kwa afya yako na ya Mpenzi sako.

Kujamiana (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule. Lakini, kuna faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa zinazotokana na 
kujamiana. 

Kutokana na matokea ambayo  yamewahi kuonekana katika tafiti kadhaa zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani imebainisha kuwa kufanya ngono..

1. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo: Wanawake ambao
hufika kilele (orgasm) angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack) na kiharusi. Uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo wakati wa kufanya mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1 tu ya vifo vyote vinavyotokana na mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na kujamiana. Aidha, sababu nyingine inayoongeza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa ambapo huchangia karibu asilimia 75 ya vifo vinavyotokana na kujamiana, na karibu asilimia 90 ya vifo hivi hutokea kwa wanaume wazee. Uwezekano wa kupata shambulio la moyo wakati wa kujamiana huongezeka ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50, uzito uliopitiliza na matatizo ya afya. Hii ni sawana kusema unaanza kufanya mazoezi mazito kwa ghafla wakati mwili na umri haviruhusu.

2. Huongeza ukakamavu wa mifupa: Wanawake waliokoma kupata hedhi (menopausal women) ambao pia hujamiana angalau mara mbili kwa wiki wana kiwango kikubwa cha homoni ya oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao hawajamiani. Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis. 

3.Hupunguza msongo wa mawazo: Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya mwili kupumzika, muscle relaxant), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiana. Watu wanaojamiana huweza kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo. Aidha watu wanaojamiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu kuliko wale wasiojamiana. Pia kuwepo kwa viasili vyaprostaglandins katika shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi hunyonywa na sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya zinc, calcium, potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu kwa afya njema.
4. Hupunguza maumivu: Kufikia kilele (orgasm) wakati wa kujamiana ni tiba ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa kujamiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi (post menopausal syndrome symptom).

5. Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume: Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wakujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi.

6. Huongeza uwezo wa kunusa: Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni ya prolactin huongezeka, ambayo hufanya seli za ubongo (brain stem cells) kutengeneza seli mpya katika sehemu inayohusika kunusa na kutambua harufu (brain olfactory bulb).

7. Hupunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema: Kujamiana ni mazoezi mazuri. Wakati wa kujamiana, mapigo ya moyo huongezeka kutoka wastani 70/dakika mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na mtu anayefanya mazoezi kwa kiwango cha juu. Kujamiana huchoma karibu 200 calories sawa na kukimbia dakika 15 katika mashine ya tredmill. Mwanamke anayefika kilele huchoma calories 47 zaidi.

8. Huongeza kinga ya mwili: Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa wiki huongeza kiwango cha seli za kinga aina ya immunoglobulin A kwa robo tatu, na hivyo kumkinga mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.

9. Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke: Wanawake wanaojamiana angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na ukweli kuwa kujamiana huongeza homoni ya oestrogen ambayo hufanya nywele za wanawake kuwa na afya nzuri na ngozi zao kung’aa. 

10. Hudhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida: Wanawake ambao hujamiana angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao hawafanyi kabisa.
11. Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini: Ikiwa litafanyika baina ya wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiana huongeza kujiamini.

12. Huongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga (pelvic floor muscles): na hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara kwa mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke (vagina atrophy) na hivyo kumwepusha na maambukizi katika njia cha mkojo (Urinary Tract Infection ).
13. Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini: Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini.

14. Huongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako: Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na ya kuvutia, haya yote hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiana na mwenza wake kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na ya kuvutia, hii huongeza hali ya kujithamini na kujipenda kwa binadamu yoyote.

15. Husaidia kuishi kwa muda mrefu: Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa wiki hurefusha maisha yako. Kila unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA (Dihydroepiandrosterone) hutolewa kwa wingi kutokana na raha ya tendo na kufikia kilele. DHEA huongeza kinga ya mwili, hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda), huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo, huiweka ngozi kuwa na afya bora na hupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo, kuongeza kufikia kilele kuna uwezekano wa kurefusha maishA yako

16. Kujamiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi, kutokana na kuongezeka kwa homoni ya oxytocin (love hormone), ambayo huleta mshikamano, uaminifu, na unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.

17. Huongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba: Mara nyingi watu huuliza kama urefu wa uume una uhusiano wowote na uwezo wa kutunga mimba. Jibu zuri ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanamume, huzifanya kuwa katika kiwango kizuri, na kama unataka kupata mtoto, ni bora kufanya mapenzi mara kwa mara sio kutumia shahawa zilizokaa kwa muda wa siku 4.


HONEYMOON



Mke wangu Harusi sasa imeisha, kila mtu amesharudi kwao. Hakuna muziki tena, hakuna kwaito tena. Harusi yetu ilikuwa nzuri. Nilijitahidi kuandaa harusi ya ndoto yako. Najua ulikuwa ukiangalia sana kipindi cha chereko TBC 1. Ukatamani tuwe na harusi nzuri kuzidi zile zilizokuwa zikioneshwa. Nimejitahidi katika hilo. 

Nilichoshindwa ni kuirusha tu live. Sasa ni historia. Harusi tumemaliza ni muda wa kujenga ndoa yetu.

 Kilichobaki ni sisi wawili tu. Kila kitu kinachotarajiwa na sisi kinaanza usiku huu.

Maisha yetu hayapo kawaida sasa, kuna siku fulani ulikuwa umevaa gauni lako jekundu. Ulionekana mrembo sana siku ile. Ni siku ile ambayo nilikuona nikavutiwa nawe Maradufu. Nilipokuona tu nilitamani nikukiss, nlitamanai nikushike kwa jinsi ulivokua ukinivutia. 

Sasa nipo nawewe maisha yangu yote, naweza nikakushika muda wowote ninaohitaji pamoja na kukikiss muda wowote ule.

 Ngoja nikuambie vitu vichache. Sina kitu cha kukuficha kuanzia sasa. Simu yangu unaweza ukaitumia kama yako, unaweza ukaingia fb yangu kama kwako, twitter, Whatsapp, Instagram na kwingineko ila simu isiwe kipimo cha Mapenzi yetu. Simu imetengenezwa na Mtu ila Mapenzi yetu yameumbwa na Mungu.

Mke wangu Kuanzia leo mimi nimekuwa mtoto wako, kwa wiki moja iliyopita nilikuwa mvulana. Nilikuwa nikiamka mwenyewe asubuhi, muda mwingine nililala na njaa. Hizi zote zilikuwa changamoto za maisha. Nilirudi gheto kwangu muda wowote niliojisikia. Na sikuwa na mshauri wa karibu mtu wa ku share nae siri zangu. Lakini vyote vimeisha kuanzia sasa.

Nisikie mke wangu Kuanzia leo wewe ni mama yangu, utakayeniuliza kama nitachelewa kurudi nyumbani bila sababu ya msingi, mama yangu utakae niamsha asubuhi saa kumi na mbili niwahi kazini, mama yangu utakae hakikisha silali na njaa. Ninajivunia kuwa na mama mwingine hivi sasa.

Ni matumaini yangu kuwa utakuwa mama mzuri kwangu. Usiwe na hasira sana na mimi nakuahidi ntakuwa mwema kwako. Usinichunguze sana maana huko mbeleni utaanza kujenga taswira ambazo hazipo zikaja kuleta ugomvi kati yetu. Najua muda mwingine nitakusababishia maumivu ya kichwa ila nakuahidi nitakuwa mfumbuzi wa hayo maumivu ya kichwa pia.

Mke wangu sikiliza Baba yangu Alipofariki, mimi ndio nilikuwa mwangalizi wwadogo zangu. kama baba kwao. Hivyo sioni kama kutakuwa na tabu yoyote mimi kuwa baba yako.

