My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, August 15, 2012

Tuzingatie muda bungeni na sehemu nyingine za kazi

Muda mwingi umekuwa ukipotea bungeni kutokana na baadhi ya mawaziri na wabunge kuanza kuchangia hoja kwa kuongea mambo ambayo kwa kweli hayana msingi wowote kwenye hoja husika. Kwa mfano, unakukuta waziri anaanza kujibu hoja za wabunge waliyochangia makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa kuwataja majina wabunge wote waliochangia wote. Wakati mwingine inamchukua waziri karibu nusu saa akitaja na kushukuru wale wote waliochangia kwenye bajeti yake.

Hotuba nyingine za bajeti zinaanza na utangulizi mrefu ambao hauna uhusiano wowote na bajeti husika. Kwa mfano soma hapo chini utangulizi wa hotuba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka 2012/2013. Zaidi ya kupoteza muda utangulizi huu hauhusiani kabisa na hotuba ya makadirio ya wizara. Ifike wakati tuzingatie muda hasa bungeni na sehemu nyingine za kazi hasa zile za umma. 

HOTUBA YA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA, MHESHIMIWA SHAMSI VUAI NAHODHA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2012/2013

UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, baada ya Bunge lako Tukufu kupokea taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013.

2. Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, aliyenijalia afya njema na kuniwezesha kuwasilisha hotuba yangu ya bajeti kwa mwaka 2012/2013. Pili namshukuru kwa dhati Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuniteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Nawathibitishia Waheshimiwa Wabunge wenzangu na wananchi wote wa Tanzania kwamba nitatekeleza majukumu niliyokabidhiwa kwa umakini na uaminifu mkubwa.

3. Mheshimiwa Spika, tatu napenda kutumia fursa hii kuwapongeza Mawaziri na Manaibu Mawaziri walioteuliwa kushika nyadhifa hizi hivi karibuni. Vile vile nampongeza Mhe. James Mbatia (Mb.) kwa kuteuliwa na Mhe. Rais kuwa Mbunge. Nampongeza pia Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge. Vile vile napenda kuwapongeza Watanzania waliochaguliwa na Bunge letu Tukufu kuwa Wabunge wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

4. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2011/2012 Wabunge wenzetu watatu waliiaga dunia. Wabunge hao ni Marehemu Jeremia Sumari, Marehemu Mussa Silima na Marehemu Regia Mtema. Napenda kutoa pole za dhati kwako Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge, ndugu, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla kwa msiba huo mkubwa uliotupata. Namuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho zao Peponi. Amin.

5. Mheshimiwa Spika, halikadhalika, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Edward Lowassa, Mbunge wa Monduli kwa kutupa ushauri na mapendekezo mazuri sana wakati wakichambua mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yangu. Kamati hii imekuwa ikiishauri vyema Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuhusu njia mbalimbali za kuimarisha utendaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Kujenga Taifa ili liweze kutekeleza majukumu yake ya Ulinzi wa nchi yetu.

6. Mheshimiwa Spika, kabla sijatoa maelezo yangu kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2012/2013 napenda kuungana na Waheshimiwa Wabunge kuwapongeza Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda (Mb), Waziri Mkuu, Waziri wa Fedha, Mhe. Dk. William Mgimwa (Mb), na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Mheshimiwa Steven Wasira (Mb) kwa hotuba zao ambazo zimetoa mwelekeo katika masuala ya Mipango, Uchumi, Mapato na matumizi ya Serikali kwa kipindi cha mwaka 2012/2013.

Utaratibu wa uteuzi wa majaji: Utetezi wa Tundu Lissu mbele ya Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge

UTANGULIZI
 
Julai 13, 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliwasilisha Maoni yake kuhusu Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Pamoja na mambo mengine, Maoni ya Kambi yalihusu utaratibu wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Tanzania.

Maoni ya Kambi yalizua mjadala mkubwa ndani na nje ya Bunge huku wachangiaji wengi wakimtuhumu Msemaji wa Kambi kwa “kuidhalilisha” Mahakama na/au “kuwadhalilisha majaji” (Gosbert Blandes-Karagwe CCM); “kuwavunjia heshima majaji” (Naibu Spika Job Ndugai); kuwatukana na kuwadhalilisha majaji (Murtaza Mangungu-Kilwa Kaskazini); “kuwa-offend, kuwadhalilisha na kuwanyanyasa majaji” (Assumpter Mshama-Nkenge CCM); “kufedhehesha Mahakama na majaji” (Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema).

