Gari linalokokotwa na ng'ombe katika barabara ya kuelekea kijijini
Gamboshi.
USIKU YAONEKANA KAMA JIJI LA NEW YORK AU LONDON. WENYEWE WAMWOMBA RAIS KIKWETE, MZEE WA VIJISENTI AKAWASAFISHE
WAKAZI wa Kijiji cha Gamboshi, kilichopo wilayani Bariadi, Mkoa wa Shinyanga, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete awasaidie kusafisha kijiji chao kutokana na jina baya lililoenezwa duniani kwamba hapo ni makao makuu ya maovu ya uchawi ulioshindikana.
Kijiji hicho ambacho ni nadra sana kutembelewa, kimepata umaaurufu mkubwa ndani na nje ya nchi kikielezwa kuwa ni kitovu cha uchawi na wachawi wanaoweza kufanya miujuza, hali ambayo imekifanya kijiji hicho kupitwa na mkondo wa kimaendeleo.
“Sisi ni wakulima wakarimu wa pamba, mahindi na 
mpunga. Yote mnayoyasikia kwamba sisi ni magwiji wa uchawi ni uvumi 
uliotiwa chumvi nyingi. Tunamwomba Rais wetu kwa kushirikiana na Mbunge 
wetu, Andrew Chenge watusadie kulisafisha jina letu,”alisihi  Zephania 
Maduhu, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Gamboshi.
Maduhu pamoja na wanakijiji wenzake walidai kuwa, 
hofu iliyoenezwa ndani na nje ya nchi kuhusua uchawi uliovuka mipaka wa 
Kijiji cha Gamboshi umesababisha madhara makubwa kwa kijiji chao kiasi 
chakutengwa na jamii yote ya Watanzania.
“Hakuna aliyetembelea kijiji hiki kwa miaka mingi 
sana. Hata sisi tunapotoka nje ya kijiji, wengi hawataki kutusogelea 
wakiamini tutawadhuru, ”  alisema Musa Deus (26), mmoja wa wakulima 
walionufaika kilimo cha mkataba kijijini Gamboshi.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, tangu Uhuru mwaka 1961, hakuna kiongozi yoyote wakitaifa aliyewahi kukanyaga kijijini hapo.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, tangu Uhuru mwaka 1961, hakuna kiongozi yoyote wakitaifa aliyewahi kukanyaga kijijini hapo.
Anaongeza kuwa mtu wa pekee aliyewahi kuzuru 
kijijini hapo ni mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge, aliyefika 
kijijini hapo mwaka 2010, wakati akifanya kampeni za ubunge.
“Tume ya Katiba ilitupita, mwenge wa Uhuru nao haujawahi kupita hapa.Tuko kisiwani mbali na Watanzania wengine,” anasema Maduhu.
Kikiwa mafichoni kabisa, kiasi cha kilometa 44 
kutoka mjini Bariadi, Kijiji cha Gamboshi si rafiki wa watu wa Kanda ya 
Ziwa kama ambavyo Mwananchi Jumapili ilibaini katika utafiti wake wa 
muda mrefu.
Mijini na vijijini, kumekwepo na ubishani mkali 
kuhusu ni mkoa gani unaokimiliki kijiji hicho, ambacho baadhi ya wakazi 
wake wanadai kuwa miongoni mwa vioja vyake ni mauzauza yanayoweza 
kuifanya Gamboshi ionekane kama Jiji la New York, Marekani au London, 
Uingereza wakati wa usiku.
Pamoja na umaarufu wake, bado uwepo wa Gamboshi 
umekuwa ni kitendawili kikubwa kwa jamii ya Wasukuma kutoka mikoa ya 
Mwanza, Shinyanga na Simiyu.
Mbali na ubishani mkali kuhusu kuhusu mahali hasa 
kilipo kijiji hicho cha miujiza, wengi wamekuwa wakidai wakazi wake siyo
 jamii ya Kisukuma.
Wakazi wa Shinyanga wanadai kuwa Gamboshi iko 
wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza, wakati wale Mwanza wakidai kuwa iko 
mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa Maduhu, Gamboshi iko katika Wilaya Bariadi, karibu na mpaka unaotenganisha na Wilaya ya Magu iliyoko mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa Maduhu, Gamboshi iko katika Wilaya Bariadi, karibu na mpaka unaotenganisha na Wilaya ya Magu iliyoko mkoani Mwanza.
“Tunaomba sana ndugu mwandishi, waambie Watanzania
 kuwa mengi wanayoyasikia kuhusu Gamboshi siyo kweli kabisa. 
Tunawakaribisha wote waje hapa kufanya biashara na sisi, waoleane na 
vijana wa Gamboshi kama wafanyavyo katika vijiji vingine. Sisi ni 
binadamu wema,” anasema mkazi wa kijiji hicho, Malimi Kidimi ambaye ni 
mkulima.
Ofisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Pamba(TCB), Ramadhani Dissa, anaielezea Gamboshi kuwa ni moja ya vijiji vilivyouza pamba nyingi msimu huu.
Ofisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Pamba(TCB), Ramadhani Dissa, anaielezea Gamboshi kuwa ni moja ya vijiji vilivyouza pamba nyingi msimu huu.
No comments:
Post a Comment