Mipango ya sheria mpya itakayowaruhusu
wapenzi wa jinsia moja nchini Ufaransa kuoana na kupata watoto
inajadiliwa katika mkutano muhimu wa baraza la mawaziri la Rais Francois
Hollande.
Ufaransa inaruhusu uhusiano wa pamoja kati ya
wapenzi wa jinsia moja lakini rais wa nchi hiyo alioongoza jitihda za
kuwaongezea haki zao kama sehemu ya kampeini yake ya uchaguzi mapema
mwaka huu.Kwa wapenzi wengi wa jinsia moja, mabadiliko katika sheria hii yalipaswa kufanyika kitambo. Wanataka nafasi sawa kuwa na familia kama ilivyo kwa wapenzi wengine wa kawaida.
Katika sheria hiyo iliyopendekezwa, wapenzi wa jinsia moja wataruhusiwa kuasili watoto kwa pamoja.
Na kutakuwa na mabadiliko katika stakabadhi rasmi, ambapo mama na baba wataondolewa na badala yake kuwekwa mzazi wa kwanza na mzazi wa pili.
Lakini mabadiliko hayo yaliyopangwa yameshutumiwa vikali na wanasiasa wa mrengo wa kulia ambapo mmoja alisema huenda hili likachangia ndoa za wake au waume wengi.
Mswada huu utakapowasilishwa kwenye baraza la mawaziri, utajadiliwa bungeni ifikapo Januari.
Chama cha kisoshalisti cha Rais Hollande kina wingi wa wabunge wanaohitajika lakini kutokana na kuwepo mzozo huenda akawa anategemea kura zote kuhakikisha kuwa mswada huo utapitishwa na kuwa sheria
No comments:
Post a Comment