Walimu hao ni wale ambao shule zao wanafunzi wake walibainika majibu yao kufanana katika mitihani ya darasa la saba iliyofanyika mwaka jana hivyo kusababisha kufutiwa matokeo ambao wanafunzi husika walipewa adhabu ya kurudia mitihani mwaka huu
RUNGU la Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo limewashukia wakuu saba wa shule za msingi wilayani hapa kwa kupewa adhabu za kuteremshwa vyeo baada ya shule zao kujihusisha na udanganyifu kwenye mitihani.
Walimu hao ni wale ambao shule zao wanafunzi wake walibainika majibu yao kufanana katika mitihani ya darasa la saba iliyofanyika mwaka jana hivyo kusababisha kufutiwa matokeo ambao wanafunzi husika walipewa adhabu ya kurudia mitihani mwaka huu.
Naibu Waziri Mulugo alitoa agizo la walimu hao
kuteremshwa vyeo kwa maofisa elimu wa halmashauri za wilaya na Mji wa
Korogwe juzi, alipokuwa wilayani humo kwa ajili ya shughuli za kikazi
ambapo alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa sekta ya elimu.
Walimu waliokumbwa na sakata hilo na shule
wanazotoka kwenye mabano kwa upande wa halmashauri ya wilaya ni Karimu
Awadhi (Hale), Eliakim Mbise (Kerenge), Ramadhani Kisairo (Rwengera
Estate), Dastan Daudi (Pambei) na Mohamed Kombo (Vuluni).
Wengine ni Elisante Elibariki wa Shule ya Msingi
Welei aliyehamishiwa Wilaya ya Kilindi ambaye hata hivyo imeelezwa
kwamba tayari anatumikia adhabu hiyo ya kuteremshwa daraja huko aliko na
Rashid Shekigenda wa Shule ya Msingi Antakaye Korogwe Mjini.
Katika mkutano na walimu wa eneo la Korogwe Mjini,
Mulugo alielezea masikitiko yake juu ya hali ya ufaulu wa wanafunzi
ambapo alisema ingawaje kimaandishi inaelezwa kuwa kiwango cha ufaulu
kimeongezeka lakini uhalisia hauelezi hivyo kwa mazingira yaliyopo.
Naibu Waziri Mulugo aliyasema hayo baada ya
kupokea taarifa toka kwa ofisa elimu wa halmashauri ya mji kuwa kiwango
cha ufaulu kimeongezeka kwa wanafunzi wa darasa la saba, hapo aliweza
kuzikumbuka baadhi ya shule zilizofutiwa matokeo kwa udanganyifu.
Baada ya naibu waziri huyo kuuliza swali hilo
Ofisa Elimu, Maajabu Nkanyemka alijibu kuwa bado na kuitaja shule
iliyofutiwa matokeo kuwa ni Antakaye ambapo mwalimu mkuu aliyekuwepo
mkutanoni aliitwa mbele na waziri akiulizwa maswali kadhaa na baadaye na
afisa elimu wa halmashauri hiyo ya mji alitakiwa kutekeleza agizo la
kumteremsha cheo.
Kuhusu majibu juu ya suala la upungufu wa vitabu
shuleni taarifa ambayo alisomewa, Mulugo aliwatoa hofu walimu kwamba
serikali imetenga fedha za kutosha kukabili tatizo hilo
No comments:
Post a Comment