Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Mrisho 
Kikwete (wa pili kushoto) Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein 
(kushoto), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange,Makamu 
wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal, Wakiwa makini wakati wimbo wa Taifa 
ulipokuwa ukiimbwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika 
maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru jana.Picha na Salhim Shao
“Utaratibu uliopo ni kuzungumza kila baada ya miaka mitano, lakini mwaka huu ninazungumza na wananchi kutokana na kuwapo kwa viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc). Nataka wasikie mafanikio yetu ya miaka 51 ya Uhuru,” alisema Rais Kikwete.
RAIS Jakaya Kikwete amesema wenye hila na chuki pekee ndiyo wanaosema kuwa Tanzania hakuna maendeleo.
“Utaratibu uliopo ni kuzungumza kila baada ya miaka mitano, lakini mwaka huu ninazungumza na wananchi kutokana na kuwapo kwa viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc). Nataka wasikie mafanikio yetu ya miaka 51 ya Uhuru,” alisema Rais Kikwete.
RAIS Jakaya Kikwete amesema wenye hila na chuki pekee ndiyo wanaosema kuwa Tanzania hakuna maendeleo.
Alisema hayo jana alipolihutubia Taifa kwenye 
maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye Uwanja
 wa Uhuru, Dar es Salaam.
“Utaratibu uliopo ni kuzungumza kila baada ya 
miaka mitano, lakini mwaka huu ninazungumza na wananchi kutokana na 
kuwapo kwa viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
 (Sadc). Nataka wasikie mafanikio yetu ya miaka 51 ya Uhuru,” alisema 
Rais Kikwete.
Viongozi walioshiriki maadhimisho hayo ni marais 
Armando Guebuza wa Msumbiji, Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya 
Kongo (DRC) na Hifikepunye Pohamba wa Namibia.
Nchi zilizotuma wawakilishi katika sherehe hizo 
zilizohudhuriwa na umati wa watu ni Lesotho, Zambia, Angola, Swaziland, 
Shelisheli, Rwanda, Zimbabwe, Mauritius na Malawi.
Rais Kikwete alisema mwenye macho hawezi kusema 
lolote, lakini kwa mwenye hila hakosi maneno na kutoa dosari kwa 
maendeleo yaliyofikiwa.
“Watu waliobahatika kuiona Tanzania ya mwaka 1961 
wakija sasa hivi, wataona mabadiliko makubwa. Kuna mabadiliko makubwa na
 hii inatokana na kuboresha nyanja mbalimbali za kiuchumi, ulinzi na 
usalama na miundombinu... kwa wenye hila hawakosi la kusema ila mwenye 
macho haambiwi tazama,” alisema.
Aliwashukuru viongozi walioshiriki mkutano SADC… 
“Tumepata bahati ya uwepo wa viongozi waandamizi wa SADC baada ya 
kukubali ombi langu la kuhudhuria sherehe hizi japo wengine wametoa 
udhuru na kutuma wawakilishi,” alisema.
Viongozi mashuhuri wakosekana
Baadhi ya viongozi wa kitaifa wakiwamo wastaafu, hawakuwamo katika sherehe hizo.
Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na mtangulizi wa Kikwete, Benjamin Mkapa ambaye yuko Lushoto mkoani Tanga.
Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, 
Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Idd 
ambao hata hivyo, haikuelezwa sababu za kukosekana kwa
No comments:
Post a Comment