Mawaziri sita wameapishwa nchini Misri katika mabadiliko ya mwanzo ya baraza la mawaziri tangu katiba mpya kukubaliwa.
Serikali sasa ina mawaziri wepya wa fedha na
mashauri ya ndani ya nchi, wakati serikali inajaribu kuimarisha uchumi
uliozorota na sarafu iliyoporomoka.Waziri mpya wa fedha, El-Morsy El-Sayed Hegazy, amekariri kuwa Misri inataka kukubaliana na IMF, ipewe mkopo wa dola bilioni nne na laki nane milioni, ambao ulicheleweshwa kwa sababu ya msuko-suko wa kisiasa nchini humo.
No comments:
Post a Comment