Tujenge taasisi yetu sasa...,


BINTI YANGU..,



Sasa nikijitazama Nimekua Mzee, Nikikutazma Usoni namkumbuka Mama yako, Nalikumbuka Tabasamu lake na ile sauti yake ya kubembeleza. Nafurahi kukuona sasa Umekua na unanipa Heshima yangu nikiwa Baba Mwema kwako.

My daughter, Kumbuka  kuanzia kesho hutakuwa ukiitwa tena jina langu. Utakuwa na furaha kuolewa na mwanaume uliyempenda. Please  Usini miss mimi kwasababu nimeshatimiza majukumu yangu. Sasa ni wakati wa kutimiza majukumu yako.

Kuanzia utoto wako, nimekulea vema kwa neema za Mungu. Ila kabla hujasema mbele ya Shekh kuwa unakubali kuolewa ningependa nikueleze kuhusu kuishi na mwanaume na maisha ya ndoa kiujumla.

Unakumbuka ulivyokua umekaribia kufanya mtihani wako wa mwisho wa kidato cha sita?

 Unakumbuka Ulikuja kwangu na nikakupa laki moja kwa ajili ya maandalizi ya mtihani?  Nakumbuka ulifurahi sana na ukaibusu Mikono yangu huku ukionesha Tabasamu la Dhati juu yangu, Sawa ingawa nilikupa mimi, lakini ukweli ni kwamba pesa ile ilikuwa sio yangu.

Najua siku zote ulikua ukijua kuwa mimi ndiye niliyekuwa nikikulipia ada. Ukweli ni kwamba mimi nilikua katika wakati mgumu, Sikua na kzi sikua na mbele wala nyuma...

Lakini mama yako alinipa pesa zake. Angeweza kukupa wewe moja kwa moja ila aliamua kunipa mimi kwanza ili nikupe, Alihitaji kuilinda Heshima yangu kama Mume kwake na Baba kwako.

Hii inamaanisha nini mwanangu, msupport mume wako! Muda mwingine atakutana na changamoto katika maisha na kukutana na ugumu wa maisha, madeni na vinginevyo ingawa ataonekana yuko sawa ila akilini mwake anayo hofu na majonzi makuu...Atahisi hutaweza kumthamini tena kwa vile mambo yamemuendea kombo. Huo ndio muda ambao itakubidi kuwa nae bega kwa bega ukimfariji na kumfanya kuwa na furaha wakati wote.

Mwanangu njia sahihi ya kumuonesha mume wako kua unampenda ni kumuheshimu, najua inaweza tokea ukabishana nae, ukakwaruzana nae ila mwisho wa siku mwache ajue kuwa heshima yako kwake iko pale pale.

Mwanangu unakumbuka siku ile nilipomkaripia vibaya sana mama yako? Alifanya nini? Alibaki kimya kabisa. Unakumbuka pia siku ile mama yako alivyonijia juu? Nilifanya nini? Nilibaki kimya kabisa!

Binti yangu jifunze kuwa Kimya muda mwingine pale mume wako atakapokuwa na hasira. Mmoja kati yenu atakapokuwa na hasira na gadhabu  mmoja lazima atulie kimya. Kama wote mtaanza kupandishiana hasira tatizo hapo ndio huibuka. Na matatizo ya ndoa ndio huanzia hapo.

Mwanangu kitu cha kwanza kujua kuhusu mume wako ni chakula anachokipenda. Kama anapenda vyakula vya aina nyingi weka katika akili yako. Usiache mpaka aombe chakula siku zote muandalie wewe, Usimpe nafasi ya kutafuta chakula akipendacho kwa jirani.

Binti yangu kuna siku mama yako alinikuta nikiwa nimemshika mwanamke mwingine mkono, hakuwa mchepuko wangu ila ni rafiki yangu nikiyepotezana nae kitambo. Mama yako aliponiona hakuanzisha ugomvi na yule mwanamke. Aliondoka kimya kimya.

