…
Michelle Obama akionyesha upendo kwa mumewe baada ya ushindi wake.
Obama akitoa hotuba baada ya ushindi wake leo huko Chicago.
Akiwa na mkewe, Michelle, na binti zake Sasha (wa pili kulia) na Malia Obama wakisherehekea ushindi wake.
Obama ambaye pia ni Mkuu wa Majeshi, akiwa Ikulu ambako atakaa kwa miaka minne tena.
Familia nzima ya Obama ikifurahia ushindi.
Obama akitoa hotuba yake mbele ya umati wa watu huko Chicago.
Michelle Obama akiwa amepandwa ‘mzuka’ kwa ushindi wa Obama.
Mkutano wa Obama ulivyokuwa umepambwa kwa rangi mbalimbali za taifa hilo.
Mke wa Romney aitwaye Ann Romney, akimliwaza mumewe baada ya kushindwa.
ALIYEKUWA mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, Barack Obama, amemshinda mpinzani wake kutoka chama cha Republican, Mitt Romney, katika uchaguzi uliofanyika jana.
Obama ambaye alishinda urais wa nchi hiyo miaka minne iliyopita, amesema hivi sasa ana dhamira ya hali ya juu zaidi na nguvu zaidi za kufanya kazi zake. Aliyasema hayo huko Chicago wakati wa hotuba yake ya kupokea ushindi huo.
Hata hivyo, wagombea wote wawili wa kinyang’anyiro hicho walitoa wito wa umoja kwa watu wa nchi hiyo kwa ajili ya maendeleo.
Katika hotuba hiyo alimshukuru mkewe na mabinti zake , Sasha na Malia, ambao alisema ni “wasichana wawili jasiri kama mama yao.”
Katika uchaguzi huo Obama alipata kura nyingi hususani katika majimbo ya Ohio, Iowa, Wisconsin, Pennsylvania, New Hampshire na Virginia.
Kiongozi huyo alipongezwa haraka na viongozi wengine duniani wakiwemo David Cameron wa Uingereza na Benjamin Netanyahu.
PICHA KWA HISANI YA : REUTERS, AP, EPA, AFP/GETTY IMAGES , KEYSTONEUS-ZUMA/REX FEATURES
Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani yameanza kutolewa kutoka maeneo mbali mbali ya nchi.
Rais Barack Obama ameshinda katika majimbo
ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni
Michigan na Pennsylvania, pamoja na mengine ambayo alishinda katika
uchaguzi wa mwaka 2008.Mamilioni ya watu walijitokeza kupiga kura siku ya Jumanne. Mshindi huenda akajulikana baada ya masaa kadhaa kuanzia sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu yakitolewa.
Kura za maoni kabla ya kufanyika uchaguzi huu zilionyesha kinyang'anyiro kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi wa kura chache tu Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya Virginia na Ohio nayo yakifunga mapema.
Kwa sasa kura za Electoral College zinaonyesha Obama yuko nyuma ya Romney kwa kura sita
No comments:
Post a Comment