Aidha, Msemaji wa Kambi alishambuliwa kwa kudaiwa kuwa mfitini na asiye na akili timamu (Muhammad Chomboh- Magomeni CCM)); na “kujiamini kwamba yeye anajua zaidi kuliko watu wengine wote” (Mangungu). Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alilihakikishia Bunge kwamba “... haijatokea hata siku moja katika nchi hii Rais akamteua Jaji wa Mahakama Kuu bila kuzingatia mapendekezo yaliyopelekwa kwake na hii Tume ya Uajiri wa Mahakama.” Zaidi ya hayo, “... labda Mheshimiwa Lissu anamjua Jaji angalau mmoja na anaweza akamtaja aseme Jaji huyu ametolewa tu mitaani na Mheshimiwa Rais, yupi hakuna… hawa majaji wote walioteuliwa wamepitia mchakato huu wa kikao kizito sana cha watu ambao ndiyo wenye sheria ya nchi hii.”

Baadaye Msemaji wa Kambi alitakiwa kufuta kauli yake kuhusu uteuzi wa majaji usiofuata utaratibu uliowekwa na Katiba. Msemaji wa Kambi alikataa kufuta kauli hiyo ambako Mwenyekiti wa Kikao alielekeza Msemaji wa Kambi apelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi. Alichukua uamuzi huo ili masuala hayo yapatiwe ufafanuzi ili wananchi wapate picha kamili na ya kweli kuhusu jambo hili muhimu. Maelezo haya yana lengo la kutoa ufafanuzi huo.

Katika maelezo yake kwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya BUnge, Lissu alisema, “Nitajitahidi kwa kadri inavyowezekana kutoa ushahidi unaothibitisha kwamba siyo tu kwamba utaratibu wa kikatiba katika uteuzi wa majaji umekiukwa mara nyingi, bali pia majaji wengi walioteuliwa kwa utaratibu wa nje ya Katiba wamekuwa hawana ‘uwezo, ujuzi na kwa kila hali hawakufaa kukabidhiwa Madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu.”

Olympiki: Matokeo rasmi ya mbio za marathon kwa wanaume


Stephen Kiprotich wins the marathon

Mganda Stephen Kiprotich ameshinda medali ya dhahabu katika mbio za marathon (wanaume) akifuatiwa na Wakenya Abel Kirui and Wilson Kipsang. Mtanzania Faustine Mussa alishika nafasi ya 33 baada ya kukimbia kwa masaa mawili, dakika 17 na sekunde 39 huku Samson Ramadhani akishika nafasi ya 66 kwa kukimbia kwa muda ta masaa mawili, dakika 24 na sekunde 53. Matokeo rasmi kama yanavyoonyeshwa hapo chini.










0 

AWAMU YA TATU YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF III), UWANJA WA JAMHURI, DODOMA, 15 AGOSTI, 2012 UKIFUNGULIWA NA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE.


 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya 
Jamii (TASAFAIII) Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Agosti 15, 2012.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wakati akizindua 
awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAFAIII) Uwanja wa Jamhuri 
mjini Dodoma leo Agosti 15, 2012.

Sunday, August 12, 2012

RAIS KIKWETE AONANA NA RAIS MPYA WA GHANA, ATEMBELEA MASHAMBA YA MANANASI




 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiagana na Rais John Dramani 
Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini  Accra jana Agosti 11, 2012 
baada ya  kumtembelea na  kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi 
hiyo Marehemu John Evans Atta Mills aliyezikwa juzi.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na Rais John Dramani 
 Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini  Accra jana Agosti 11, 2012  
 wakati alipomtembelea kiongozi huyo mpya wa Ghana na  kumpa pole ya msiba 
wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama mananasi yakitayarishwa kwa ajili ya 
kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha  Bomarts Farms Ltd 
 katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra jana Agosti 11, 2012.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa mananasi yanayolimwa  
kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shamba la Bomarts Farms Ltd katika kijiji cha 
Dobro katika eneo la Nsawam  nje kidogo ya jiji la Accra jana Agosti 11, 2012. Kulia 
kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya 
bluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo, Mhe. Kwesi Ahwol.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya  mananasi katika 
shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya jiji la Accra. Kulia kwake ni 
Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd, Bw Emmanuel B. Koranteng ambaye 
amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka 27. Mwalimu Nyerere aliwahi 
kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka ya 1980 kujionea ukulima 
huo wa matunda.

(PICHA NA IKULU)

TAMASHA LA DINI "LOVE TANZANIA" LILIVYOTIA FORA VIWANJA VYA JANGWANI JIJI DAR.



