Pichani
Juu na Chini ni Umati wa Watanzania uliofurika kwenye
Tamasha la Dini
lililopewa jina la LOVE TANZANIA linaloendelea
katika viwanja vya
Jangwani jijini Dar es Salaam likiongozwa na Askofu
Andrew Palau kutoka
Marekani.
Vijana walioongoza na Askofu Andrew Palau wakitoa burudani na
mafundisho ya dini kwa njia muziki.
Wana Dar es Salaam wakiendelea kumiminika katika
viwanja vya Jangwani.
Mmoja wa Wahudumu katika Tamasha hilo akipata chakula cha
mchana na familia yake Uwanjani hapo.
Umati wa watu ukiwa kwenye foleni ya kupata
huduma ya chakula uwanja hapo.
Moja
ya Magari na wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi iliyopewa
Zabuni ya
kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd likiwa
limepaki katika
Viwanja vya Jangwani kuhakikisha Usafi unazingatiwa
Uwanjani hapo wakati
tamasha la Dini lililopewa jina la
LOVE TANZANIA likiendelea.
Pichani
Juu na Chini ni moja ya michezo iliyofanyika kama sehemu ya
burudani
uwanjani hapo ambapo ilionekana kuvutia Umati wa Watanzania
waliohudhuria tamasha hilo.
Vijana, Watoto kwa Wazee wakitazama mchezo wa mapikipiki.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd
akihakikisha swala usafi linazingitiwa uwanjani hapo
kama inavyoonekana.
Wananchi waliohudhuria tamasha hilo wakishuhudia
mchezo wa Baiskeli.
Palikuwa hapatoshi Jangwani.
Ulinzi na Usalama kwa raia ulikuwepo.
Familia zikiendelea kula, kunywa na kufurahi uwanjani hapo.
Hili
ni Jukwaa la kimataifa kutoka nchini Uganda maalum kwa ajili ya
Tamasha
lililopewa jina la LOVE TANZANIA likiongozwa na
Askofu Andrew Palau
kutoka nchini Marekani, haijawahi kutokea
kusikia Sound na Mziki wa
Ukweli nchini kwa mliohudhuria
tamasha hili mtasema.
No comments:
Post a Comment