My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, October 24, 2013

NJIA YA KUEPUKA KUKABWA NA JINAMIZI

jinsi mtu anavyokabwa na jinamizi akiwa amelala usingizi, tukasema watu wengi hufikiri kwamba anayewakaba ni jini lakini tukabainisha kuwa tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama Mwili kupooza katika usingizi (Sleeping Paralysis).
Tulifafanua kuwa tendo hilo huwa linawatokea watu kwa  sekunde 20 lakini wahusika waliokabwa hudhani kuwa wamekuwa katika hali hiyo kwa  dakika 5 au dakika 10 kutokana na jinsi watakavyojisikia.
Ili kuepuka kukabwa na jinamizi unapaswa kufanya yafuatayo: Ikikutokea hali hiyo jaribu kuvuta pumzi nyingi ndani kwa sababu pumzi peke yake ndiyo unayoweza kuidhibiti ukiwa umekabwa.
Ukihisi unakabwa jaribu sana kujitingisha na ukifanya hivyo hali ya kukabwa itakwisha. Wengine wana bahati hali hiyo huwatokea kabla hawajapata usingizi mzito, hivyo ukiona kama unataka kukabwa amka kaa kwa dakika 5 halafu lala tena, hali hiyo itatoweka.
Unapolala zingatia au jiepushe ukiwa umetazama juu yaani kulala chali. Kila mtu anashauriwa kupunguza mawazo mengi wakati wa kulala.
Ushauri mwingine wa kuzingatia ni kulala katika muda mzuri na jaribu kupata muda mrefu wa kulala usingizi na kwa mtu mzima kitaalamu inashauriwa ulale kati ya saa 6 mpaka 8.
Usiku unashauriwa kuwa uwe na ratiba ya kulala. Hii maana yake ni kwamba jaribu kuwa na muda maalum wa kulala ikiwa ni saa 4 usiku basi iwe muda huo wakati wote.
Lakini pia unashauriwa kula vizuri kabla hujalala. Ukifanya haya tuliyoyaelezea hapa, utaepuka kukabwa na jinamizi.

No comments:

Post a Comment

New