Pichani Juu na Chini ni Umati wa Watanzania uliofurika kwenye 
Tamasha la Dini lililopewa jina la LOVE TANZANIA linaloendelea 
katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam likiongozwa na Askofu 
Andrew Palau kutoka Marekani.
Vijana walioongoza na Askofu Andrew Palau wakitoa burudani na 
mafundisho ya dini kwa njia muziki.
Wana Dar es Salaam wakiendelea kumiminika katika
 viwanja vya Jangwani.
Mmoja wa Wahudumu katika Tamasha hilo akipata chakula cha 
mchana na familia yake Uwanjani hapo.
Umati wa watu ukiwa kwenye foleni ya kupata 
huduma ya chakula uwanja hapo.
Moja ya Magari na wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi iliyopewa 
Zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd likiwa 
limepaki katika Viwanja vya Jangwani kuhakikisha Usafi unazingatiwa 
Uwanjani hapo wakati tamasha la Dini lililopewa jina la 
LOVE TANZANIA likiendelea.
Pichani Juu na Chini ni moja ya michezo iliyofanyika kama sehemu ya 
burudani uwanjani hapo ambapo ilionekana kuvutia Umati wa Watanzania
 waliohudhuria tamasha hilo.
Vijana, Watoto kwa Wazee wakitazama mchezo wa mapikipiki.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd 
akihakikisha swala usafi linazingitiwa uwanjani hapo 
kama inavyoonekana.
Wananchi waliohudhuria tamasha hilo wakishuhudia 
mchezo wa Baiskeli.
Palikuwa hapatoshi Jangwani.
Ulinzi na Usalama kwa raia ulikuwepo.
Familia zikiendelea kula, kunywa na kufurahi uwanjani hapo.
Hili ni Jukwaa la kimataifa kutoka nchini Uganda maalum kwa ajili ya 
Tamasha lililopewa jina la LOVE TANZANIA likiongozwa na 
Askofu Andrew Palau kutoka nchini Marekani, haijawahi kutokea 
kusikia Sound na Mziki wa Ukweli nchini kwa mliohudhuria 
tamasha hili mtasema.

Friday, August 10, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AWASILI ACCRA KUSHIRIKI MAZISHI YA RAIS WA GHANA JOHN EVANS ATTA MILLS


 

  

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili jana Agosti 9, 2012 katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Kotoka jijini Accra, Ghana, kuhudhuria mazishi
ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills anayetarajiwa
kuzikwa leo Ijumaa Agosti 10, 2012. PICHA NA IKULU

Friday, August 3, 2012

TAARIFA KUTOKA SIMBA SC KUHUSU MKUTANO MKUU NA USAJILI WA MRISHO NGASSA



MKUTANO MKUU
MKUTANO Mkuu wa Wanachama Wote wa Simba utafanyika Agosti tano mwaka huu katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay kama ilivyopangwa.
Mipango yote kwa ajili ya mkutano huo muhimu kikatiba imekamilika na klabu inawaomba wanachama wake wote hai kuhudhuria mkutano huo muhimu.
Uongozi umepanga kutoa mabasi kwa ajili ya kuwasafirisha wanachama wake kutoka katika maeneo mbalimbali kwenda katika ukumbi wa mikutano.
Kutakuwa na mabasi matatu kwenye eneo la Shibam Magomeni... Mabasi matatu Temeke mwisho na mabasi matatu katika makao makuu ya Simba SC Mtaa wa Msimbazi.
Pia klabu itapeleka mabasi mawili katika wilaya za Mkuranga na Kibaha kwa ajili ya kuwaleta wanachama wake walio katika mkoa wa Pwani kuhudhuria mkutano huo.
Mwenyekiti wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, amewahakikishia wanachama wa Simba kwamba mkutano huo utaendeshwa kisasa na usalama umehakikishwa kwa asilimia 100 kwa vile eneo la mkutano liko chini ya Jeshi la Polisi.
"Napenda kuwahakikishia wanachama wote wa Simba kwamba mkutano huo utakuwa bora na wote watakaokuja watafurahi na kujisikia fahari kuwa washabiki wa klabu ya soka ya Simba. Kwa wale ambao wamepanga kuja kufanya vurugu kwenye mkutano huo, klabu itaviachia vyombo vya dola vifanye kazi yake," alisema.
NGASSA
MCHEZAJI mpya wa Simba, Mrisho Ngassa, leo amekabidhiwa jezi namba 16 atakayokuwa akiitumia kwenye klabu yake msimu huu.
Ngassa alikabidhiwa jezi yake hiyo katika makao makuu ya Simba Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.
Kaburu alisema Simba inamkaribisha Ngassa kwa moyo mmoja na kwamba wapenzi wote wa Wekundu wa Msimbazi wana imani kubwa naye kwani uwezo wake mkubwa wa soka unafahamika ndani na nje ya nchi.
"Tunashukuru kwamba tumekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyu. Tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza muda wa mkopo wake kutoka Azam na ni imani yetu kwamba ujio wa Ngasa utaimarisha zaidi timu kwani yeye ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, anawapenda," alisema. 
Akizungumza katika tukio hilo, Ngassa alisema amefurahi kusajiliwa na Simba kwani ni sawa na historia kujirudia, akikumbusha kwamba baba yake mzazi, Khalfan Ngassa, aliwahi kuwa mchezaji wa klabu katika miaka ya 1990.
Kabla ya mkutano huo na waandishi wa habari, Ngassa alifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba katika ufukwe wa Coco, jijini Dar es Salaam ambako Simba inaendelea na mazoezi yake chini ya makocha Amatre Richard na James Kisaka.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

