
Mastaa wetu wa filamu hapa nchini, wametokelezeaje sasaaa


Wema Sepetu pia akizungumzia ujio wao 
ndani ya mji wa Moshi, kuwa wao kama Wasanii Nyota wa Filamu wamewasili 
mkoani humo kusaka vipaji vipya mbalimbali vya filamu, usahili huo 
unafanyika kwenye ukumbi wa Mr Price, ulioko mtaa wa Malindi.

Mmoja wa wasanii mahiri katika fani ya
 uigizaji hapa nchini, Wema Sepetu akifanya mahojiano mafupi na Millard 
Ayo wa Clouds FM mapema leo kwenye amsha amsha ya tamasha la Serengeti 
Fiesta ambalo linafanyika jioni ya leo mpaka lyamba ndani ya uwanja wa 
chuo cha Ushirika,ndani ya mji wa Moshi, ambapo katika tamasha hilo 
kiingilio kimepangwa kuwa ni nusu mnyama tu a.k.a 5,000/= kwa kila 
kichwa.

Msanii mwingine nyota katika tasnia ya
 filamu, Aunt Ezekiel akielezea ni namna tamasha la Serengeti Fiesta 
lilivyowambamba wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake, na pia ujio 
wao kuwatafuta wasanii wapya chipukizi katika tasnia hiyo ambayo imekuwa
 ikikua siku hadi siku.


Millard Ayo akifanya mahojiano na Ray a.k.a Vincent Kigosi kuhusiana na ujio wao ndani ya  mji wa Moshi

Jacob Steven a.k.a Steven akifafanua 
jambo mapema leo mtaa wa Malindi kuhusiana na suala zima la wasanii hao 
kulivamia jiji la Moshi.


Wema na Steve Nyerere Wakiwa katika mazungumzo yao ya hapa na pale.

  Kiongozi wa msafara wa tamasha la 
Serengeti Fiesta 2012, Mully B akiwa na mastaa wa filamu, Wema Sepetu na
 Aunt Ezekiel afu fulllll BBM kama kawa.

 Wema Sepetu katika pozi na washabiki wake mapema mchana huu.

 Pichani ni Gari aina ya Vits 
itakayotolewa jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, kwa 
mshindi atakaejishindia kwenye droo itakayofanyika katika uwanja wa chuo
 cha ushirika, ambako tamasha hilo litarindima mpaka majogoo.

Mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo 
akiwa Live mapema leo mtaa wa Malindi katika mpango mzima wa amsha amsha
 kwa wakazi wa Moshi kuhusiana na tamasha la Serengeti Fiesta 2012, 
ambapo pia katika tamasha hilo kutatolewa zawadi mbalimbali ikiwemo gari
 ndogo aina ya Vits kama uinavyo pichani ikinadiwa vilivyo. 

Kawa kawa amsha amsha ya tamasha la 
Serengeti Fiesta pia linatoa mafuta kwa magari daladala,pikipiki 
sambamba na baji lita 10 ama tano kutoka kampuni ya GAPCO ambao pia ni 
sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment