Kumekuwa na mlipuko mkubwa katika mji mkuu wa Syria,
Damascus karibu na hoteli ambayo hutumiwa na wafnyakazi wa Umoja wa
Mataifa.
Runinga ya kitaifa ya Syria imesema kuwa lilikuwa shambulizi la bomu na kwamba watu watatu walijeruhiwa.Shirika la muungano wa nchi za Kiarabu OIC leo linatarajiwa kuliondoa taifa la Syria kama mwanachama wake kuhusiana na ghasia na machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo.
Wajumbe wa shirika hilo lenye wanachama 57, wanakutana katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Mecca na wanatarajiwa kuidhinisha azimio lililopitishwa na mawaziri wake wa nchi za kigeni kuhusu kutimuliwa kwa Syria kama nchi mwanachama wa muungano huo.
Serikali ya Iran imepinga vikali azimio hilo.
Runinga ya taifa imesema mlipuko huo ulisababisha na bomu lililokuwa limetegwa karibu na lori moja ya mafuta, lililokuwa limeegeshwa karibu na hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment