Rais JK akiagana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Ikulu mara baada ya mazunguzo jana.
Leo wanakutana tena kuendelea na mazungumzo yao
...akiagana na Mhe. Tundu Lissu
....akiagana na Mhe. John Mnyika
...akiagana na Prof. Adabballah Safari
..Mhe. Lissu akisepa taratibu kutoka Ikulu
...mambo yalivyokuwa ndani wakati wakipata chai na juisi...ilikuwa kirafiki zaidi.
PICHA: Hisani ya Ikulu
************************************************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe
wa Serikali yake leo, Jumapili, Novemba 27,
2011, amekutana na kufanya mazungumzo
na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA).
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika
Ikulu, Dar Es Salaam, yamefanyika katika
mazingira ya urafiki na ujumbe wa CHADEMA
umewasilisha mapendekezo yake kuhusu
mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya
Tanzania. Serikali imepokea mapendekezo
Hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana
kukutana tena asubuhi ya kesho, Jumatatu,
Novemba 28, 2011, ili kuipa nafasi Serikali
iweze kutafakari mapendekezo hayo.
Lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa
Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa
kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya
sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na
amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa
ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.
Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu
umuhimu wa kutunga Katibu Mpya kama
Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa
wakati wa salamu zake za mwaka mpya
Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba
ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa
miaka mingine 50 ijayo.
Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Rais
aliwahakikishia wajumbe hao wa CHADEMA
wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho,
Mheshimiwa Freeman Mbowe kuwa ni dhamira
yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa
Tanzania inapata Katiba mpya.
Katika mkutano huo, pande zote mbili
zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana
kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba
Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na
kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na
umoja wa kitaifa.
Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa
mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia
misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa
la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo
vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa
misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa
misingi ya maeneo.
IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NOVEMBA 27, 2011
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment