My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, October 24, 2013

Kukabwa na jinamizi ni nini?

Kuna watu wengi wamekuwa wakiniuliza swali hilo hapo juu na  kwamba kukabwa na jinamizi wakiwa wamelala usingizi kunasababishwa na nini? Pia wanataka niwaeleze jinsi ya kuepuka na hali hiyo.
Watu wengi hufikiri kwamba anayewakaba ni jini lakini tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama “Mwili kupooza katika usingizi” (Sleeping Paralysis) .
Tendo hilo huwa linawatokea watu katika muda wa sekunde 20 lakini wewe unayehusika utahisi kama dakika 5 au dakika 10.
Matukio hayo ya kijinamizi yanatofautiana na yanakutokea wakati ukiwa nusu usingizini na nusu macho.
Ukweli ni kwamba hayana madhara yoyote, ila yanakupa hofu kwa muda fulani. Unapokabwa na jinamizi unakuwa na fahamu nusu. Unaweza kufungua macho na utahisi kupiga kelele lakini watu hawakusikii, mwili wako unakuwa hauwezi kufanya lolote na viungo vya mwili wako vinakuwa havifanyi kazi.
Inapokutokea unakuwa huwezi kunyanyua mguu, mkono wala kichwa. Kwa ujumla unakuwa kama uliyepata “ugonjwa wa Kupooza”.
Hali hii ya kukabwa inapotokea unaweza ukamuona mtu anayetisha akiingia ndani chumbani kwako, wengine wanaona kama wanatekwa nyara au kuchukuliwa, wengine wanahisi wanabakwa, wengine wanaona wakipigwa au kukimbizwa na matukio mbalimbali ya kutisha.
Kukabwa na jinamizi kama tunavyoita kunatokana na sababu nyingi, ya kwanza kabisa ni jinsi wewe mwenyewe ulivyolala, mara nyingi unapolala chali mambo hayo yanakutokea, au ukiwa na jambo linalokusumbua kimaisha ambalo huwezi kulitatua linaweza kukuletea hali hiyo ya kukabwa.
Sababu nyingine ni mazingira unayoishi au  eneo ulilopo kama kuna makelele, au chumba kisicho na hewa ya kutosha au kuwa na mawazo kuhusu jambo fulani, au kulala na njaa au ukiwa umelala umekasirika au ndoto unazoota.

No comments:

Post a Comment

New