Nilikuwa na hofu  kurudi nyumbani, ningemwambia nini anielewe? Lakini niliporudi nyumbani hakunisema chochote. Aliniandalia chakula mezani kama kawaida. Ila nafsini nilijiona kama nina hatia. Nikaanza kumuomba msamaha. 

Kuanzia siku ile sikukaa kumtazama mwanamke wa pembeni mara mbili. Nani anajua? Je kama mama yako angegombana na mimi siku ile, labda ningeondoka nyumbani nakuangukia katika mikono ya mwanamke yeyote tu barabarani akanipoze. 

Muda mwingine ukimya huleta ufumbuzi mkubwa kuliko ugomvi.

Mwanangu Sahau kuhusu riwaya za mapenzi ulizosoma ulipokuwa shuleni. Unakumbuka filamu za kihindi na za kimarekani? Unakumbuka filamu za kitanzania na Kinaijeria? Unakumbuka tamthiliya za kifilipino? Nyimbo za westlife na Diamond,  unazikumbuka?  Maisha ya kina Wema na Zari? Sahau kabisa hayo mambo mwanangu! Usitegemee vitu ulivyokua ukiviona huko vitakuwepo katika ndoa yako. Maisha halisi ni tofauti na hadithi za kufikirika.

Kitu cha mwisho nachotaka nikuambie... Unakumbuka jinsi ulivyozaliwa? Sijawahi kukwambia!

Nilipanga kuja kukwambia siku utakapokua tayari kuishi ndani ya uhalisia.

 Baada ya ndoa yetu mimi na mama yako mambo yalikuwa magumu. Na mama yako ilimlazimu afanye kazi mbili kusupport familia. Nami pia nilikuwa nikifanya hivyo. 

Nilikuwa nikirudi nyumbani saa moja jioni na mama yako alikuwa akirudi saa mbili usiku akiwa amechoka. Lakini tulipoenda kulala hakuninyima chakula cha usiku kitandani. Na kwa jinsi hii ndipo ulipozaliwa. Usijenge tabia ya kumyima mumeo chakula chake akipendacho cha usiku. Maana kufanya hivyo sio kumkomoa bali ni kuiharibu ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe. 

Kuwa mke mwema, na utakuwa binti yangu nitakae jivunia mpaka naingia kaburini....., Naamini Mama yako atakua anatabasamu huko Mbinguni kwa kuwa umemlindia Heshima yake hapa Duniani.

#Nakutakia Maisha Marefu ya Ndoa Binti yangu...,

MWANAMKE wa daraja la Pili

Kipindi utakapokubali kutoka kimapenzi na mme wa mtu, utakuwa umekubaliana kuwa mwanamke wa daraja la pili. Na siku zote mtu wa daraja la pili ni mtu wa daraja la chini ukilinganisha na daraja la kwanza.

Angalia sasa...kama yupo na wewe na mke wake akapiga simu atamdanganya mkewe kwamba yupo ofisini au katika kikao na hautakuwa na ujasiri wa kuingilia mawasiliano yake. Pia anapokua nyumbani kwake kwa mkewe huwezi kumpigia au hata kumtumia text.

Dada yangu wewe ni mdoli? Anakuchukua kwenu na gari yake anakupeleka katika vyumba vya hotel lakini mke wake amemkabidhi nyumba nzima. Dada yangu shtuka!! Anakutembelea nyumbani kwako na unamtambulisha kwa rafiki zako na majirani kwamba ni boyfriend wako bila kujua unajizibia nafasi za kupata mtu sahihi wa kuweza kujenga nae maisha. Na mbaya zaidi hupajui hata yeye anapoishi.

Dada yangu mpaka lini utaendelea kujiharibia future yako? Anatoka na wewe out na anakununulia kila aina ya pombe na wakati huo huo hawezi kumruhusu mkewe kunywa pombe ya aina yoyote ile. Akili ya kawaida ikwambie kwamba anafanya hivyo ili ulewe vilivyo na apate wasaa wa kukukandamiza vizuri kitandani.

