UNAWEZA kuwa makini sana na kila kitu unachochokula au unachokunywa  kwa lengo la kulinda afya yako, lakini kama wakati wa kulala hupati  usingizi, hali hiyo inaweza kuathiri afya yako.
Halikadhalika,  kama mahali unapolala (kitandani au jamvini) na mazingira yake  hayaendani na mahitaji ya mwili wako, huwezi kuwa na afya njema pia.
Mahali  tunapolala pamoja na suala la kupata usingizi ni kitu muhimu sana kama  kilivyo chakula. Utakumbuka kwamba karibu nusu ya maisha yetu  tunayamalizia kitandani. Kama mtu ukijaaliwa kuishi duniani kwa muda wa  miaka 60, kwa mfano, miaka 20 au 25 utakuwa umeitumia kwa kulala.
Unapolala,  usingizi hufanyakazi ya kurejesha nguvu ya ubongo na mwili iliyopotea  wakati wa mchana. Usingizi hurejesha upya nishati ya mwili na ubongo  inayokuwezesha kupata akili ya kuainisha matatizo na kuyapatia ufumbuzi.  Vile vile hukuwezesha kuamka asubuhi ukiwa na nguvu mpya ya kupambana  na masuala mengine ya siku hiyo.
KWA NINI USIPATE USINGIZI?
Kama  usingizi ndiyo muhimu kiasi hicho, kwa nini mtu usilale na kupata  usingizi? Kuna sababu kadhaa zinazoweza kukufanya usipate usingizi,  kuanzia chakula unachokula hadi mahali unapolala. Lakini habari njema ni  kwamba kasoro zote unaweza kuzirekebisha na kupata usingizi mnono.
Kama  una matatizo wakati wa kulala, kama vile kukosa usingizi, kuamka usiku  mara kwa mara, kujisikia mchovu unapoamka asubuhi, au unahitaji  kuboresha usingizi wako, kuna mambo mengi ya kufanya, yakiwemo haya  yafuatayo:
HAKIKISHA unalala muda ule ule kila siku na muda mzuri ni saa 4:00 usiku.
JIEPUSHE  kula vyakula muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, hususan vitafunwa  (snacks) vitokanavyo na nafaka na vyenye sukari. Badala yake kula  vyakula vyepesi vya kuongeza protini mwilini, kama vile maziwa, n.k.
HAKIKISHA  chumba unacholala kisiwe na baridi au joto sana. Wastani mzuri wa  kiwango cha joto kinachokubalika kiafya ni nyuzi joto kati ya 18 na 21.
EPUKA kunywa kahawa au chai muda mfupi kabla ya kulala, vinywaji hivi huathiri usingizi kwa kiasi kikubwa.
HAKIKISHA  unafanya mazoezi mara kwa mara, lakini siyo muda mfupi kabla ya kulala.  Fanya mazoezi mapema na upate muda mrefu wa kupumzika kabla ya kupanda  kitandani.
MWISHO kitanda, shuka na mto unaolalilia, hakikisha  una ubora unaotakiwa. Shuka ya kujifunika na mto uliotengenezwa kutokana  na pamba halisi (cotton wool) ni bora zaidi kuliko zilizotengenezwa kwa  malighafi zingine, kama ‘polyester’, ‘synthetics’ n.k., ambazo  zinadaiwa kuwa na kemikali zenye madhara kiafya.
My Web
Emmanuel
CONTACT
Tuesday, November 8, 2011
Ukosefu usingizi una athiri afya yako
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment