Sehemu ya burudani ya Seaside Heights, New Jersey, ilivyoharibiwa.
Nyumba zilizokumbwa na kimbunga Superstorm Sandy
Sehemu ya Daraja la Mantoloking, New Jersey, ilivyoharibiwa.
Mama aliyekumbwa na simanzi za kimbunga hicho,
huko Lavallette, New Jersey.
Boti zilizokumbwa na kimbunga karibu na jiji la Jersey, New Jersey.
Rais Obama akimliwaza mmoja wa waathirika wa kimbunga hicho.
Kushoto ni Gavana wa New Jersey, Chris Christie.
Vyakula vilivyoharibika vikisubiri kutupwa huko Brooklyn, New York.
Mkazi wa Seaside Heights akitazama madhara ya kimbunga kutoka
kwenye mabaki ya makazi yake.
Nyumba zilizoharibiwa huko Seaside Heights, New Jersey.
Uharibifu uliotokea huko Breezy Point, New York,
ambako moto uliharibu nyumba 110.
Wafanyakazi wakisafisha eneo la Long Beach Island, New Jersey,
baada ya kimbunga hicho.
Freddie Nocella, Jr, akitazama mabaki ya mali za babu yake katika kijiji cha Babylon, New York.
SAFARI za ndege zimerejea tena katika Jiji la New York, Marekani,
japokuwa taratibu, na shughuli zingine za mambo ya soko la fedha
zimerejea kwa kutegemea jenereta za umeme. Vilevile, pamoja na kwamba
njia za treni za chini ya ardhi hazijatengemaa vyema, watu wengi
walionekana wakitembea kuvuka Daraja la Brooklyn kuelekea sehemu ya
Manhattan, jambo ambalo ni kinyume na ilivyokuwa wakati wa shambulio la
kigaidi kwenye jiji hilo lililofanyika Septemba 11, 2001 ambapo watu
wengi walikuwa wakikimbia kutoka Manhattan kuelekea Brooklyn.Hayo yote yametokana na kimbunga kinachoitwa Superstorn Sandy ambacho kiliikumba sehemu ya kaskazini-mashariki mwa sehemu hiyo na kuua watu zaidi ya 70 juzi (Jumatano). Maeneo makubwa ya jiji hilo bado hayana umeme na shughuli zake nyingi zimesimama.
Sehemu kubwa ya wakazi wa jiji hilo, hadi habari hizi zinachapishwa, walikuwa wakihangaikia umeme, maji na huduma mbalimbali.
Gavana wa jiji hilo, Andrew Cuomo, alisema sehemu kadhaa za treni za chini ya ardhi zitaanza kufanya kazi leo, na kwamba njia tatu miongoni mwa saba za chini ya ardhi eneo la East River, zimenyonywa maji ili kuondoa vikwazo kabla ya kuanza huduma kamili.
Kwa kawaida, mabasi jijini New York huhudumia watu milioni 2.3 kwa wastani, lakini baada ya kimbunga hicho yalijikuta yakilazimika kuhudumia watu milioni 5.5 wakiwemo wale waliokuwa wakitumia treni za nchini ya ardhi.
Maeneo ya magharibi ya Wisconsin na Carolinas, kusini, kaya na biashara zaidi ya milioni sita zilikuwa hazina umeme, ikiwa nipamoja na kaya 650 jijini New York, alisema Meya Michael Bloomberg.
Meya huyo alisema wagonjwa 500 wamehamishwa kutoka Hospitali ya Bellevue kutokana na uharibifu wa kimbunga hicho na wagonjwa wengine 300 walihamishwa kutoka Hospitali ya Manhattan kutokana na ukosefu wa umeme.
Safari za ndege pia zimeanza katika viwanja vya Kennedy na Neward japokuwa kwa kiasi fulani, japokuwa uwanja wa LaGuardia bado haujaanza kupokea ndege kutokana na uharibifu uliotokea.
Vilevile, sehemu mbalimbali za jiji hilo, askari maalum walikuwa wakigawa vyakula vya kuliwa hapohapo vilivyokuwa katika magari mbalimbali, ambapo pia walikuwa wakishughulika na uokoaji wa watu kutoka katika majengo marefu.
CHANZO: LEADER-TELEGRAM
(Picha kwa hisani ya: AP, EPA, Reuters, Getty Images)
No comments:
Post a Comment