Dada yangu Je mwili wako ni wa majaribio? Anakupa mimba na anakupa pesa uende ukaitoe lakini mke wake akipata mimba nyumbani ni sherehe na anampa pesa za kuandaa martenity dress na vitu vya mtoto.

Dada yangu kumbuka tayari anayo familia yake, kama ulikua hujui Jamaa huwaelezea marafiki zake yote mnayofanya hotelini, lakini hata siku moja hawezi kuwalezea yale anayofanya na mkewe. Hii inafanya marafiki zake wakuone kama mwanamke wa hadhi ya chini kabisa.

Unazo picha zake katika simu yako na ume save namba yake kwa majina mazuri kama Sweetheart, My love, etc... Lakini picha zako haziwezi kupatikana ktk simu yake na namba yako amei Save kama Fundi Genereta, Fundi gari, Mzibua Chemba.

Unatakiwa ukumbuke kwamba mwanamke asie na akili sehemu zake za siri ndizo zitakazoumia zaidi.


JIFUNZE EWE MWANAMKE



1. Usikimbilie kuhama na kuondoka nyumbani kwa wazazi wako kabla hujajipanga vizuri.

2. Usimsubiri mwanaume ndio uanze maisha, unaweza ukaishi maisha yako mwenyewe na ukaweka msingi mzuri utakaokusaidia huko baadae.

3. Kaa mbali na marafiki waovu, jifunze kuheshimu kila mtu kuwa na busara na vaa mavazi ya heshima.

4. Usimchekee chekee kila mwanaume, kwa maana wengine sio waoaji ni chui waliojivika ngozi ya kondoo! Ni bora ukaendelea kuabki single kuliko uje kuolewa na mtu ambaye atakufanya ujute maisha yako yote hapa duniani. Omba Mungu akupe busara na ustahimilivu.

5. Jijengee tabia ya kula kwa afya, siku zote jitahidi ule milo yote mitatu acha kula biscuit na soda, usipendelee chips na mishkaki na vyakula vya aina hiyo. Fanya mazoezi mepesi kuuweka mwili wako uendelee kuwa mzuri wa kuvutia. Wewe ni tunu kwa mume wako mtarajiwa au uliyenae.

6. Vaa kwa heshima, watu watakujaji kulingana na jinsi tu ulovyovaa hata maongezi yao yataegemea kutokana na uvaaji wako.

7. Usitumie SEX kama njia ya kujihakikishia Mapenzi. Kufanya mapenzi sio tiketi ya kupendwa. Ata SEX na wewe na atakuacha kwenye mataa ya ubungo junction.

8. Usiolewe nae kwa vile ana pesa za kutosha na ni tajiri kwa sababu karibuni tu na wewe utakua moja ya mali anazomiliki.

8. Jiongezee thamani, get a career! Usiwe mpumbavu kufikiri mwanaume ndio atasuluhisha matatizo yako yote. Jibidiishe kwa kazi zako binafsi hakuna raha juu ya kuwa na maamuzi ya kutumia kile kipato ulichokipata kwa jasho lako.

10. Wewe ni wa muhimu mno, una thamani kubwa sana! Jipende jiheshimu, jijali. Usijali umetendwa na wangapi katika mahusiano! Usikate tamaa jiweke vizuri. Ishi maisha yako. Hayo unayopitia ni funzo tu ktk maisha.

Above all, Remember this, Charm is deceitful, and beauty is vain: but a woman that fears the LORD, she shall be respected.

MUNGU AWABARIKI WANAWAKE WOTE ULIMWENGUNI, ABARIKI KAZI ZA MIKONO YENU NA SIO KAZI ZA MAUNGO YENU. NINYI NI WA THAMANI MNO.


