tutazungumzia jinsi ya kuwa na msingi imara kwa biashara yako
ili idumu kwa muda mrefu na ikuletee faida kwa sasa na siku zijazo!Jambo la kwanza kabla hujaanza ni kuangalia Uwiano wa Thamani wa Biashara yako (The Value Equation).Watu
wengi sana huanzisha biashara kabla ya kufanya uwiano mzuri wa thamani
kati ya mtaji utakaotumika na faida wanayotarajia kuipata. Kila mtu huwa
analifahamu hili akilini mwake kwa kiwango fulani, lakini ni watu
wachache ambao hujitaabisha vya kutosha kuangalia uwiano kati ya hizi
pande mbili. Mfano, mama anayetaka kuanza biashara ya maandazi kama
kitafunwa cha chai asubuhi, huanza kwanza kwa kukokotoa hesabu ya
gharama ya unga wa ngano, amira, sukari, mafuta, umeme au mkaa
utakaotumika kuivisha maandazi hayo n.k. Baada ya hapo, mama huyu
hukokotoa tena mahesabu ya idadi ya maandazi anayoweza kupika, bei
atakayouzia na faida atakayoipata kwa kila andazi. Kisha kutokana na
utafiti ambao mama huyu atakuwa ameufanya, maamuzi hufanyika, ama kuanza
biashara hii au la. Mara nyingi hivi ndivyo ilivyo hata kwa biashara
nyingine nyingi.
Watu huangalia japo juujuu gharama za uendeshaji na
hulinganisha na faida inayoweza kupatikana kisha huingia moja kwa moja
kwenye biashara.Tatizo kubwa ninaloliona kwa wajasiriamali wengi ni
kwamba huwa hawauchukulii uwiano huu kiumakini zaidi. Na hii hufanya
wengi kufunga au kushindwa biashara zao baada ya muda mfupi! Kwa kuwa
mara nyingi utakuta kuwa mategemeo yao ni tofauti sana na uhalisia
wenyewe.
Kwa mfano mtu anayeanzisha shule huwa anakuwa hajaangalia
ukweli kwamba kuna miezi ambayo shule zinafungwa lakini waalimu hawaendi
likizo, ikiwa ina maana kwamba japo wanafunzi watakuwa majumbani na
hawalipi ada, lakini walimu watatakiwa walipwe mishahara kama kawaida.
Hii huwasababisha wamiliki wa shule kuhamaki hususan mwaka wa kwanza wa
uendeshaji wa shule.Hivyo kuwa na uwiano mzuri wa thamani ni
kuyaangalia yote haya. Je, pesa itakuwa inaingia kila siku, kila mwezi
au kila baada ya miezi mitatu, sita, tisa au mwaka? Je, kiasi
kinachopatikana kitatosha kulipa mishahara na kulipia gharama za
uendeshaji?
Baada ya hapo, je, kutakuwa na akiba kwa ajili ya kukuza
mtaji na wewe mwenyewe mjasiriamali kulipwa? Mara nyingi ninashangazwa
na watu wanaokuja kuniomba ushauri wakiwa tayari na pesa mkononi jinsi
ambavyo wanakuwa hawajayaangalia mambo haya kwa kina. Jiulize maswali
magumu mengi kadiri uwezavyo kabla hujaamua kuanzisha biashara yako.
1.
Je, utanunua bidhaa yako au malighafi kwa kiasi gani? Ni wapi unaweza
kupata kiasi kingi au kikubwa kwa gharama ndogo kadiri uwezavyo?2. Gharama za usafiri ni kiasi gani (kama usafiri unahusika) na utapataje kwa bei ndogo kadiri iwezekanavyo?4.
Sehemu yako ya kuendeshea biashara itagharimu kiasi gani? Malipo
yatakuwaje? Utakodi? Utapewa bure kwa muda gani (kama inawezekana).
Itahitaji matengezo au ukarabati kiasi gani?
5. Utahitaji
wafanyakazi wangapi wa kuanza nao? Utawalipa kiasi gani? Au utaanza
mwenyewe na mkeo/mumeo/mwanao/nduguyo n.k? Watanufaika vipi na biashara
yako? Watafanya kazi kwa muda gani kila siku? Je, watahitaji pesa ya
chakula cha mchana au itajumlishwa kwenye mshahara?6. Utahitaji vitendea kazi vipi? Mashine (kama utahitaji)? Kompyuta je? Meza? Viti? Vitagharimu kiasi gani?7. Malipo ya kodi yatakuwa kiasi gani? Utalipa kodi za aina ngapi na kwenye mamlaka aina ngapi?8. Gharama za uendeshaji wa biashara yako kila siku ni kiasi gani? Kama vile umeme, usafiri, maji, usafi, simu n.k?
9. Gharama za uzalishaji/utengezaji au utoaji wa huduma wa siku itakuwa kiasi gani?10. Je, wewe mwenyewe utajilipa kiasi gani kwa wiki, mwezi n.k?
No comments:
Post a Comment