HATIMAE MRISHO NGASSA AANZA MAZOEZI SIMBA SC

 
Mrisho Ngassa akiwa mazoezini.
 
Gari aina ya Toyata Verossa  alilopatiwa Mrisho Ngassa.

  

   

  

  

  
Mrisho Ngassa pamoja na wachezaji wa Simba wakiwa mazoezi.
 
Mashabiki wakifuatilia mazoezi ya Simba.
 
Ngassa akiwa kwenye gari lake.
 
Wanahabari wakimhoji Ngassa.
Na Saleh Ally
KIUNGO mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa leo asubuhi ametua rasmi na kuanza mazoezi katika timu  yake mpya, Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba.
Ngassa alikuwa mmoja wa wachezaji wa Simba waliokuwa mazoezini kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.
Mashabiki kibao walijitokeza kumshuhudia kiungo huyo ambaye amejiunga Simba kwa kulipwa dau la Sh milioni 30 pamoja na gari aina ya Toyota Verossa lenye thamani ya Sh milioni 18.
Baadhi ya mashabiki waliokuja eneo la tukio ni vijana waliokuwa katika mlolongo wa kuwania kushinda shindano la muziki la BSS zilizokuwa zikiendelea katika eneo hilo.
Ngassa alionekana kuwa mwenyeji tu na alifanya mazoezi vizuri kwa ushirikiano na wenzake. Mazoezi hayo yalikuwa chini ya Kocha Msaidizi, Richaed Amatre raia wa Uganda.
Simba imeilipa Azam kitita cha Sh milioni 25 ili kumchukua Ngassa ambaye amekuwa akidai hana raha.

Thursday, August 2, 2012

MAELEZO BINAFSI YA ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto
Ndugu Waandishi,
Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba hata mimi nimeshiriki katika vitendo vya rushwa, kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Taarifa hizo, kama kawaida ya uzushi mwingine wowote zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa kiasi cha kuukanganya umma.
Nafahamu nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa. Mkakati huo wa kuniunganisha na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanaotuhumiwa kwa kupokea Rushwa unatekelezwa kwa njia zifuatazo:
Kumekuwa na kauli za watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakizieneza na hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zangu zinatokana na ushawishi wa rushwa; Kuna taarifa ambazo zimeandikwa tena katika kurasa za mbele za baadhi ya vyombo vya habari zikidai” Zitto kitanzini” ama ‘Zitto sawa na popo nundu” zikiashiria kwamba na mimi ni mla rushwa; na Waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wamefikia kuaminishwa habari hizi kiasi cha wengine kuuliza kwa nini Mhe. Zitto Kabwe hakutajwa katika orodha iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani.
Ndugu Waandishi,

Majeshi wa Serikali, waasi yapambana kuupigania Mji wa Allepo


Mwanajeshi kazini
MAPAMBANO ya kuuwania Mji wa Allepo baina ya vikosi vya Serikali na waasi yamezidi kupamba moto huko Syria, ambapo sasa waasi wamekiteka kituo muhimu cha ukaguzi kwenye mpaka baina ya nchi hiyo na Uturuki.
Kufuatia hali hiyo, Ufaransa imetangaza kutaka kuitisha kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Waasi wamekitwaa kituo hicho cha Anadan kilichopo kaskazini magharibi mwa mji huo wa Aleppo hii baada ya mapigano makali yaliyodumu saa10 mfululizo. Hatua hii inawapa uhuru wa kusafiri kwenye maeneo ya kaskazini na Uturuki.
Shirika la Habari la AFP linaarifu kuwa vifaru saba na magari yenye silaha yamechukuliwa na waasi kutoka vikosi vya serikali, huku mengine manane yakiharibiwa vibaya.
Wanajeshi sita wameuawa kwenye mapigano hayo na wengine 25 wamekamatwa na kuwekwa kizuizini ambapo waasi wanne pia wameuwa. Kamanda wa Jeshi Huru la Waasi wa Syria, FSA, Khalid al Shamsi anasema kuwa mambo ni mazuri kwa upande wao.
“Hali ni nzuri sana kwetu, tumeuchukua mkoa wa Al Bab na wapiganaji wetu wataendelea kulithibiti jimbo la Aleppo. Sasa tunaimarisha nguvu yetu Aleppo kwa kuwaunganisha wapiganaji wa huko. Tunapata silaha na vifaa kutoka huko na sehemu nyengine za mkoa wa Al Bab”. alisema, Kamanda Shamsi.
Mapigano hayo yamewalazimisha kiasi ya raia 200,000 kuukimbia mji huo. Umoja wa Mataifa umeonya kuwa kuna uwezekano mji huo ukakumbwa na janga la kibinaadamu. Mkuu wa umoja huo anayeshughulika na misaada ya kibinaadamu, Valerie Amos, amesema kuwa bado kuna idadi kubwa ya watu wamekwama kwenye mji huo. Watu wengi wametafuta hifadhi kwenye maeneo ya shule na majengo ya umma. Amos anasema kuwa wanahitaji haraka chakula, magodoro, madawa na maji ya kunywa.
Mataifa ya magharibi yameeendelea na juhudi zao za kukomesha hali hiyo na sasa Ufaransa imetangaza kuitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutafuta namna ya kusitisha mauwaji hayo.
Waziri wa mambo ya Nje wa nchi hiyo, Laurent Fabius, amemuita Rais Bashar al-Assad wa Syria kuwa ni muuwaji na kuutaka umoja huo ufanye kila liwezekanalo kuzuia mauwaji yasiendelee. Fabius amesema kuwa nchi yake itaitisha kikao hicho kabla ya mwisho wa wiki hii.
Ufaransa inatarajia kuchukua kiti cha Urais wa baraza hilo hapo Jumatano. Rais Francois Hollande amesema kuwa atajitahidi kuzishawishi Urusi na China zikubali hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya utawala wa Assad. Nchi za magharibi hadi sasa hazijaweza kukomesha mauwaji ya Syria kutokana na pingamizi za nchi hizo zenye maamuzi ya kura ya turufu kwenye baraza la usalama.
-DW

Vodacom yalalamikiwa kuhusu upendeleo tuzo za blogu, tovuti


Vodacom Tanzania
Ujumbe wa Makene kuhusiana na tuzo za bloggerz zilizotolewa na Vodacom Hivi majuzi niliskia kuwepo kwa tuzo za waandishi wa habari za mtandaoni maarufu kama waandishi wa magazeti tando (blogs). Katika Tuzo hizo ambazo ziliandaliwa kwa vigezo wanavyovijua Vodacom, wametajwa washindi fulani. Kama mdau wa kawaida katika magazeti tando, miongoni mwa waasisi wa Bloger wa kwanza kabisa wa Kitanzania naamini kwa sasa kama nchi hii itakuwa inaendeshwa kishkaji, kirafiki, kima kundi na ikaachwa bila kukemewa basi siku si nyingi tutapoteza ladha ya mashindano yanayopima viwango na ubora wa kazi hali itakayofanya nchi kubakia kuwa ya wababaishaji kila siku.
Eneo hili la magazeti tando niliwahi kulilalamikia kutokana na kukosekana ubunifu hasa inapotokea habari moja inajaa kila blog kama ambavyo ipo katika magazeti ya Tanzania. Kwa kuona hili hili nashangaa blog iliyo na kazi ya kubandika picha za magazeti ya kila siku ama habari za wasanii walio nje au kuchota mawazo ya watu katika FB na twitter, au kusubiri taarifa za Maafisa Habari ikaibuka mshindi kwa kuwa tu eti inaonesha kuwa na wasomaji wengi. Kwamba hamjui kuwa ukiseti weblog yako ihesabu wanaoitembelea itahesabu bila kujali ni nani anaingia mara ngapi?

New