Hizi Hapa Sababu Zitakazokufanya Wewe Binti Usiolewe Mapema



★1. Kuvaa nguo za ajabu ajabu kama changudoa. Sijui ni nani aliyewaambia kuwa mkivaa hivyo mnapendeza!

★2. Kujipaka marangi ya ajabu ajabu usoni kama mwali wa kimakonde au kizaramo kwanza mnatutisha tu.

★3. Kupenda kujirahisisha au kujipendekeza pendekeza kwa wanaume, yani ukiguswa kidogo tu twende.

★4. Kuwa na picha karibia 500 Facebook, Twitter nk halafu picha zenyewe hazieleweki yani zimepigwa katika mavazi au mapozi ya ajabu ajabu, mara umebinua makalio, mara tumbo, mara mdomo, Haaaaa!

★5. Kila unachofanya basi unakimbilia kupost mfano kwenye Facebook account
yako au Instagram na nyinginezo hata ukienda haja basi lazima upost.

★6. Ni mtu wa maneno maneno yani we kila unachokiona unaongea na kuropoka ropoka tu hauna break! mwanamke gani?

★7. Huna mawazo ya malengo endelevu yani we kwenye bichwa lako kumejaa umbea tu sijui leo Wema Sepetu amefanya nini? Sijui Kim, Lupita amefanya vile na upuuzi mwingine.

★8. Mizinga. Yani siku ya pili tu baada ya kukutongoza unaanza " honey nataka galaxy" Htc" Huawei" mara baby nimeona nguo nzuri mara ooh baby yaani njaa inauma'' kwani huyo mwanaume ni babaako, utasindikiza harusi za wenzio hadi upigwe alama..


Friday, March 4, 2016

Airbus 380, Emirates imekamilisha safari ndefu zaidi

Ndege ya shirika la Emirates imekamilsha safari ya moja kwa moja ndefu zaidi duniani kutoka Dubai hadi New Zealand.

Ndege hiyo aina ya Airbus 380, ambayo ndiyo kubwa zaidi ya abiria duniani imesafiri angani kwa kilomita 14,200 bila kusimama, safari iliyochukua masaa 17 na dakika 15.






Tuesday, March 1, 2016

Rais Magufuli na Rais Museveni wamekubaliana Ikulu ndogo leo jijini Arusha

President wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amekutana na kufanya Mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Tanga Tanzania hadi nchini Uganda.

Rais Museveni amemtembelea Rais Magufuli katika Ikulu ndogo ya Arusha leo jioni mara baada ya kuwasili hapa nchini akitokea nchini Uganda, ambapo hapo kesho atahudhuria mkutano mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Museveni

Baada ya wawili hawa kufanya mazungumzo ya faragha, Rais Magufuli amesema wamekubaliana kutekeleza mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanga hadi Uganda kwa manufaa ya nchi zote mbili na nchi nyingine za Afrika Mashariki, litakuwa na urefu wa kilometa 1,120 na kwamba mradi huo utazalisha ajira za watu zaidi ya 15,000.

Rais Magufuli ameongeza kuwa pamoja na kujengwa kwa bomba la mafuta, pia wamezungumzia kuongeza biashara ndani ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, kujenga viwanda na kuzalisha ajira zaidi kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji mali.

magufuli 2

Ikulu ndogo Arusha.

Rais Magufuli amesema katika mkutano huu nchi wanachama watajadili maombi ya nchi ya Sudan Kusini kupata uanachama ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa Sudan Kusini kuwa mwanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa na uwezo wa kufanya biashara katika eneo lenye takribani watu milioni 150.

Kwa upande wake Rais Yoweri Museveni pamoja na kuunga mkono yaliyosemwa na Rais Magufuli amempongeza kwa kasi yake nzuri aliyoanza nayo katika uongozi na amesema ni matumaini yake kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sasa zitakuwa katika nafasi nzuri ya kwenda kwa kasi ya Rais Magufuli katika maendeleo.

Addis Ababa light railway under construction in Addis Ababa


New