My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, August 29, 2012

Annan kujiuzulu wadhfa wake Syria

Mjumbe wa amani wa kimataifa nchini Syria, Kofi Annan, amesema kuwa mwenendo wa kutotaka kupatana kutoka kwa utawala wa rais Bashar al Assad ndiyo sababu kubwa ya hatua yake ya kujiuzulu ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.
Bwana Annan amesema kuwa harakati za kijeshi kutoka kwa wapiganaji wa upinzani pia zimechangia katika kufanya majukumu yake kuwa magumu na pia mgawanyiko uliokuwepo katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Kofi Annan
Miezi mitano iliyopita Kofi Annan alikabidhiwa jukumu Kubwa la kupatanisha utawala wa Rais wa Syria Bashar Al Assad na waasi wa upinzani wenye nia ya kumng'oa madarakani.
Lakini leo inaelekea maji yamezidi unga na Bw Annan ametangaza nia yake kujihuzulu.
Amesema hatua hiyo imechochewa na ukosefu wa Ushirikiano kutoka kwa Rais Assad na pia makundi ya waasi. Mpango wa kusitisha mashambulio uliopendekezwa na Bw Annan umekuwa ukipuuzwa na pande zote.
Serikali kwa upande wake imeendeleza mashambulio na kusababisha mauaji ya raia huku wapinzani nao wakiimarisha vita dhidi ya serikali.
Vilevile Bw Annan ameshtumu jamii ya kimatifa kwa kutounga mkono kikamilifu juhudi zake. Amesema huku umwagikaji damu ukiendelea nchini Syria jamii ya kimataifa imegawanyika kuhusu jinsi ya kutatua mzozo huo.
Rais Assad hajawahi kukubali upunzani kufanya maandamano ya kupinga utawala wake na badala yake amekuwa akitumia nguvu.
Amekuwa akiungwa mkono na Uchina na Urusi na hata kupewa msaada wa silaha.
Waasi katika mji wa Aleppo nchini Syria
Katika miezi ya hivi karibuni juhudi za Kofi Annan kutafutia mgogoro huo suluhu pia zimekuwa zikisambaratishwa na mgawanyiko kati ya baadhi nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Marekani,Uingereza na Ufaransa zimetofautiana vikali na Uchina na Urusi kuhusu mwelekeo unaofaa kumaliza mapigano nchini Syria.
Baada ya Kofi Annan kujihuzulu mwishoni mwa mwezi huu,haijulikani Umoja wa mataifa utakuwa na jukumu gani katika mpango wa kutafuta amani nchini Syria.
Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Susan Rice amesema juhudi za Annan hazingeweza kufaulu kutokana na utawala wa Rais Assad kupuuza mapendekezo ya kumaliza mapigano.
Naye Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema amejuta kujihuzu kwa Kofi Annan ambaye amemtaja kama mwanadiplomasia shupavu.
Serikali ya Syria inaendelea kutumia nguvu.
Hali katika mji mkuu Damascus ni ya kusikitisha na mjini Allepo makabiliano makali yanaendelea.
Mwelekeo wa Syria sasa umegeuka na kuwa vita badala ya amani.

No comments:

Post a Comment

New