Wafuasi wa dini ya Sikh wakiwa katika  sherehe hiyo.
salam,
MAELFU ya wafuasi wa dini ya Sikh  walijitokeza siku ya Jumapili tarehe 6 Novemba 2011 katika mji wa  Southall, Middlesex UK ili kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi  wa dini yao Guru Nanak aliyezaliwa mwaka 1469 nchini Pakistan.
Muasisi wa Dini ya Sikh
Wakati akiwa na umri wa miaka 30 alipotea kwa hali ya miujiza kwa  muda wa siku tatu. Alipo rejea alianza kuhubiri, kufundisha na kuandika  dini ya Sikh wakati wa maisha yake yote. Pia Guru Nanak alisafiri dunia  nzima kuitangaza na kujadili dini hii kwa waumini wengine kama waislamu  pamoja na Wahindu.
Kwa  miaka zaidi ya 550 wafuasi wa dini hii wamekuwa na desturi hii ya  kusherehekea siku moja kabla ya kuzaliwa kwake Guru Nanak kwa kuandaa  maandamano haya makubwa ya Sherehe hii ambayo hufanyika India pamoja na  baadhi ya sehemu za nchi ya Uingereza.
Kwa  kawaida sherehe hizi huongozwa na wafuasi wakuu watano wanaojulikana  kama "Panj Piare" wakiambatana na waimbaji, wanamuziki na timu ya  wacheza Upanga (Martial Arts) kuelekea hekaluni kwao "Gurdwara" Sri Guru  Singh Sabha, hapa Southall hekalu lao ndio kubwa kuliko yote katika  bara la ulaya.
Maandamano ya Southall yanaitwa Nagar Kirtan,
Asanteni,
No comments:
Post a Comment