Wabunge wa muungano mkuu wa
wabunge wasioegemea upande wowote katika serikali ya mseto nchini Libya,
wamejiondoa na kutangaza kuwa hawatahudhuria vikao vya bunge
kulalamikia kucheleweshwa kwa shughuli ya kuandika katiba mpya, ili
kuongoza nchi hiyo, baada ya kuondolewa na kuuawa kwa kiongozi wa zamani
wa nchi hiyo Muamar Gadaffi.
Mbunge mmoja wa muungano wa Liberal National
Forces Alliance (NFA) Souad Sultan, kuwa bunge hilo
limeshindwa kuafikia matakwa na matarajio ya raia wa nchi hiyo.Bunge hilo ambalo lilichaguliwa mwezi Julai mwaka uliopita, miezi Tisa tangu kuuawa kwa Kanali Muammar Gaddafi.
Sultan amesema kuwa wabunge wameshindwa kukubaliana kuhusu jinsi katiba hiyo mpya inapaswa kuandikwa.
Lakini, makundi mengine yanataka bunge hilo lenye wanachama mia mbili kuchagua kamati hiyo.
Muungano wa NFA, ambo ndio mkubwa zaidi katika bunge la nchi hiyo, pia umesema ukosefu wa usalama na jinsi bunge hilo linavyoendesha ndio sababu kuu ya wao kujiondoa.
Wabunge wa muungano huo wamedhulumiwa mara kadhaa katika meizi ya hivi karibuni, baada ya waandamanaji kuvamia bunge hilo, na kutatiza vikao vyake.
Lakini mbunge mmoja wa chama cha Minority Front Party, MFP, Mohamed Addarat, amesema kujiondoa kwa wabunge wa NFA hakutakua na athari yoyote, katika shughuli za bunge hilo.
Amesema bunge hilo litaendelea na vikao vyake bila tatizo lolote.
Ibrahim al-Gheriani, ambaye ni kiongozi wa muungano huo wa NFA, amesema wamegadhabishwa na utendaji kazi wa bunge hilo.
Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari, wabunge wa muungano huo wanatarajiwa kurejea tena bungeni baadaye wiki hii.
Libya imekubwa na msukosuko wa kisiasa tangu kuondolewa madarakani na kuuawa kwa Kanali Muammar Gaddafi Oktoba mwaka wa 2011.
Serikali ya nchi hiyo imekuwa ikijaribu kuwapokonya silaha makundi ya wapiganaji ambayo yamekuwa yakijaribu kupambana na wanajeshi wa serikali ya sasa.
No comments:
Post a Comment